Wednesday, July 31, 2013

WASIFU WA HABIB AHMAD BIN ABUBAKAR BIN SUMAYT, radhi za Mwenyezi Mungu zimwalie


Shaykh Abdallah bin Muhammad bin Swaleh Baakathir (radhi za Mwenyezi Mungu zimwalie), mmoja kati ya wanazuoni wakubwa wa zama zake alirushwa roho na jambo moja akiogopa sana kwamba watu wasifike hadi ya kutotambua neema kubwa waliyokuwa nayo. Akiogopa kwamba wakiacha kuitambua neema hiyo, hapatakuwa tena na shukurani na shukura ni kufuli ya neema. Ikifanywa shukura, neema hubakia. Zaidi kuliko hayo ni kwamba neema ile hustawi ikaingia na baraka. Na huvuta neema nyingine ambazo mtu kamwe hazikumpata kumjia katika mawazo yake. Kwani si anasema Azza-wa-Jaala, "lau matashukuru hakika hakika nitakuzidishieni”. Aya haifafanui kitakacho zidishwa ni kipi na wala kitazidishwa kwa kiwango gani. Na madamu hayo yanasemwa na Mola ambaye yeye mwenyewe kajiita Shaakhir, mwingi wa kushukuru, basi mawazo ni huria. Shaykh Abdallah Baakathir (radhi za Mwenyezi Mungu zimwalie) anataja dukuduku lake mwanzo wa kitabu chake cha al-Ashwaaq anasema hivi, “kupatikana mtukufu huyu na watu mithali yake katika zama hizi ni neema kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Anaitambua mwenye kuitambua na mjinga nayo, yule ambaye ni mjinga nayo. Tunamwomba Yeye taala atupe sisi tawfiqi ya kusimama na kushukuru neema zake zote zile za nje na ndani.
Na anaendelea kusema, “au wanazijua lakini wanazikataa na hawazishukuru.” Hapa Shaykh Abdallah anaashiria kuwa neema huwapo na mtu akaikataa.
Al-habib Ahmad bin Abubakar bin SumeitJe, neema hiyo anayoizungumzia Shaykh Abdallah Baakathir ni neema ipi? Hiyo ni neema ambayo pengine leo watu wa Unguja na Afrika Mashariki nzima wameisahau, nayo ni kuwepo kwa Al-Habib Ahmad bin Abi-Bakar bin Sumayt (radhi za Mwenyezi Mungu zimwalie) miongoni mwao.  Neema ambayo al-Habib Ahmad bin Umar bin Sumeyt (radhi za Mwenyezi Mungu zimwalie) alikwisha bashiria kuzaliwa kiasi miaka ishirini kabla ya ujudi wake. Na Leo ni Miaka thamanini na sita toka kutawafu kwake.
Shaykh Abdallah Baakathir anamweleze hivi basi, Shekhe wake, al-Habib Ahmad bin Abi-Bakar bin Sumayt mwanzo mwanzo wa kitabu chake cha al-Ashwaqq, "Bwana mwenye sharafa kuu na utukufu mkuu, aliyekunywa kifu yake ilmu zote zile za akili na kupokea, mwenye kukusanya fani za lugha fasaha, mtatuaji wa mishkeli na mtanzuaji wa mitata. Nadra wa zama na pambo la miji na Mufti wa pekee aliyekusanya ya fadhila na matukufu.... nilisoma kwake vitabu kadhaa wa kadhaa na huyu ni Bwana ambaye mazoe yake ni kutembea kwenye bustani za ilmu na ma’arifi na kuchuma hikma na zile ilmu zenye kufichika baina wino na ibara. Aliyepweke katika kuhakiki masaaili na mpweke wa zama zake katika kudiriki undani wake. Kawaswahibu ma-Qutbu na Mashekhe wakubwa wa zama zake, na mawalii ma-‘Arfina, wanazuoni wahakiki wa dahari yake. Na kwao kapata enga enga na malezi na madadi. Na  wao wakamshuhudia kwa matukufu walionayo na ukamilifu wake. Wakamhisabu kuwa yeye ni mmoja wapo ya rijali waliokamilia na wakamfungulia mapazia kumjulisha siri za tarika na hakika zilizomo humo. Na wakamnywesha kinywaji safi cha ilmu ladunniya. Kutokana na baraka zao Mwenyezi Mungu kadhihirisha mangapi kwenye ulimi wake na kalamu yake, yale ambayo yamefichika kwenye fahamu za wengine, na akamimina kwenye maji ya matamko yake matamu yale ambayo yanakonga kiu cha figo cha wanazuoni wa wanazuoni. Ana shuhudiwa kwamba katika ilmu za hakika na maarifi yeye ni Imamu na mzuri aliyoje kuwa Imam. Na kwamba yeye ni nguzo marji'i ya watengwa makhsusi na watu wa kawaida kwenye fani zote za lugha na pia sharia na hukumu.....”
Zaidi ya Shaykh Abdallah Baakathir, Habib Ahmad bin Sumayt alikuwa pia ni Shekhe wa Al-Habib Umar bin Ahmad bin Sumayt, Habib Abdulrahman bin Ubaydillah, Shaykh Sulaiman Alawy, Shaykh Hassan bin Amer na Shaykh Burhan Mkele, kuwataja kwa uchache. Wanazuoni wa zama, ambao matukufu yao hayahitaji kupigiwa debe.
                                     KWA MAKALA NYINGI ZAIDI TEMBELEA

MATUKUFU YA LAYLATUL-QADR

Al-Habib Ali Bin Muhammad Al-Habshy, radhi za Mwenyezi Mungu zimwalie.
k3Nimekuwa nikijuiza kwanini linaponijia jina la Shaykh Nurdiin bin Hussain bin Mahmoud Al-Ghassany, radhi za Mwenyezi Mungu zimwalie, huwa ni kope kwa nyusi na jina la al-Habib Ali bin Muhammad bin Hussain al-Habshy, radhi za Mwenyezi Mungu zimwalie? Ewa. Sasa naona.
Shaykh Nurdiin alikuwa ni Shaykh wa tarika ya Shadhilly kama Sayyidina Ibn ‘Atwaai-Llah as-Sakandari, radhi za Mwenyezi Mungu zimwalie, alivyokuwa Shaykh wa Shadhilly. Jina lake jingine Bwana huyo ni al-Imam, al-‘Arif bi-Llah Ahmad bin Muhammad bin Abdulkarim.  Kuna mengine yanayowaunganisha hawa watatu. Lakini hayo si ya leo. La leo ni kwamba Sayyidina Ibn ‘Atwaai-Llah ash-Shadhilly ni tarika moja na  Shaykh Nurdiin bin Hussain. Aliandika kitabu juu a Shaykh wake al-Imam Abi-l-‘Abbas Ahmad bin Umar al-Mursii, radhi za Mweneyzi Mungu zimwalie.
Habib Ali al-Habshy MosqueWasifu anaoutoa kumfafanua Shaykh wake ni karibu wasifu ule ule anayeutoa al-Imam, Shaykh Abdallah bin Muhammad bin Salim Baakathir, radhi za Mwenyezi Mungu zimwalie, kumfafanua Shaykh wa Shaykh wake, al-Habib Ali bin Muhammad bin Hussain al-Habshy.  Yale ambayo Mwenyezi Mungu kamfungulia Ibn ‘Atwaai-Llah kuyaona kwa Shaykh wake Abi-l-‘Abbas al-Mursii ni yale yale ambayo Mwenyezi Mungu kamfungulia Shaykh Abdallah Baakathir kuyaona kwa Shaykh wa Shaykh wake, Habib Ali al-Habshy, jamali ya kupigiwa mfano, jalali isoweza kuchanganyishiwa macho, ilmu zenye kuduwaza akili na akhlaqi za juu na rehema na shafaka kubwa juu a umma wa Mtume, swalla-Llahu aalay wa Ssalaam.
Ni kwa Habib Ali al-Habshy basi ndiyo kwenye ukurasa wa leo tunakwenda kumsikiliza, atufahamishe yale makuu ya Laylatul-Qadr.
بِسْمِ اللهِ  الرَّحْمَنِ الرَّحِيم
Himdi zote zinamhakia Mwenyezi Mungu ambaye liko juu neno Lake na hoja Yake ndiyo mwisho wa hoja, Mola ambaye ni ya wasaa Rehema Yake, na Neema Yake ni yenye kukunjuliwa juu ya viumbe wote, Mwenye kulingania waja kwenye tawhidi Yake. Wakamjibu wale waja Wake waliopewa tawfiqi. Na akawaita kwenye twaa Yake. Na wakafanya haraka kuitikia wito huo, wale walio halisi kwenye mapenzi Yake, na watashi wa kweli wa pendo Lake.
Kazifanya neema namna namna na kajalia wakati maalum wa kudhihiri athai za neema hizo kwenye wujudi. Kwa hivyo hakuna zama zezote zile isipokuwa Mwenyezi Mungu anayo mumo siri kubwa ambayo hushuka kwa mujibu wa takdiri Yake na wakati alioiwekea.
Na kautukuza mwezi wa Ramadhani juu ya miezi mingine kwa mambo makhsusi na akashusha humo Qur’ani, uongofu mkubwa kwa watu na ubainifu mkuu. Ikadhihiri siri hiyo kwenye  mawahibu yenye kushuka kwenye zama hizi tukufu, kulingana na kushushwa Qur’ani humo kutoka hadhra ya Mola yenye kubainisha taklifu za ibada na kuzifafanua. Ni Yeye basi Subhannak – Aliye takata na mawii, Mfalme alioje, Aliye unganisha sababu na matokeo yake. Tena akazipitisha aqdari kama alivyosajili kwenye Mama wa Vitabu. Na nakiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kwamba hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Mfalme ambaye wamenyenyekea kwa utisho wake wafalme, na Karimu ambaye enga enga Yake imemvaa anayejiweza na yule asio kitu. Na nakiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kwamba Bwana wetu Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake na mpenzi Wake, ambaye iqbali Yake kwake na kabuli Yake ni jambo lililo hakikishwa, Mwenyezi Mungu amswaliye na amsalimiye, na amzidishie sharafu na ikramu mbele Yake, azihusishe swala hizo tukufu na taslima zilizo latifu kwa Aali zake watukufu, na ma-Swahaba zake wajuzi, na wale waliosimama kwenye njia yao iliyonyooka.
Enyi waja wa Mwenyezi Mungu nakusieni nyinyi na nafsi yangu kwa taqwa ya Mwenyezi Mungu. Mwenye sada na sudi njema kweli ni yule mwenye kutekeleza ahkami Zake na akajikunjulia nje na ndani alama Zake tukufu. Na hizo, tutanabahi na tujue, ni kutekeleza yale ambayo Mwenyezi Mungu kaamrisha na kukatazika na yale ambayo kayakataza na kayakataza kwa ukali.
Basi kwa umri wangu, hiyo ndiyo njia yenye kumfikisha mtu kwenye radhi za Mwenyezi Mungu na njia iliyokusanya namna zote za mema na atiyya zake kocho kocho. Basi yule mwenye kuwajibika nayo itamkusanya yeye chanda kwa pete kwenye kheri za Dunia na Akhera na ataishi kwenye Baraka Zake, za nje na ndani.
Zaidi ya hayo hakika nyinyi, Mwenyezi Mungu akuwafikisheni mko katika mwezi, ambamo Mwenyezi Mungu kakunjua katika mwezi huo, kutoka maandalio ya u-Karimu Wake, kakunjua busati la maghfira na akafungua humo kwenye hazina za Wema Wake, milango ya ihsani.
Mawingu mangapi, na Akajaalia yaangushe mvua za Fadhila Yake kwenye mwezi huo, (zikaanguka) kwa yule aliyepigwa na ukame, na zidhihiri ndani yake papo kwa papo alama za uhai.
Na katika mwezi huo ihsani za u-Karimu Wake zimeokoa  wangapi wale waliozama kwenye maasi, na la si ukarimu huo basi moto wa jahimu ndiyo ungekuwa maskani yao ya mwisho.
Na uwe wenye baraka kwenu basi huo mwezi adhimu ambao masiku yake ni mataa kwa wote, na michana yake ni michana ya furaha, kwa sababu ya twaa ya Mwenyezi Mungu tangu Dhikri na Tilawa na Swaumu.
Furaha kubwa iliyoje hiyo ambayo matunda yake ni furaha ya daima dawamu kwenye darii ya salama.
Basi mshukuruni Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu akurehemuni, kwa neema hii iliyokunjuliwa. Na jitahidini kwa amali njema inayokubalika mbele ya Mwenyezi Mungu kwa sababu matunda ya jaza njema huumana na amali njema. Na jikingeni katika wakati huu mtukufu msijitupe kwenye wimbi la maasi. Kwa sababu kwenye zama tukufu mizigo ya machafu hulipwa marudufu kama thawabu za mema zinavyotolewa maraudufu. Kuweni basi na hadhari kubwa msije mkafungulia milango ya ghadhabu za Mwenyezi Mungu na adhabu yake yenye maumivu makali.
Kwa sababu yule ambaye haachi kauli ya kuongopa na amali yenye kukamatana nayo, basi Mwenyezi Mungu hana haja kamwe na kuwacha kwa mja huyo chakula chake kitamu na kinywaji chake.
Na shaitwani kalipambia kundi lake lilo khasirika, yale mambo ambayo yatawatia kwenye fedheha siku ya mwisho. Kwa hivyo kuweni na hadhari na adui huyo na mtindo wake wa kupamba amali mbaya, na ombeni msaada kwa Mwenyezi  Mungu akulindeni na vitimbi vya adui huyo na mpangilio wa hila zake, na zile njia anazopitia kukuharibieni amali zenu na kauli pamoja na niya.
Na juweni kwamba mwezi wa Ramadhani ni mwezi adhimu. Huwapeleka wenye kuuamirisha, kwa amali njema, kwenye Pepo za Naimu. Mwezi adhimu ambao Qur’ani umetaja fadhila zake na Sunna pia.
Neema ngapi Mwenyezi Mungu anazitoa kwa upya, na upya tena kutupa sisi kwenye mwezi huu. Kati ya mambo ambayo ni yake mwezi huu, ni ule usiku ambao ni bora kabisa kuliko miezi alfu. Tanabahini mjue hiyo ni Laylatul-Qadr. Na utaijuaje, Laylatul-Qadr ndiyo ipi. Ni amani adhimu, inayoendelea mpaka kuchomoza kwa al-Fajiri.
Sunna imetaja fadhila zake, yale ambayo kwayo imani ya waumini huzidi na nyoyo za wenye kuwafikiwa hukunjuka.
Kati ya yaliyo pokewa makhsusi kwa yule mwenye kusimama kwa ibada kwenye Laylatul-Qadr, hali ya kuwa ana amini vilivyo na kwa sababu anataka fadhila za usiku huo, huyo hughifiriwa dhambi zake zilizo tangulia na zile za baadae.
Na Bibi Aisha, Radhy-Allahu ‘Anha kasema kwamba, ‘usiku huo ni usiku wa tarehe kumi na tisa.’ Basi fanyeni ukomo wa uwezo wenu kuipata bidhaa hiyo.
Na imetajwa kuhusu fadhila za mwezi wote kwenye Hadithi iliyopokewa na Abii Masoud al-Ghifaariyyi, Radhy-Allahu ‘Anhu kwamba yeye amemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, swalla-Llahu aalay wa Ssalaam akisema, siku ulipoandama mwezi wa Ramadhani, “lau waja walijua yaliyomo kwenye mwezi wa Ramadhani, basi waja wangelitamani mwezi wa Ramadhani uwe mwaka mzima.... mpaka mwisho wa hadithi.
Na katika yale yaliyopokewa kutokana na Salman, Radhy-Allahu’Anhu kuwa alisema, “alituhutubia Mtume wa Mwenyezi Mungu swalla-Llahu aalay wa Ssalaam, siku ya mwisho ya Shaaban na akasema, ‘enyi watu umekufunikeni nyinyi mwezi adhimu, mwezi mkuu wa baraka kuu. Mwezi ambao ndani yake una usiku ulio bora kuliko miezi alfu. Amejalia Mwenyezi Mungu kuufunga mwezi huo ni jambo la faradhi na kusimama kwa ibada jambo la khiyari. Mtu mwenye kutafuta mkuraba kwa Mwenyezi Mungu humo kwa jambo la kheri au katekeleza faradhi, huwa kana kwamba kafanya faradhi sabini katika miezi isyokuwa huo. Nao ni mwezi wa subira na subira thawabu zake ni Pepo.
Na huo ni mwezi wa kutekelezeana haja, na mwezi ambao mumo rizki ya muumini huzidishwa. Basi yule mwenye kumfuturisha mwenye kufunga mwezi huo, hayo huwa ni maghfira kwa dhambi zake na shingo yake kuachiliwa huru kwa moto. Naye hupata thawabu kama za yule pasina kupunguka chechote kile katika ujira wake.
Walisema, “si yeyote yule miongoni mwetu anayepata kile cha kumfuturisha mwenye kufunga.” Akasema, “Mwenyezi Mungu humpa thawabu hizi yule mwenye kumfutarisha mwenye kufunga, kwa Tende au gao la Maji au Maziwa kidogo. Nao ni mwezi mkuu. Mwanzo wake ni Rahma, kati yake ni Maghfira na mwisho wake shingo kuachiwa huru na moto.
Yule mwenye kumfanyia mtumwa wake mambo wepesi katika mwezi huo, Mwenyezi Mungu humghufiria na akamwacha huru na moto.
Basi fanyeni kwa wingi katika mwezi huo mambo manne. Mambo mawili, kwayo mtamridhisha Rabbu wenu. Na mawili mengine, hayo hamna budi nayo.
Ama yale mawili ambayo kwayo mtamridhisha Rabbu wenu ni ile shahada ya Llaa-Illaha illa-Llaa na kumwomba maghfira Mwenyezi Mungu.
Ama mawili ambayo kwayo nyinyi hamna budi nayo ni, (kwamba) mtamuomba Mwenyezi Mungu Pepo na kwaye mjalinda na Moto.
Na mtu mwenye kumpa mwenye kufunga chakunywa, Mwenyezi Mungu atamnywesha mtu huyo kwenye hodhi Langu, kinywaji ambacho baada ya hapo, mtu huyo kamwe hatoshikwa na kiu.”
Basi zingatieni hayo Mwenyezi Mungu akurehemuni,  ya  fadhila ambayo yamo kwenye mwezi huu na yale yanayozalika ya amali njema yenye kukubalika mbele ya Mwenyezi Mungu. Na kuweni nyinyi watu walioshikamana na njia ya wenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na wenye taqwa Yake. Na jitahidini nyinyi mwezi ukuondokeeni hali kurasa za madaftari yenu zimejaa mema na nje yenu na ndani yenu zimehifadhika na mambo yanayo kwenda kinyume na sharia.
Sehemu kubwa ya mwezi imekwisha pita na umewadia wakati wake wa kuondoka kwenu na kuendelea na safari yake. Je, mwezi umekufikisheni kwenye hazina zake, au umekufunulini siri zake, na au umezusha ndani yenu ninyi toba ya dhati kwa dhambi zilizopita na mabaya yenye kufuata?
Kwani hakika, hakika dalili za kupata kabuli kudhihiri kwenye udhati wa iqbali na kumuogopa Mwenyezi Mungu ndiyo dalili yenye nguvu kupita zote yenye kuthibitisha kwamba hali imo katika istikama.
Na katika kupita siku za mwezi huu kuna mazingatio kwa upande wenu, ikiwa mtazingatia. Na makumbusho kwenu vile vile, lau mtakumbuka. Kwa sababu hakika, hakika siku hizo zitahisabiwa kuwa ni sehemu ya umri wenu na kwenye kurasa zenu hayo yataandikwa. Basi zingatieni hayo enyi ndugu zangu. Na simameni kidete kwenye amali njema zenye sifa ya kukubaliwa na Mwenyezi Mungu na rudini nyuma, msiyaingie maasi katika zama na nyakati zinazokukabilini. Kwa sababu, hakika, hakika nyinyi mmo kwenye safari mnaiaga dunia na Akhera ndiko mnako kwenda. Na mtakapofika Akhera, hapo itakubainikieni waziwazi, ipi biashara yenye faida na ipi ile ya hasara.
Kwa hivyo jiandaeni kwa nyumba hiyo inayokabili, kwa maandalio yaliyo kamilia. Na jitahidini kwenye twaa ya Mwenyezi Mungu upeo wa kujitahidi. Na uchukulieni fursa umri wenu wenye kutoweka, kwa yale ambayo yatakuleteeni raha ya milele, na kukusanyeni nyinyi na fadhila za Mwenyezi Mungu hali mna madadi iliyo kamilia kupita zote. Kwa sababu hakika, hakika, mja aliye wafikiwa ni yule ambaye anatumia nyakati zake zenye kupita katika yale mambo ambayo yatampatia yeye maisha ya milele kwenye nyumba ya maziidi. Kwa sababu nyumba ya Akhera imefichwa kwenu na hamjuwi alama zake. Utakukuteni nyinyi, na hilo lisiwe na shaka, unyonge wake ama utukufu wake. Yatakukabilini nyinyi, mtaposhuka huko, yale ambayo huotesha mvii wana wa mkononi, na itakukumbeni nyinyi kitapo, zama za kushuka huko, ambacho hata majabali hawamudu kukibea. Je, kwa mazito hayo yenye kusakama koo, mnayo maandalio? Na je, kwa safari ndefu hiyo mmetanguliza zawadi za njiani?
Basi tanabahini kabla majuto hayajawa mjukuu na mguu haukukutieni kwenye telezi, na kabla ya kalamu haijakauka juu ya lile ambalo limekwisha kuandikwa kuhusu hatima yenu.
Basi toba na tena toba, Mwenyezi Mungu akurehemuni toba dhidi ya machafu kabla hamjanywa manywaji ya unyonge, na kuingi kwenye shamla baina yenu na wanafiki, na waouvu kwenye makao mabaya kabisa, na nyumba yenye kutisha kabisa.
Hasara kubwa ilioje ni ya yule ambaye mizigo ya maovu ndiyo zawadi yake ya njiani na maasi ndiyo sifa yake na ada yake.
Hatima ya hali yake huyo ni mbaya, tena mbaya na watu wa hali hiyo hawana thamani kwenye masoko ya saada na sudi njema ya abadi na abadi.
Ni kweli mwenye akili na uoni wa jicho la ndani ataridhia afike kwenye mkusanyiko wa kiyama na sura yake ni mbovu kupita sura zote, na aingie kwenye fedheha katika hadhara hiyo kwa sababu ya yale maovu aliyoyachuma?
Kwani ni vizuri itambulikane kwamba hizaya yasiku hiyo ni hizaya mbovu kweli na makazi ya wenye dhambi humo ni makazi mabaya kweli.
Hakimu Mwadilifu atadhihiri kwa maangamizo. Na itadhihiri mumo kwa watenda madhambi mwisho mbaya wa pahali hapo. “Siku itakapobadilishwa ardhi na kuwa ardhi nyigine sio hii, na mbingu pia. Na wao watahudhuria mbele ya Mwenyezi Mungu mmoja asio na mshirika, mwenye nguvu. Na utawaona waliokwenda kinyume na maamrisho siku hiyo wamefungwa kwenye minyororo. Nguo zao ni za lami na nyuso zao zimegubikwa kwa moto. (Na hayo) ili Mwenyezi Mungu ailipe nafsi yeyote ile iwayo ile iliyoyachuma (Ibrahim, Aya 48-50).” “Siku hiyo mtahudhurishwa  - haitofichika siri yeyote yenu ile iliyofichika. Basi ama yule atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia atasema; haya nisomeeni kitabu changu. Hakika nilijuwa ya kuwa nitapokea hisabu yangu. Basi yeye atakuwa katika maisha ya kuridhisha (al-Haqqa 18-21).Na ama yule atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kushoto huyo atasema laiti nisingalipewa kitabu changu wala nisingalijua nini hisabu yangu. Lati mauti ndiyo yangelikuwa yakunimaliza moja kwa moja. Mali yangu haikunifaa kitu kamwe, Usultani wangu umeniangamilia (al-Haqqa 25-29).
Je mmejua enyi ndugu zanguni haki ya siku hiyo na yale malipizo yatakayodhihiri humo, na kwa hivyo mkawa katika nyumba hii mnaifuata ile njia ya kumuogopa Mwenyezi Mungu na kuwa na taqwa Yake? Kwa sababu hatima ya watu wa pote hilo ni hatima ya salama na mwisho wao ni kwenye nyumba ya milele. Nyumba nzuri iliyoje nyumba hiyo. Mumo kuna Naimu ambayo haiwezi kudirikiwa na akili wala macho, “na wakatiwa wale wenye kuamini na kutenda amali njema, zenye sifa ya kukubaliwa na Mwenyezi Mungu, kwenye Pepo kuu ambamo chini yake inapita mito.”
Je hamyajui mambo hayo ya siku hiyo? Na ikiwa ni hivyo basi yenu ni hasara iliyofunika hasara zote, “sema; stareheni, kwani hakika hakika mwisho wenu ni motoni. Jahanamu wataiingia na makazi yaliyoje hayo.”
Mwenyezi Mungu atusalimishe sisi na nyinyi na vitisho vya nyumba hiyo na atuhifadhi sisi na nyinyi na yale yatoleta unyonge na fedheha, na Atushike sisi mkono sote kwenye mwezi huu mtukufu na umri uliobaki, Atushike mkono kwenye jua ya waja wake aliowapa mkuruba Naye, na watenda zema.
Ewe Allahumma, Ewe Mola Karimu, Mwenye kutoa pasina kungoja ukaombwa, Ewe Wahhaabu, Mpaji msikikomo katika upaji Wako, Ewe Rahimu, Mrehemevu, Ewe Tawwaabu, Mwingi wa kumpa toba mja wako hata akatubia, Nawe ukawa Mwingi wa kupokea toba, tena na tena.
Sifa Yako ni Rehema na Ukarimu, na athari za hayo ziwazi kweupe katika wujudi. Ikiwa nyuso zetu zinapiga weusi kwa dhambi na kufanya mambo kinyume na maamrisho, basi tegemeo letu za kunawirishwa nyuso hizo zikapata weupe, tegemeo letu ni juu ya Ukarimu Wako. Ewe Mwenye kukubali toba ya waja Wake na Mwenye kusamehe maovu, mlangoni Kwako tumesimama, na Wema Wako tunauomba, na tamaa haiwi njema isipokuwa Kwako tu, na maombi, haliwi jambo lililo ndilo ila yakifanywa Kwako.
Tunakuomba kwa ndimi ambazo kwa muda mrefu kwazo tumekuasi. Na tunaelekea Kwako kwa nyoyo na viungo, ambazo kwa muda mrefu tumefanya maovu mbele Yako. Na lau si wingi mkuu wa madadi Yako kuu na furifuri ya hilmu Yako adhimu, ambazo kwazo Ume-tuamili na sisi tumo katika hali hiyo, kamwe tusingejistirisha kutaka na kuomba. Lakini dhana njema Kwako ndiyo iliyotasua ndimi zetu kwa maombi. Na kutupa sisi bishara njema kwamba tutayafikia tunayoyataka na tutayadiriki malengo yetu, hasa hasa kwa kuwa sisi tuna wasila Kwako, nao ni Mja Sharifu kupita wote uliyemsogeza Kwako, Bwana wetu al-Habib, alo adhimu, mwenye raafa, mwingi wa rehema, Habibi Wako ambaye umemteua akawa na cheo cha juu kuliko kila Habibi, na mtengwa Wako ambaye umemnyanyua na kumweka kwenye cheo kitukufu kupita vyote kwenye hadhara za mkuruba, muombezi mkuu kupita wote, na Mtume mtukufu kupita wote, Bwana wa Mitume mursali na Mtume wa mwisho wa Mitume yote, Bwana wetu Muhammad bin Abdillah, mkweli, muaminifu.
Ni huyo ndiye tunatanguliza jaha yake Kwako, na kwaye tunaomba uombezi wake, ili amali zetu zipate kabuli na dhambi zetu zighufiriwe.
Tunakuomba Ewe Allahumma, kwa cheo ulichompa mbele Yako uumpe shafaa juu yetu na umsalie Yeye kamilifu kabisa ya swala na timilifu kupita zote, na yenye sharafa kupita zote, na yenye ku’umu kupita zote. Na swala hiyo iwafunike Aali zake wote, na Sahaba zake watukufu, na wale wenye kwenda mwendo wake ulionyooka na wenye kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu, na salamu juu ya Mitume mursali wote. Na himdi zote zile zinamhakia Mwenyezi Mungu pekee na Rabbi wa viumbe piya.
 KWA MAKALA NYINGI ZAIDI TEMBELEA : www.mwinyibaraka.com

FATAWA N NAWAWI



الكتاب: فَتَّاوَى الإِمامِ النَّوَوَيِ المُسمَّاةِ: "بالمَسَائِل المنْثورَةِ

المؤلف: أبو زكريا محيي الدين يحيى بن شرف النووي (المتوفى: 676هـ

  ترتيبُ: تلميذه الشيخ عَلَاء الدِّين بن العَطّار 
 
تحقِيق وتعلِيق: محمَّد الحجَّار

  الناشر: دَارُ البشائرِ الإسلاميَّة  للطبَاعَة وَالنشرَ والتوزيع، بَيروت - لبنان 

  الطبعة: السَادسَة، 1417 هـ - 1996 م  

عدد الأجزاء: 1
                                              Download hapa kama Umekipenda

Zakaat al-Fitr

Zakaat al-Fitr 

(Importance and When to give)

Zakaah al-Fitr is often referred to as Sadaqah al-Fitr. The word Fitr means the same as Iftaar, breaking a fast and it comes from the same root word as Futoor which means breakfast. Thus, Islamically, Zakaah al-Fitr is the name given to charity which is distributed at the end of the fast of Ramadaan.

Sadaqah al-Fitr is a duty which is Waajib on every Muslim, whether male or female, minor or adult as long as he/she has the means to do so.

The proof that this form of charity is compulsory can be found in the Sunnah whereby Ibn `Umar reported that the Prophet (sallallaahu `alaihi wa sallam) made Zakaah al-Fitr compulsory on every slave, freeman, male, female, young and old among the Muslims; one Saa` of dried dates or one Saa` of barely. [collected by Bukhari - Arabic/English, vol. 2, p. 339, no. 579]

The head of the household may pay the required amount for the other members. Abu Sa'eed al-Khudree said, "On behalf of our young and old, free men and slaves, we used to take out during ALLAH's Messenger's (sallallaahu 'alaihi wa sallam) lifetime one Saa` of grain, cheese or raisins". [collected by Muslim - English transl. vol. 2, p. 469, no. 2155]

WHEN TO GIVE ZAKAAT AL FITR
Ibn ‘Umar (may ALLAH be pleased with him) said: They used to give (zakaat) al-fitr one or two days before (Eid). Narrated by al-Bukhaari (1511).

Zakaat al-fitr must be paid before the Eid prayer, because of the report narrated by Abu Dawood (1609) and Ibn Majaah (1827) from Ibn ‘Abbaas (may ALLAH be pleased with him) who said: The Messenger of ALLAH (peace and blessings of ALLAH be upon him) enjoined zakaat al-fitr as a purification for the fasting person from idle and obscene talk, and to feed the poor. Whoever pays it before the (Eid) prayer, it is accepted zakaah, and whoever pays it after the prayer, it is (ordinary) charity

KIWANGO CHA ZAKKATUL - FITRI NCHINI MISRI 6LE


مفتي الجمهورية: الحد الأدنى لقيمة زكاة الفطر 6 جنيهات تخرج قبل صلاة العيد عن كل فرد
ــــــــــــــــــــــــــ
حدد فضيلة الأستاذ الدكتور ‫#‏شوقي_علام‬ ‫#‏مفتي_الجمهورية‬ قيمة ‫#‏زكاة_الفطر‬ لهذا العام بما لا يقل عن 6 جنيهات عن كل فرد، مشيراً إلى أنه يستحب للمستطيع أن يزيد عن تلك القيمة

وأوضح في بيان له أن قيمة زكاة الفطر تعادل 2كيلو و 40 جرام من القمح عن كل فرد
وأشار فضيلته إلى أن دار الإفتاء مالت إلى الأخذ برأي الإمام أبي حنيفة في جواز إخراج زكاة الفطر بالنقود بدلاً من الحبوب تيسيراً على الفقراء في قضاء حاجاتهم ومطالبهم، كما أنها تحدد هذه القيمة كل عام عن كل فرد في الوقت المناسب لذلك

وأكد مفتي الجمهورية على ضرورة إخراج زكاة الفطر قبل موعد ‫#‏صلاة_العيد‬، وذلك لنيل أجرها، وحتى يتيسر للمحتاجين الاستفادة منها، وبين أن إخراجها بعد صلاة العيد يعد صدقة من الصدقات ولا تجزئ عن زكاة الفطر

المركز الإعلامي لدار الإفتاء المصرية

Tuesday, July 30, 2013

NGUZO YA IHSANI

NGUZO YA TATU NA YA MWISHO NI YA  IHSANI.

Na Nguzo yake ni Moja nayo ni:-

1.Kumuabudu Allah kama unamuona Kama humuoni yeye anakuona wewe.

Huu kwa muhtasari ndio Uislamu, dini na mfumo sahihi na kamili wa maisha kwa wanadamu wote waliochaguliwa na Allah Mola Muumba wao:

Rejea Dalili ya Aya Qur an 

"… LEO NIMEKUKAMILISHENI DINI YENU NA KUKUTIMIZIENI NEEMA YANGU NA NIMEKUPENDELEENI UISLAMU UWE DINI YENU...” (5:3) 

tuelewa na tufahamu kwamba kuishi nje ya dini hii ni kulikana umbile lako kwani UISLAMU NI HAKI YAKO YA KUZALIWA uliyopewa hadiya (zawadi) na Mola Muumba wako.

"Kila chenye kuzaliwa huzaliwa katika UISLAM ..." Kama alivyosema Mtume .

Angalizo 

Ewe Kijana wa Kiislam mpaka hapa  tutakuwa tumefahamu kwa Muhtasari (ufupi).

1.NGUZO ZA UISLAMU
2.NGUZO ZA IMANIE.
3.NGUZO YA IHSAN

Tunawatakia Funga Njema na yenye baraka na M/Mungu atujaalie wenye kuudiriki Usiku wa Laylatul Qadir (Usiku wa cheo ) katika Ibada .

Nguzo za IMANI

Jikumbushe

hii ni Nguzo ya Pili ya Dini ya Kiislamu inajengeka juu ya nguzo sita zifuatazo


1.Kumuamini Allah
2.Kuwaamini malaika wa Allah.
3.Kuviamini vitabu vya Allah.
4.Kuwaamini mitume (wote ) wa Allah.
5.Kuamini siku ya mwisho.
6.Kuamini qadari (Uwezo) wa Allah ( ya kheri au ya shari) kuwa inatoka kwa Allah .

hizi Sita Ndio Nguzo za Imani ...

NGUZO ZA UISLAMU

Jikumbushe Ndugu yangu Muislamu kuwa

Nguzo za Uislam ziku Tano

1.Kutamka Shahada Mbili

2.Kudumisha Swala

3.Kutoa Zakkah

4.Kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

5.Kuhiji Makkah kwa Ajili ya Ibada ( kwa Mwenye uwezo ) .

JIKUMBUSHE ZAIDI KUHUSU SWALA .

Swala ndio ibada ya kwanza kabisa aliyo iwajibisha M/Mungu Mtukufu kwa waja wake katika ule usiku Mtukufu wa Israa na Miraji.

Na ndio ibada pekee aliyopewa Mtume Mbinguni bila ya Ukati wa Malaika Jibrilu (Malaika ambaye kazi yake kushusha Wahyi kwa Mitume) kwani ibada nyingine zote alipewa hapa hapa duniani kupitia kwa Malaika Jibrilu-Allah amshushie amani.

Ibada ya Swala NDIO NGUZO KUU YA DINI YA UISLAM ....

AKHERA NI BORA KULIKO DUNIA

Tunapokuwa tuna furahia Maisha kwa kuwa na Gari nzuri , Nyumba Nzuri , Kitanda kizuri , Simu Nzuri ya HTC , Blackberry , Laptop za Model tofauti , Kadi za ATM katika Benki tofauti na Uwezo wa kubadili chakula cha Kila aina  tutakayo TUKUMBUKE kuilinda FURAHA HIYO YA HAPA DUNIANI NA KESHO AKHERA KWA CHUMO LILO HALALI.

Bora kutembea na Miguu, Baskeli , Kulala katika Nyumba isiyo na Umeme na kutumia Simu ya Tochi kuishi bila ya kuwa na ATM Card za Benki TUKUMBUKE  kuwa Chumo la halali ni Bora kwa %100 kuliko kuwa na FURAHA AMBAYO CHANZO CHAKE NI MALI ZA HARAMU.

AKHERA NI BORA KULIKO DUNIA 

Ewe M/Mungu tunakuomba tujaalie Rizki za halali na tufanye wenye kutosheka na kidogo tujaalie Dunia iwe kwa Mikono yetu na wala isiwe kwa Mioyo yetu Tusamehe Makosa yetu na Zipokee Dua zetu . Amiin

Majina ya Maswahaba 10 Wa Mtume waliobashiriwa Pepo.


Ewe M/Mungu tujaalie nasi kuwa Miongoni Watu wa Peponi na wazazi wetu waliotangulia Mbele ya Haki.








Majina ya hao Maswahaba 10 ni :-

1.Abuu bakar Siddiq
2. Omar Bin Khattab
3. Uthman Bin Affan
4. Ali Bin Abi Talib
5.Talha Bin Ubaidullah
6. Saeed Bin Zaid
7. Abuu Ubaidah Bin Jarrah
8. Zubair Bin Awwam
9. Saad Bin Abi Waqqas
10.Abdul Rahman Bin Auf

MUONGOZO WA MANENO YA WAJA WEMA


RAMANI YA TANZANIA KWA LUGHA YA KIARABU

Chuo cha Azhar Shareef CAIRO - MISRI


Jengo la Ofisi ya  Mkuu wa Chuo cha Azhar Dr Ahmad Tayb , Darrasa Cairo.

Msikiti wa Azhar - Hussein
Jengo la Shule ya Azhar Msingi na Sekondari Cairo - Misri 


                                Picha kwa hisani ya Mwanahabari : Amir Maine

DUA


اَللَّهُمَّ افْتَحْ لِيْ فِيْهِ أَبْوَابَ فَضْلِكَ وَ أَنْزِلْ عَلَيَّ فِيْهِ بَرَكَاتِكَ وَ وَفِّقْنِيْ فِيْهِ لِمُوْجِبَاتِ مَرْضَاتِكَ وَ أَسْكِنِّيْ فِيْهِ بُحْبُوْحَاتِ جَنَّاتِكَ يَا مُجِيْبَ دَعْوَةِ الْمُضْطَرِّيْنَ


O Allah throw open the doors of Thy generosity for me in this month, and make available to me multiplying blessings, keep me attached with that which obtains Thy pleasure, allot a central place for me right in the middle of the Paradise, O He who hears the cries of the distressed needy.

حكم إفطار المرضى وما الواجب عليهم

أجمع أهل العلم على إباحة الفطر للمريض، لقوله تعالى: "شهر رمضان الذي أنزل فيه القرآن هدى للناس وبينات من الهدى والفرقان، فمن شهد منكم الشهر فليصمه، ومن كان مريضًا أو على سفر فعدة من أيام أخر، يريد الله بكم اليسر ولا يريد بكم العسر
السؤال:  السلام عليكم ورحمة الله وبركاته: لي أب مريض معي في البيت وعنده ظروف صحية صعبة تمنعه من الصيام وكنت أريد أن أعرف من فضيلتكم  ما حكم إفطار المريض
وما الواجب عليه؟ جزاكم الله خيرا


د. يوسف القرضاوي

الحمد لله والصلاة والسلام على رسول الله ومن والاه وبعد

فقد أجمع أهل العلم على إباحة الفطر للمريض، لقوله تعالى: "شهر رمضان الذي أنزل فيه القرآن هدى للناس وبينات من الهدى والفرقان، فمن شهد منكم الشهر فليصمه، ومن كان مريضًا أو على سفر فعدة من أيام أخر، يريد الله بكم اليسر ولا يريد بكم العسر" (البقرة: 185).

فبالنص والإجماع يجوز الفطر للمريض، ولكن ما المرض المبيح للفطر، إنه المرض الذي يزيده الصوم، أو يؤخر الشفاء على صاحبه، أو يجعله يتجشم مشقة شديدة، بحيث لا يستطيع أن يقوم بعمله الذي يتعيش منه ويرتزق منه، فمثل هذا المرض هو الذي يبيح الفطر، قيل للإمام أحمد: متى يفطر المريض ؟ قال: إذا لم يستطع . قيل له: مثل الحمى ؟ قال: وأي مرض أشد من الحمى ؟ وذلك، أن الأمراض تختلف، فمنها مالا أثر للصوم فيه، كوجع الضرس وجرح الأصبع والدمل الصغير وما شابههما، ومنها ما يكون الصوم علاجًا له، كمعظم أمراض البطن، من التخمة، والإسهال، وغيرها فلا يجوز الفطر لهذه الأمراض، لأن الصوم لا يضر صاحبها بل ينفعه، ولكن المبيح للفطر ما يخاف منه الضرر

والسليم الذي يخشى المرض بالصيام، يباح له الفطر أيضًا كالمريض الذي يخاف زيادة المرض بالصيام . وذلك كله يعرف بأحد أمرين: إما بالتجربة الشخصية، وإما بإخبار طبيب مسلم موثوق به، في فنه وطبه، وموثوق به في دينه وأمانته، فإذا أخبره طبيب مسلم بأن الصوم يضره، فله أن يفطر، وإذا أبيح الفطر للمريض، ولكنه تحمل وصام مع هذا فقد فعل مكروهًا في الدين لما فيه من الإضرار بنفسه، وتركه تخفيف ربه وقبول رخصته، وإن كان الصوم صحيحًا في نفسه، فإن تحقق ضرره بالصيام وأصر عليه فقد ارتكب محرمًا، فإن الله غني عن تعذيبه نفسه . قال تعالى : "ولا تقتلوا أنفسكم . إن الله كان بكم رحيما". (النساء: 29

 هل يجوز للمريض أن يتصدق بدل الأيام التي أفطرها؟

المرض نوعان: مرض مؤقت يرجى الشفاء منه وهذا لا يجوز فيه فدية ولا صدقة، بل لابد من قضائه كما قال تعالى: "فعدة من أيام أخر" فإذا أفطر شهرًا فعليه شهر وإذا أفطر يومًا فعليه يوم، فإذا أفطر أيامًا فعليه أن يقضي مثلها حين يأتيه الله بالصحة وتتاح له فرصة القضاء .. هذا هو المرض المؤقت

أما المرض المزمن فحكم صاحبه كحكم الشيخ الكبير والمرأة العجوز إذا كان المرض لا يرجى أن يزول عنه. ويعرف ذلك بالتجربة أو بإخبار الأطباء فعليه الفدية :إطعام مسكين. وعند بعض الأئمة - كأبي حنيفة - يجوز له أن يدفع القيمة نقودًا إلى من يرى من الضعفاء والفقراء والمحتاجين

والله أعلم


* مادة الفتوى محررة من كتاب "فقه الصيام" للعلامة الدكتور يوسف القرضاوي، والصادر عن مكتبة وهبة بالقاهرة، في 28 
نوفمبر 2004م

 SOMA ZAIDI http://qaradawi.net/fatawaahkam/30/4911-2011-08-06-16-37-34.html

SABABU 25 ZINAZOMFANYA MUISLAMU ASHEREHEKEE MAZAZI YA MTUME REHMA ZA M/MUNGU ZIMSHUKIE JUU YAKE NA AMANI

Kwanini Tunasherehekea Mawlid ?

1.Mawlid ni kuonesha kumfurahikia Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam), na kufurahikia mazazi ya Mtume swalallahu aleihi wa salaam kulimnufaisha kafiri, jee sisi waislamu?! na hio ni dalili aloitumia Ibnu hajar katika fathul bary v9 p145 aliposema:
وذكر السهيلي أن العباس بن عبد المطلب رضي الله عنه قال : لما مات أبو لهب رأيته في منامي بعد حول في شر حال فقال ما لقيت بعدكم راحة الا أن العذاب يخفف عني كل يوم اثنين قال وذلك أن النبي صلى الله عليه وسلم ولد يوم الإثنين وكانت ثويبة بشرت أبا لهب بمولده فاعتقها .

Ametaja imam assuhayli kua Abbaas bin Abdilmuttwalib (r.a) amesema: "Alipokufa Abu Lahab nilimuona ndotoni baada ya mwaka yupo katika hali mbaya, akanambia sijapata baada yenu mapumziko, isipokua nakhafifishiwa adhabu kila siku ya Jumatatu, akasema na jilo ni kwasababu Mtume (swalallahu aleihi wa salaam) amezaliwa siku ya Jumatatu na Thuwayba alienda kumpa bishara Abu Lahab kwa kuzaliwa Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) akamwacha huru.
Ikiwa huyu kafiri aliefurahikia mazazi ya Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) mara moja kwa kumwacha huru kijakazi chake, anakhafifishiwa adhabu kila Jumatatu, jee waislamu wanamfurahikia mara kwa mara watapata jaza gani kwa Allaah (Subhannahu wa taala)

2: Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) alikua akiitukuza siku ya kuzaliwa kwake na akiisherehekea kwa kufunga kama ilivyothubutu katika hadithi iliopokewa na Imam Muslim kutoka kwa Abu Qatada kua Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) alipoulizwa kwanini anafunga Jumatatu akasema "Ni siku nilozaliwa na kuteremshiwa wahyi"
عَنْ أَبِى قَتَادَةَ الأَنْصَارِىِّ رضى الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ -صلى الله عليه وسلم- سُئِلَ عَنْ صَوْمِ الاِثْنَيْنِ فَقَالَ ( فِيهِ وُلِدْتُ وَفِيهِ أُنْزِلَ عَلَىَّ) .

3: Tumeambiwa na Allaah (Subhannahu wa taala) katika Qur'an tumfurahikie Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam):
. ( قُلْ بِفَضْلِ اللَّهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِمَّا يَجْمَعُونَ )) (يونس:58)
"Sema kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake, basi na wafurahi kwa hayo, haya ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya"

Katika aya hii Mwenyezi Mungu (Subhannahu wa taala) anatuamrisha kuifurahikia rahma, na Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) ndio rahma adhimu. Asema Mwenyezi Mungu (Subhannahu wa taala) katika aya nyengine: ( وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلاَّ رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ )) (الانبياء:107))
"Na hatukukutuma ispokua ni rehema kwa walimwengu"

4: Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) alikua akizingatia mafungamano kati ya zama na matokeo ya kidini yalopita, inapofika wakati ambao lilitokea ndani yake lile tokeo hua ni farsa na kulikumbuka, na kuitukuza siku hio, kwasababu ya hilo tukio. Na huu msingi ameuweka mwenyewe Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) kama ilivokuja kwa Bukhary na Muslim na Tirmidhy na wengineo kua Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) alipofika madina alikuta mayahudi wakifunga siku ya Ashuraa, akaulizia kuhusu hilo, akaambiwa kwamba wanaifunga kwasababu Mwenyezi Mungu amemuokoa Mtume wao na akamzamisha adui wao katika siku hii, kwahivo wao wanaifunga kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hio, Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) akasema: "Sisi ni bora kumkumbuka Musa kuliko nyinyi", akafunga na akaamrisha watu wafunge.

Alhafidh Ibn Hajar ndio mwanachuoni wakwanza kutolea dalili hadithi hii katika kufaa kufanya mawlid, na hakuna muislamu anaeshuku aqida ya Ibn Hajar, na maulamaa wote wamekubaliana kua yeye ndie amiri wa waumini katika hadithi.

5: Mawlid yakupelekea kumswalia Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam), na Mwenyezi Mungu (Subhannahu wa taala) ametuamrisha kumswalia aliposema:
. ( إِنَّ اللَّهَ وَمَلائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيماً )) (الأحزاب:56)
"Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu"

Na chochote kinachokupelekea kufanya yaloamrishwa na sheria basi kitu hicho pia kinakubalika kisheria, kwani kumswalia Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) kunamfaidisha mja mambo mengi:

a) Anakua amefuata amri ya Mwenyezi Mungu (Subhannahu wa taala)
b) Anaswaliwa na Mwenyezi Mungu (Subhannahu wa taala) mara kumi kwa swala moja.
c) Anapandishwa daraja kumi na kuandikiwa thawabu kumi na kufutiwa madhambi kumi.
d) Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) humrudishia salamu.
e) Huondolewa hamu zake na kusamehewa madhambi yake, Na mengine mengi.

6: Mawlid yamekusanya kutaja mazazi yake na sera yake na miujiza yake, na sisi waislamu tumeamrishwa kumjua Mtume swalallahu aleihi wa salaam na kumfuata, tunapohudhuria mawlid tunapata kuyajua yote hayo.

7: Unapomsifu Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) unapata jaza kutoka kwake, kama alivyokua akiwajazi washairi walokua wakimsifu, alimpa Ka'b bin Zuhayr (r.a) kishale na akatengezea Hassaan bin Thabit (r.a) membar. Na alikua akifurahikia kusifiwa, vipi asiurahikie kwa kukusanywa sera yake na sifa zake na miujiza yake!!!
Ametaja Alhafidh ibn Sayyidin naas katika kitabu cha منح المدح zaidi ya maswahaba mia moja na sabiini walomsifu Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) kwa mashairi mazuri mazuri.

8: Maswahaba hawakuwacha kumsifu Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) hata baada ya kufa, tena ndani ya msikiti. Ametaja Imam Shafi katika musnad yake (1706), wakati wa khilafa ya Sayyidna Omar (r.a) aliingia msikitini akampata Hassan bin Thabit akitoa mashairi ya kumsifu Mtume swalallahu aleihi wa salaam, akamwambia: "Hassan watoa mashairi katika msikiti wa Mtume?!!" (Swalallahu aeihi wa salaam) Hassaan akamjibu: "Nimeyatoa mbele ya ambae ni mbora kuliko wewe ewe Omar", akamgeukia Abu Hurayra (r.a) akamwambia: "Hukumsikia Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) akisema: "Ewe Mola mjaalie Jibril amuunge?" Abu Hurayra akasema: "Ndio nimemsikia", akasema: wakamwekea membar Hassaan msikitini ili atoe mashairi ya kumsifu Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam)

Hii ni dalili tosha kuonesha maswahaba walimsifu hata baada ya kufariki, na maneno ya Sayyidna Omar (r.a) hayakua kwa ajili ya mashairi au kumsifu Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam), bali yalikua kwa ajili ya sehemu ambayo ni msikiti, lakini alipojua kua wakati wa Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) alikua akiyatoa msikitini mbele ya Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) akajua inafaa na akamwekea na membar khaswa kwa hilo.

9: Kujua miujiza yake na sera yake na tabia zake Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) kwazidisha imani kwake na kwa aliemtuma, kwani mwanadamu ameumbwa kupenda mazuri ya umbo, tabia, ilimu, amali na mengineyo, na hakuna tabia nzuri na zilokamilka na bora kama za Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) na kuongeza mahaba inatakikana katika sheria, kwahivo na lolote lenye kupelekea hilo pia latakikana.

10: Kumtukuza Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) ni jambo liloamrishwa katika sheria,
. ( : لتؤمنوا بالله ورسوله وتعزروه وتوقروه وتسبحوه بكرة وأصيلا ) (سورة الفتح)
Na kufurahikia siku ya kuzawa kwake kwa kudhihirisha furaha na kukusanyika kuleta dhikri, na kuweka chakula, na kuwakirimu maskini ni katika alama za kumtukuza na kumfurahikia na kumshuru Mwenyezi Mungu (Subhannahu wa taala) kwa kutuongoza kwa dini ya kiislamu na kutuletea zawadi kubwa ambayo ni Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam)

11: Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) alipokua anataja ubora wa siku ya Ijumaa alitaja kua ni siku aloumbwa nabii Adam (a.s) ikiwa Ijumaa imekua bora kwa kuumbwa nabii Adam siku hiyo, je siku alozaliwa mbora wa Mitume na manabii itakosaje kua ni siku bora.

12: Qur'an imetaja mazazi ya baadhi ya mitume, na hii ni dalili tosha kuonesha siku ya mazazi ya Mtume swalallahu aleihi wa salaam ni siku tukufu na ni siku ya kukumbukwa.

13: Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) alipokua anaenda israa alipofika Bayt Lahm aliambiwa na Jibryl ashuke aswali rakaa mbili, alipomuuliza hapa ni wapi, akamwambia hapa ni sehemu alipozaliwa nabii Isa (a.s). Ikiwa sehemu alozaliwa nabii Isa (a.s) imestahiki kukumbukwa, vipi mazazi ya Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) yasikumbukwe?

14: Mwenyezi Mungu (Subhannahu wa taala) katika Qur'an anasema: 
. ( وَكُلاًّ نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنْبَاءِ الرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِ فُؤَادَكَ )) (هود: من الآية120)(
"Na yote tunayo kusimulia katika khabari za Mitume ni ya kukupa nguvu moyo wako"

Ikiwa moyo wa Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) wapewa nguvu kwa kusimuliwa khabari za Mitume, je sisi hatustahiki kuzipa nyoyo zetu nguvu na thabati kwa kusimuliana khabari za Mtume  (Swalallahu aeihi wa salaam)?

15: Kuhuisha ukumbusho wa mazazi ya Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) ni kitu kinacho takikana kisheria, kwani hatuoni amali za hajj nyingi ni kuhuisha ukumbusho ulotangulia, kama kupiga mawe jamaraat na sa3y kati ya swafa na marwa na kuchinja katika mina.

16: Amepokea Imam Bayhaqi kutoka kwa Anas (r.a) kua Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam)alijichinjia aqiqa baada ya kutumilizwa. Na imepokewa kua babu yake alimchinjia siku ya saba baada ya kuzaliwa. Imam Suyuti asema: na aqiqa hua ni mara moja tu, itakua maana ya kitendo hicho ni kua alichokifanya Mtume (Swalallahu aeihi wa salaam) ni kudhihirisha shukurani kwa kuletwa na Mwenyezi Mungu kama rahma kwa walimwengu, kwahivo inapendekezwa kudhihirisha shukurani kwa kuzawa kwake na kulisha chakula na mengineo katika sampuli za ibada na furaha.

17: Mwenyezi Mungu (Subhannahu wa taala) katika Qur'an asema:
. ( اللَّهُمَّ رَبَّنَا أَنْزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيداً لِأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً مِنْكَ وَارْزُقْنَا وَأَنْتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ) المائدة / 114 )
"Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshia chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni Ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku"

Ikiwa kuteremshwa meza ya chakula waliifanya ni sikukuu ya kuikumbuka hio neema, je siku ya kuzaliwa neema kubwa (Mtume swalallahu aleihi wa salaam) si inastahiki zaidi kukumbukwa?

18: Mwenyezi Mungu (Subhannahu wa taala) katika Qur'an anaamrisha kukubusha masiku yake yeye:
. ( وَذَكِّرْهُمْ بِأَيَّامِ اللَّهِ ...) (إبراهيم:5)
"Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu"

Je, kuzaliwa kiumbe bora na rehema ya walimwengu na Mtume wa mwisho sio siku katika masiku ya Mwenyezi Mungu? Siku ambayo imepelekea kupatikana Mtume alikuja kuziongoza nyoyo na kuwatoa watu katika kiza cha ushirikina na ukafiri.

19: Mawlid ni moja katika njia ya kufanya da'wa, na sote tunakubali kuwa mawlid imesilimisha mamilioni ya watu afrika mashariki, hii ni dalili tosha kuonesha ni jambo la kheri.

20: Amenukuu Sheikh Ibn Taymiya katika Iqtidhwaa swiratwal Mustaqim katika ukurasa wa 304 na 305 kuwa maansari (watu wa Madinah) kabla ya kuja Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) Madina walisema: Tuangalieni siku tukusanyike tukumbuke hii neema alotuneemesha Mwenyezi Mungu wakasema: "Siku ya Jumamosi", kisha wakasema: 'hatutangamani na mayahudi katika siku yao', wakasema "Jumapili", wakasema: 'hatutangamani na manaswara katika siku yao', wakasema "Ijumaa", wakajumuika katika nyumba ya Abu Umamah Saad bin Zurarah, wakachinjiwa mbuzi akawatosha wote.

21: Mawlid imefanywa kwa muda ma maqarne bila ya kupingwa na wanazuoni, na wametaja sherehe ya mawlid wana tarekhe katika vitabu vyao, kama Ibnu Kathyr na Ibnul Jawzy na Ibnu Dihya al'Andalusy, na Ibnu Hajar na Assuyutwy na wengineo na wote hao ni vigogo katika elimu za Hadith, Fiqhi, Aqidah na hawakuogopea kwa kuwatisha waisilamu na neno la Shirk au Bidaa na mengineyo tuyasikiyao zama hizi zenye kutokuwa na Maulamaa sampuli za maulamaa hao tuliowataja.
Ha hadithi ya Ibn Mas'ud yasema:
. "مَا رَآهُ المُسلِمونَ حَسَناً فَهوَ عِندَ اللهِ حسنٌ، وَمَا رَآهُ المُسلمونَ قَبيحاً فَهوَ عندَ اللهِ قَبيحٌ"
"Wanaloliona waislamu ni jema basi na mwa Mwenyezi Mungu pia ni jema, na wanachokiona waislamu ni kiovu basi na kwa mwenyezi Mungu pia ni kiovu"

22: Mwenyezi Mungu (Subhannahu wa taala) asema:
{وَمَنْ يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِنْ تَقْوَى الْقُلُوبِ} [الحج:32]
"Na mwenye kutukuza sha'air za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo"

Ikiwa kuadhimisha na kutukuza tambiko la Mwenyezi Mungu (Subhannahu wa taala) ni katika unyenyekevu wa nyoyo, basi na Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) ni tambiko la Mwenyezi Mungu (Subhannahu wa taala), na kutukuza mazazi yake ni kumtukuza yeye.

23: Kuhudhuria mawlid kunakuza mahaba ya mu'min kwa Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam), na Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) anasema katika hadithi iliopokewa na Imam Bukhary:
. "لاَ يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكونَ أحبَّ إليه مِن والده وَوَلدِه وَالنَّاسِ أَجمعين"
"Haikamiliki imani ya mmoja wenu mpaka anipende mimi zaidi ya mzazi wake na watoto wake na watu wote"

24: Maulamaa wakubwa walofika daraja ya kua mahuffaadh wametunga vitabu kuhusu mawlid:

A: Alhaafidh Ibnu Kathyr anayetegemewa na wenye kujiita Salafiyah. Ametaja hilo Ibn Hajar katika Addurarul Kaaminah.

B: Alhafidh al'Iraqy, ametunga : المورد الهني في المولد السني .

C: Alhaafidh Ibn Naaswiruddyn Addimashqy, huyu ana vitabu vitatu:
i) جامع الآثار في مولد النبي المختار
ii) اللفظ الرائق في مولد خير الخلائق
iii) مورد الصادي في مولد الهادي .

D: Alhaafidh Assakhaawy, ametunga: الفخر العلوي في المولد النبوي .

E: Alhaafidh Mullaa Ali Alqaary, ametunga: المورد الروي في المولد النبوي .

F: Alhaafidh Ash'shaybany Azzabidy, anaejulikana kwa Ibnud dayba’a, ametunga maulidi yake mashuhuri mawlid addayba’a.

G: Alhaafidh Assuyutwi, ametunga حسن المقصد في عمل المولد .

H: Alhaafidh ibnu Dihya, ametunga: التنوير في مولد البشير النذير .

J: Alhaafidh Ibnul jazary, ametunga: عرف التعريف بالمولد الشريف .
Mbali na hufaadh kuna muhadditheen walotunga mawlid na fuqahaa na mufassireen na wengineo wengi, hatutowataja wote kwa kutorefusha nukta hii.

25: Sababu wanazotoa wanaokataza kusherehekea mawlid:

Sababu ya 1: Wanasema lingekua ni kheri basi Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) angelifanya.

Tunawauliza; je, kutia nukta na shakli katika msahafu ni kheri ama si kheri? na Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) hakulifanya, je, tuzitoe kwa kuwa (Swalallahu aleihi wa salaam) hakulifanya?

Sababu ya 2: Wanasema Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) hakufanya mawlid.

Tunasema; Sio kila ambalo hakuliamrisha Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) wala hakulikataza halifai, mashindano ya Qur'an Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) hakufanya, tahajjud kwa jamaa msikitini Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) hakuifanya, kukhitimisha msahafu katika tarawehe Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) hakulifanya hilo, na wengi wanaopinga mawlid wanayafanya yote hayo na hayakufanywa na Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) Nani kawapa rukhsa ya kuyafanya hayo na kutukataza sisi tusifanye kwa kuwa tu wao hawafanyi na hawapendi?

Sababu ya 3: Wanasema Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) amesema mwenye kuzusha katika dini kisokua katika dini basi haikubaliwi!

Tunawaambia; hamkuifahamu hadithi kama walovyoifahamu maulamaa wakubwa wa karne na karne tena Mahufaadh. Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) amesema kisochokua katika dini, ama kilichoko katika dini basi kinakubaliwa, na yote yanayopatikana katika mawlid kama kusoma Qur'an na kumswalia Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) na kulisha chakula yote yapo katika dini.

Sababu ya 4: Wanatumia lugha ya kutisha na wanasema kufanya mawlid ni kumtuhumu Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) kuwa amefanya khiyana na haitufikishia kila jambo katika dini!

Tunawaambia; Na hayo mambo tulowatajia hapo juu ambayo hata wao wanayafanya na hayakutajwa na Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) sio kumtuhumu kwa khiyana? Kisha maulamaa waloweka mambo haya tayari mushawatuhumu.

Sababu ya 5: Wanasema katika baadhi ya mawlidi kunapatikana munkarati, kwahivo ni haramu.

Kwanza twawauliza; Je, Mawlid isiyokua na munkaraati mwaikubali? pili kama kuweko munkaraati kwa baadhi ya mambo itapelekea kuharamisha yote basi itabidi tuharamishe harusi pia, maana kuna zengine hujaa munkarati.

Sababu ya 6: Wanasema mawlidi haifai kwasababu kwasifiwa Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam), na Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) amekataza aliposema:
. "لا تُطْروني كما أطْرَتِ النَّصارى الْمَسيحَ ابنَ مَرْيَمَ"

Tunawaambia; Neno ‘’itraa’’ katika lugha maana yake ni kuvuka mpaka katika kusifu, na kuvuka mpaka kwenyewe tayari Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) amekupigia mfano katika hadithi hiyohiyo aliposema kama walivyo vuka mpaka manaswara kwa Isa. Ni mpaka upi huo waliovuka manaswara? Walifika kumuita Mungu na Mtoto wa Mungu. Je, kuna muislamu ambae anaitakidi Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) ni Mungu ama ni mtoto wa Mungu? Kwahivo namna tutakavyo msifu madamu hatujafika katika huo mpaka basi hakuna uharamu wala makosa. Na qaaida ya ki-usuli yasema, linapokatazwa jambo maana yake ni kulifanya jambo hilo kinyume cha makatazo yake, kwahivyo Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) katika hadithi hii hajatukataza kumsifu sana, bali ametuamrisha kumsifu sana, madamu hatutavuka mipaka.

Sababu ya 7: Wanasema kufanya mawlid ni kuyafunga mahaba ya Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) katika siku moja tu!

Tunawauliza; Pale Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) aliposema sisi ni awla kumsherehekea Musa kuliko wao, kisha akafunga na akaamrisha watu wafunge je, aliyafunga mahaba ya nabii Musa katika siku moja?

Sababu ya 8: Wanasema maswahaba walikua ni wabora na wanampenda Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) kuliko sisi na hawakunya mawlid

Tunawaambia; je, alotia nukta katika msahafu wakati wa Hajjaaj bin Yusuf alikua aipenda Qur'an kuliko maswahaba? je, Sayyidna Omar (r.a) alipowakusanya watu msikitini kuswali tarawehe alikua ni mbora kuliko Sayyiduna Abu Bakr ambae hakulifanya hilo? je, Sayyiduna Uthmaan (r.a)alipoweka adhana yapili alikua ni mbora kuliko sayyidna Abu Bakr na Sayyidna Omar? wanazuoni wamesema: الْمَزِيَّةُ لا تَقْتَضي التَّفْضيلَ .

Sababu ya 9: Wanasema mawlid imekua ni hoja ya wanaoenda kufanya uchafu wao!

Tunawaambia; Tatizo lipo katika niya ya huyo mtu, wala sio kwa mawlid, na kama anavotumia mawlid kama hoja na pia atatumia mengine pia kama kuenda tarawehe. Kuna watu wanaenda hajj kwa ajili ya kuiba, na wengine huenda kutongoza na wengine huenda kufanya makubwa kushinda hayo, jee tuondoe ibada ya hajj? Usiseme huswali kwa kua nguo ina najasa, safisha najasa uswali.

Sababu ya 10: Wanasema mawlid ni katika mambo yenye shaka, na Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam) ametuambia tuwache yenye shaka.

Tunawaambia; Shaka ipo katika wahm zao, ama kwetu hamna shaka hata kidogo kuwa mawlid yafaa na hayapingani na mafundisho ya dini tukufu ya Kiisilamu wala Mafundisho ya Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam)

Mwisho tunatoa nasiha kwa wanaotumia juhudi kubwa kupinga mawlid:

Lau mngelitumia juhudi hizo katika kukataza mambo ya haramu ambayo hayana shaka tungekua hatuna uchafu tunaouona katika jamii, kuenea madawa ya kulevya na zinaa na vijana kupuuza swala na mengineo.

Wabillahi Tawfiq.

Imetayarishwa na Vijana wa Kitwariqa Afrika Mashariki  , Followers of Tariqah Alawiyah East Africa.

kwa makala zaidi tembeea : www.twariqah.blogspot.co.uk

♥ I Need Allah In My Life ♥

A person may be healthy but not free due to being busy with earning a living, or he could be without need [for earning a living] and not be healthy. If the two factors come together and laziness from acts of obedience overcomes him, he is deceived. The full [picture] is that this world is a farm of the next world. In it is business whose profits will appear in the next life. So whoever uses his free time and health in doing acts of obedience is in an enviable position, fortunate, and blessed, and whoever uses them in acts of disobedience is deceived. Because free time is followed by business, and health by sickness, even if it is only old age - Ibn al-Jawzi [not a hadith]

Allahu Akbar!

BADO NATAFARI KAULI HII NITAKUJA NA FIKRA " Onyo la Mufti Simba".

Mufti Simba amesema viongozi wa dini wanaotumiwa na viongozi wa siasa kuzitumia nyumba za ibada kufanya siasa wamefilisika kiimani na wanaendekeza njaa.

Kiongozi huyo alitoa kauli hiyo juzi jijini Dar es Salaam katika hafla ya kufuturisha, iliyoandaliwa na familia ya Mwenyekiti wa Taasisi ya Kiislamu ya Imamu Bukhary, Sheikh Khalifa Khamis, ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

Mufti Simba alisema maimamu wanatakiwa kutambua kuwa misikiti ni tiba ya kiroho, hivyo si vema kuwaruhusu wanasiasa kujitakasa na kujenga makundi kwa waumini wenyewe kwa wenyewe.

Alisema kunahitajika kuwa na amani katika nyumba za ibada hivyo Waislamu wana wajibu wa kulinda dini yao, si kuingia misikitini na kutoa mada zinaloleta shida na migawanyiko kwenye jamii.

“Kama wewe ni mwanasiasa nenda huko bungeni ndiko eneo lako, misikitini si eneo la siasa, msiingie na kuanza kutoa maneno ya kujitakasa. Unaizungumza Bakwata vibaya kwakuwa unataka uiteke, wewe nani? Nenda zako bungeni kafanye hiyo siasa yako,” alisema Mufti Simba.

Mufti alisema kutokana na fujo za mara kwa mara na kuvunjika kwa amani misikitini kutasambazwa waraka maalumu kwa ajili ya kuanzisha kamati za ulinzi misikitini ili kudhibiti fujo hizo zinazotokea kwa mgongo wa dini.

Alisema waraka huo unatokana na kongamano la amani lililofanyika kati ya viongozi wa dini na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, kwa ajili ya kudhibiti matukio mabaya misikitini yanayoashiria uvunjifu wa amani.

Alisema kwa sasa kila msikiti utakuwa na kamati ya ulinzi na kama kutakuwa na yeyote anayefikiria ama kufanya vurugu atadhibitiwa na kukamatwa kama mhalifu wa makosa ya jinai na atashitakiwa kama watuhumiwa wengine.

Naye Sheikh Khalifa aliwashukuru wananchi mbalimbali na masheikh kwa kujumuika nao lakini alisisitiza kuwa katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu ujao maimamu wanatakiwa kujitambua na kuacha kutumika kwa wanasiasa waliofilisika.

Alisema ni aibu kwa kiongozi wa dini kufikia hatua ya kuwa na mgombea wake msikitini, hivyo kuwagawa waumini wake wasiomtaka mgombea husika.

“Katika chaguzi mbalimbali hali imekuwa mbaya, kwa kuwa chaguzi sasa zimegeuka pesa, mtu anatoa pesa zake na kuwatumia viongozi wa dini, hali hii haitavumiliwa kabisa, utakuta wanasiasa mufilisi wanatoa fedha na viwanja kwa ajili ya kujineemesha wao wenyewe,” alisema Sheikh Khalifa.

Naye Rais mstaafu Mwinyi, aliwashukuru watu wote waliohudhuria futari hiyo huku akisisitiza umoja, amani na utuvuli ambavyo vinawafanya watu waishi na kufanya shughuli zao bila hofu yoyote.

BADO NATAFARI KAULI HII NA NITAKUJA NA FIKRA ...

WAISLAMU WENYEWE KWA WENYEWE TUNAMALIZANA KAULI YAKE NZURI LAKINI PAANGALIWE UPANDE WA PILI JEE WAKITUMIA NYUMBA ZAO SISI TUFANYEJE ?

NASAHA ZA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Ndugu zangu Waislam
Tukiwa tupo tunaendelea na Ibada hii ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani tukumbuke kuwa kuna Mambo ambayo tunatakiwa tuyafanye kwa wingi na vile

vile kuna Mambo tunatakiwa tujiepushe Nayo.

AMBAYO TUNATAKIWA KUJIEPUSHA NAYO KATIKA MWEZI HUU NA BAKI YA MIEZI MINGINE.

1.Tabia Mbaya na maneno maovu Mfano wa kusengenya, kusema uongo n.k (Mwezi huu sana na baki ya miezi ).

2.Kulala sana kwani kulala huko kunatupotezea Fursa za kufanya Ibada ya Kusoma Qur an na Ibada Nyenginezo (Mwezi huu sana na baki ya miezi ).

3.Kupoteza wakati mwingi katika michezo na maongezi yasiyo na faida Vijiweni kwa

Kucheza Bao,

Karata na kuacha kuutumia wakati huo katika kazi na ibada mbali mbali Mfano kuhudhuria Darsa Misikiti kipindi cha Swala ya Alasiri au kwa Mujibu wa Ratiba za Masheikh wasimamizi wa Darsa hizo (Mwezi huu sana na baki ya miezi ).

4.Kuacha kula daku au kuchelewa kufuturu (Mwezi huu ).

5.Kufanya israfu katika vyakula na vinywaji wakati wa kufutari tukumbuke kwamba kuna wenzetu wengi nao wanahitajia Vyakula hivyo na Viywaji hivyo hakuna haja ya Israfu na kufanya Fujo katika Chakula (Mwezi huu ).

6.Kuacha kuswali Swala ya Tarawekhe ambayo ni Sunna inayopatikana Mwezi wa Ramadhani tu (Mwezi huu ).

Ndugu zangu wapendwa haya ni katika Mambo ambayo Mfungaji anatakiwa ajiepushe nayo zaidi katika Kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhani na Muda wake wote wa Maisha yetu .

Tumuombe M/Mungu kwa Ujumla azipokee Ibada zetu na azikubali Funga zetu Amiin ...

اللهم إنك عفواً كريم تحب العفو فاعف عنا

اللهم إنك عفواً كريم تحب العفو فاعف عنا
 
M/MUNGU AKIKUBARIKI KUUDIRIKI USIKU  WA CHEO SOMA DUA HII KWA MAELEKEZO YA MAMA AISHA
alimuliza Mtume Jee? tukiidiriki LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO) tufanye nini ? Mtume akajibu kithirisha kusema ALLAHUMA INNAKA AFUWUN TUHIBUL AFWAA FA'AFUANNAA ". Kama alivyosema Mtume
 

INTERNATIONAL HOLY QUR AN MEMORIZATION COMPETITION 2013 .

 CONTRIBUTE TO DEVELOP HOLY QUR AN MEMORIZATION IN TANZANIA ..

MAANA YA FUNGA

Neno Swaumu ambalo ni funga kilugha (Maana yake katika Lugha) ni Kujizuia

Ukijizuia na kula wewe unakuwa Umefunga.
Ukijizuia na Kuzungumza wewe unakuwa umefunga katika Maana ya Kilugha.

Dalili : Qur an

M/Mungu anasema katika kusimulia Kisa cha Bi Maryam "...Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu."Qur an Surat Maryam aya ya 26.

MAANA YA FUNGA KISHARIA .

Kujizuia/kujizuilia na vyenye kufuturisha [kufunguza] kuanzia kudhihiri alfajiri [ya pili] mpaka kuchwa [kuzama] kwa Jua pamoja na Nia.

Hii ndio Maana ya Funga.


Baadhi ya Wanawazuoni wameigawa Swaumu katika Vigawanyo Vikuu Viwili.

1.WAAJIB
2.SUNNA

Funga za Wajib ni kama Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambayo ni Nguzo katika Nguzo za Uislam.

Funga ya Kaffara na Nadhiri .

Funga za Sunna Mfano wa Funga za Jumatatu , Alhamis na Nyingi nyenginezo.

Angalizo :

Wapo wanachuoni wengine wamezigawa/wamezifanya Aina za Funga zaidi ya hizo Mbili kwa kuongeza Funga za Karaha , na Funga za Haraam .
  

HISTORIA YA FUNGA

Ndugu zangu wapendwa Tukumbuke kuwa Funga si ibada Ngeni, bali ni Ibada iliyofaradhishwa/Wajibishwa kwa WATU waliotangulia kabla yetu na pia kufaradhishwa katika umati huu wetu wa Mtume Muhammad Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani (S.AW).

Dalili

M/Mungu Subhanahu Wataallah anasema katika Qur an " Enyi mlioamini! mmelazimishwa kufunga [Swaumu] kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu". Qur an Suratul Baqarah aya ya 183.

Ama katika umati huu wa Mtume Muhammad Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani (S.AW) Funga ilifaradhishwa katika Mwezi wa Shaabani mwaka wa pili baada ya hijrah Mtume Muhammad (S.A.W).

Mtume (S.A.W) amefunga Miaka 9 na Baada ya hapo akafariki Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani.

Tumesema kuwa Funga ya Mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani ni Wajib na Ni Nguzo katika Nguzo za Uislam kwa Dalili zipi tunatolea Dalili kwa haya tunayo yasema InshaAllah Ukumbusho Ujao tutazieleza Dalili ambazo zimeifanya Funga ya Mwezi wa Ramadhani kuwa ni wa Wajib kutoka Qur an , Sunna na Ijmai za Wanawachuoni.
 


M/Mungu Subhanahu WataAla anasema katika Qur an

“ Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga (Saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu. Qur an Suratul Baqarah aya ya 183.
Siku chache tu ( kufunga huko)...(Mwezi huo mlioambiwa mfunge) ….. “. Qur an Suratul Baqarah aya ya 184.

Ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika mwezi huo hii Qur-aani ili iwe uwongozi kwa watu, na hoja zilizo wazi wa uongozi na upambanuzi (wa baina ya haki na batili) Atakae Uona ( kuwa katika mji katika huu mwezi) (wa Ramadhani) afunge .…” Qur an Suratul Baqarah aya ya 185.

Dalili ya Hdithi

Imepokelewa hadithi kutoka kwa Abdullah ibn Umar M/Mungu amuwie Radhi amesema : Nimemsikia Mtume Muhammad (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani akisema: “ Umejengwa Uislam juu ya nguzo tano;

1.kushuhudia ya kwamba hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah Subhaanahu wa Ta3ala na hakika ya Mtume Muhammad (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie juu yake na Amani ni mtume wa M/Mungu.

2.Kudumisha Swala.

3.Kutoa Zakkah.

4.Kuhiji Katika Nyumba Tukufu Alkaaba Makkah (kwa Mwenye uwezo).

5.Kufunga Ramadhani ( Ushahidi wetu ) Kama alivyosema Mtume hadithi imepokewa na Imamu Bukhari na Muslim.

Na kuna hadithi nyingine nyingi zinazojulisha Uwajibu wa Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Dalili katika Ijmai (Makubalino ya Wanawazuoni) kwa Mujibu wa Wanawazuoni wote wamekubaliana na kuwafikiana kwamba Funga ya Mwezi wa Ramadhani ni Wajib kwa Maana ni lazima kwa kila Muislam.

Ndugu yangu Muislamu

Hizi ndio Dalili ambazo zimeifanya Ibada ya Funga ya Mwezi wa Ramadhani kuwa Ni wajibu kwetu.


InshaAllah tuta endelea kuelezea  hukmu ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 

Wabillahi - Taufiqh 

By :- Ghalib Nassor Monero l Azhary