
Ndugu
yangu katika Imani Kaka yangu Mpendwa Dada yangu Mpendwa leo Inshallah
kwa Uwezo wake M/Mungu Mtukufu tunaingia katika Ukumbusho Mpya Niwaombe
wale Marafiki zetu na Ndugu zetu wageni warejee katika Post zetu
zilizotangulia ili tupate kwenda
sawa.Ukumbusho wetu leo utahusu au zungumzia Udhu na Kama Ada yetu
tunaangalia neno kwa Maana Mbili ya Lugha na Maana ya watu Sharia(Fiqh).
1.MAANA YA UDHU
Tamko/Neno udhu linafasirika katika lugha ya kiarabu kama wema, uzuri na ung'avu.
Ama maana ya udhu katika istilahi ya wanazuoni wa fani hii ya Elimu ya
Sharia (Fiqh) Udhu ni twahara inayotumia maji, twahara hii inahusisha
viungo maalum vya mwili, baadhi yake hukoshwa kama mikono, uso na miguu
na vingine hupakwa maji kama vile kichwa.
2.HUKUMU YA UDHU NA DALILI YAKE
Udhu kwa maana tulivyoieleza ni FARDHI/WAJIBU katika kusihi na
kukubalika kwa ibada ya swala kwani hapana swala bila ya udhu kwa maneno
mengine, tunaweza sema kuwa udhu ndio msingi mkuu na imara wa ibada ya
swala.
Udhu ndani ya Qur-ani unapatikana katika kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema :
"Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Swala basi osheni nyuso
zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni
miguu yenu mpaka vifundoni..." Qur an Suratil Maidah aya ya 6
Ama dalili na ushahidi wa udhu katika sunna ni ile kauli yake Mtume wa
Mwenyezi Mungu Rehma za M/MUNGU zimshukie Juu yake na amani aliposema "
Allah haikubali swala ya mmoja wenu atakapohuduthi kwa Maana kwamba
atakapo tengukiwa na udhu mpaka atawadhe (tena)" kama alivyosema Mtume
Hadithi imepokelewa na Maimamu wawili.
3.UBORA/FADHILA ZA UDHU
Ewe Ndugu yangu Kijana Mwenzangu tukumbuke kwamba zimepokelewa hadithi
nyingi kutoka kwa Bwana Mtume -Rehema za M/Mungu zimshukie juu yake na
Amani katika kutaja na kuonyesha ubora na fadhila za udhu miongoni mwa
hadithi hizo ni :-
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani
zimshukie juu yake "yeyote atakaye tawadha vyema ( kama alivyoelekezwa
na sharia), hutoka madhambi zake mwilini mpaka chini ya kucha zake"kama
alivyosema Bwana
Mtume Muslim.
Na katika Hadithi Nyengine Mtume (S.A.W)
amesema "Hakika umati wangu wataitwa siku ya Kiyama (mbele ya Mola
wao) hali ya kuwa wang'avu wa nyuso, mikono na miguu kutokana na athari
ya udhu, basi yeyote yule awezaye kurefusha mipaka ya viungo vyake
(katika kutawadha) na afanye hivyo." kama alivyosema Mtume Imepokelewa
Hadith na Imamu Muslim.
Ewe Ndugu yangu Mpendwa baada ya kujua haya
Inshallah azimia na tia Nia kuanzia sasa kushikamana na Udhu ili
zisikupite fadhila na Ubora wa Udhu kama tulivyo eleza Inshallah tuwe
pamoja katika Ukumbusho Ujao ambao tutaeleza Namna ya kutawadha.