Monday, July 29, 2013

MAMBO YENYE KUHARIBU FUNGA

 1.Kula au kunywa kwa kukusudia.

2.Kila kinachoingia tumboni au kooni kwa kukusudia.

3.Kukutana kimwili (kuingiliana) kati ya mume na mke. 

4.Kujitoa Manii au kusababisha kutokwa na Manii (kwa kujichezea sehemu za siri, kukumbatiana au kupigana mabusu n.k

5. Kujitapisha kwa makusudi.
Imepokelewa hadith kutoka kwa Abu Hurayrah Radhi za M/Mungu zimshukie juu yake na Amani Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie juu yake na amani amesema " ...na mwenye kujitapisha basi inamuwajibikia kulipa". kama alivyosema Mtume (Wameipokea Maimamu watano).

6.Kutokwa na Damu ya Mwezi (Hedhi) au Damu ya Uzazi ( nifasi ).

Na tukasema kwamba hukmu za Mambo haya zimegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo tuliahidi kwa uwezo wa M/Mungu katika Post hii tutayaeleza hukmu hizo.

Ndugu yangu Mpendwa katika Imani Fahamu kwamba Mambo haya tuliyo yaeleza yenye kuharibu funga kwa upande wa HUKMU ZAKE pale yanapo mtokea Mtu yapo ambayo yanampasa Mtu

1.KULIPA.

2.KULIPA NA KAFARA .

Mambo yote tuliyoyataja ukitoa namba tatu (3) yanabeba/yanachukua Hukmu ya Namba Moja Namba Tatu lina Chukua Hukmu ya Namba 2.

KAFARA

tuliposema katika hukmu ya Mtu mwenye kumuingilia Mke wake Mchana wa wa Mwezi wa Ramadhani alipe na kafara tunamanisha kulipa hapo ni kulipa ile siku ambayo ameiharibu funga yake kwa kumuingilia Mke wake baada ya Ramadhani.
Ama kafara iko katika Mpangilio kama ufuuatao :-

1.Kumuachia Huru Mtumwa - Alhamdullilah utumwa hakuna siku hizi.
2.Kufunga Miezi Miwili mfululizo ikiwa hawezi
3.Kulishiza/lisha Maskini 60

na vile vile inampasa kuleta Istighfaari kwa Mola wale kwa kosa alilo litenda kwa kuingilia Mchana wa Mwezi Ramadhani M/Mungu ndiye Mjuzi zaidi

BY : GHALIB NASSOR MONERO L AZHARIY

FADHILA ZA FUNGA


Ndugu zangu wapendwa tukumbuke kwamba Funga iko na Fadhila Nyingi sana Soma Hadithi zifuatazo ili tupate kujikumbusha Miongoni mwa Fadhila za Funga.

Zimepokewa Hadithi nyingi sana zinazoelezea fadhila za funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, miongoni mwa hadithi hizo ni hadithi zifuatazo:

1- Amesema Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani " Mwenye kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa imani na kutarajia malipo (toka kwa M/Mungu Mtukufu (aliyetakasika na kutukuka ) husamehewa madhambi aliyoyatanguliza". kama alivyosema Mtume Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani hadithi imepokewa na Maimamu wawili Bukhari na Muslim.

2- Amesema Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani " Kila amali (Matendo) ya mwanaadamu (aifanyayo) ni yake, wema (mmoja) hulipwa kwa mfano wake mara kumi mpaka mara mia saba, isipokuwa funga, hakika ya funga ni Yangu mimi, na Mimi najua namna gani Nimlipe kwa funga hiyo, ameacha matamanio yake na chakula chake na kinywaji chake kwa ajili Yangu, mfungaji ana furaha mbili, furaha wakati wa kufutari kwake na furaha nyengine pale atapokukutana na Mola wake. Harufu yakinywa cha mfungaji inapendeza zaidi kwa M/M ungu kuliko harufu ya miski ". Imepokelewa hadithi na Imamu Bukhari na Muslim.

3- Hufungiwa ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Mashetani kama alivyosema Mtume katika Hadithi ambazo tumeshazitaja katika Darsa zetu zilizopita.

4-Ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hufunguliwa Milango ya Peponi na hufungwa Milango ya Motoni.
Amesema Mtume (S.A.W) " Unapoingia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hufunguliwa Milango ya Peponi na hufungwa Milango ya Motoni hutiwa Macheni/Minyororo Mashetani " kama alivyosema Mtume Hadithi Imepokelewa na Imamu Bukhari.

5-Ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kunapatikana Usiku wa Cheo Usiku wa LAYLATUL QADIR Ubora wake ni zaidi ya Miezi 1000.

6- Ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuna Saa ambayo Mja akiomba kwa Mola wake Dua zake hazirudi patupu na tumeusiwa sana kuomba Dua wakati pale tunapo futuru .

Ndugu zangu wapendwa hizi ni katika chache ya Fadhila za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni hasara kwetu kama tutaudiriki Mwezi huu na ukaisha bila ya kupata nao faida.

من لم يربح في هذا الشهر، ففي أي وقت يربح

Mtu ambaye hatopata faida katika Mwezi huu wenye Nyingi Fadhila Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Wakati gani Mwengine atapata faida.
JE YAJUZU(INAFAA) KWA MWANAMKE KUKAA ITKAFU NYUMBANI KWAKE?

Moja katika Nguzo za itkafu ni Kukaa itkafu msikitini.
Hivyo iwapo kama Mwanamke atakaa itkafu Nyumbani kwake haito swihi kutokana na kukosekana Nguzo hiyo isipokuwa iwapo kama mwanamke atajetenga Nyumbani kwake na kujitahidi katika ibada Twatarajia atapata malipo makubwa insha Allah.

Iwapo mwanamke atahitaji kwenda kukaa itkafu msikitini yanahitajika mambo yafuatayo:

1.Kuwe msikitini kuna sehemu Maalum kwa wanawake.

2.Iwe ni sehemu yenye amani dhidi ya fitina kwa mwanamke huyu.

3.Ikiwa mwanamke kaolewa basi yatakiwa apate idhini kutoka kwa mumewe.

4.Isiwe katika kukaa kwake itikafu atapoteza haki za mumewe
wazazi wake au kulea watoto wake.

Tunamuomba M/Mungu azikubali Funga zetu na Maombi yetu yote kwa Ujumla ...

MAMBO YANAYO PENDEZA KUFANYWA NA MKAAJI WA ITKAFU

MAMBO YANAYO PENDEZA KUFANYWA NA MKAAJI WA ITKAFU

yafuatayo ni Baadhi ya Mambo yanayopendeza kwa Mwenye kukaa Itkafu kuyafanya .

1.Ibada za Sunna kama Vile Swala n.k
2.Kusoma Qur an
3.Kufanya Dhikri tofauti Mf, Tasbihi , Tahmid , Kuleta Takbir ,Istighfaar N.k
4.Kumswalia Mtume Muhammad (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani.
5.Kukithirisha Kuomba Dua na Nyingi katika Ibada Ambazo hatuzazitaja hapa unazozifahamu.

Ni Jambo Jema Masheikh/Maustaadh katika Kipindi kama hiki cha Itkafu kukawa na Darsa katika Msikiti husika ili kupata Waumini kungeza Maarifa kwa kipindi kila ambacho wapo katika Ibada hiyo ya Itkafu.

Inapendeza kwa Mkaaji wa Itkafu achukue Vitu Muhimu atakavyo hitajia katika kipindi atakacho kuwa amejitenga / amekaa itkafu Msikitini ili asilazimike au aepuke kutoka toka Msikitini.

MAMBO YASIYO PENDEZA KUFANYWA NA MKAAJI WA ITKAFU
Haipendezi kwa mkaaji wa itkafu kujishughulisha na mambo yaliyo nje ya ibada na utiifu.Mfano mazungumzo yasiyo kuwa na faida na shughuli zisizokuwa na faida kwa mkaaji itkafu.Vile vile yachukiwa kwa mkaaji itkafu kukaa kimya na kuto zungumza akidhani ya kwamba hiyo ni katika ibada.

MAS A LLAH

JE YAJUZU(INAFAA) KWA MWANAMKE KUKAA ITKAFU NYUMBANI KWAKE AU MSIKITINI ?
InshaAllah endelea kufuatilia na tunakutakia Funga Njema ...

MUDA WA ITKAFU

MUDA WA ITKAFU

Muda wa itkafu ikiwa ni itkafu ya Wajib basi utatakiwa kukaa itkafu mpaka uishe ule muda Ulio Nadhiria kukaa itkafu.

Ama ikiwa ni itkafu ya sunna basi itkafu hii haina muda maalumu, bali Mja anapata Thawabu kulingana na muda atakao kaa msikitini.

MASHARTI YA ITKAFU

1.Uislam
2.Utambuzi
3.Twahara ya Janaba Hedhi na Nifasi.

Itkafu haiswihi kwa ASIYE kuwa Muislam wala mtoto asiyekuwa Mtambuzi Vile vile haiswihi kwa mwenye Janaba Hedhi na Nifasi.

NGUZO ZA ITKAFU

Kama tulivyo ieleza Maana ya Itkafu Kishaaria kuwa ni kukaa msikitini kwa nia ya kujikurubisha kwa M/Mungu Subhanahu Wataallah.

Kupitia Maana hiyo tunapata tambua kuwa Nguzo za Itkafu Ni

1.Nia ya kujikurubisha/Kumtii M/Mungu.

2.Kukaa msikitini.

Kwa Mujibu wa Nguzo hizo tulizo zitaja ikiwa Mtu atakaa Msikitini bila ya Nia ya Itkafu ya Kujikurubisha/Kumtii M/Mungu basi atakuwa hana Itkafu NDUGU KIJANA WA KIISLAM KUMBUKA KUWA NIA NDIO MPANGO MZIMA KATIKA IBADA ZETU ZETU ILI KUTOFAUTISHA KATI YA ADA NA IBADA NA HILI NDIO LENGO KUU LA NIA .

NAKUOMBA USINICHOKE TUENDELEE KUWA PAMOJA KATIKA MFULULIZO WETU HUU WA DARSA ZETU KUPITIA FACEBOOK ID :KIJANA WA KIISLAM DSM

UKURASA WA TUNAKUOMBA U - LIKE :Kijana wa Kiislam Tanzania
UKURASA WA TUNAKUOMBA U - LIKE :NAJIVUNIA KUWA BINT WA KIISLAM
WHATSAPP :+201110189580
SKYPE : al.amin_2010

Na : Ghalib N Monero L Azhary

ITIKAFU NA MAANA YAKE NA DALILI ZAKE .

ITIKAFU NA MAANA YAKE NA DALILI ZAKE .

Maana ya Itikafu Ki - Lugha ni Kushikamana na kitu na kuizuia nafsi kwa ajili ya kitu hicho sawa kitu hicho kiwe ni kizuri au kibaya.
Dalili
M/Mungu Anasema katika kumuelezea Nabii Ibrahimu pindi alipo kuwa akimsimamishia hoja baba yake na watu wake dhidi ya kuabudia masanamu "Alipo mwambia baba yake na watu wake: Ni nini haya masanamu mnayo yashughulikia kuyaabudu? ".
Qur an Suratil Anbya Aya 52.

Ama Maana ya Itkafu Upande wa Ki - Sharia na Ndio Kusudio letu

Kushikamana na Msikiti na kukaa ndani yake pasina ya kutoka kwa ajili ya kujikurubisha(kuwa karibu) kwa M/Mungu Mtukufu .

Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu katika kila Mwaka ndani ya kumi la mwisho la Ramadhani na Mwaka alio fariki alikaa itikafu muda wa siku ishirini Kama ilivyo pokelewa na Bukhari.

Vile vile Maswahaba wa Mtume na Wake zake walikaa nae itikafu na walikaa Itikafu baada ya mtume kufariki.

Ibada hii ya Itkafu imekokotezwa sana katika kumi la Mwisho la Ramadhani kwa Ajili ya Ku utafuta Usiku wa Cheo (LAYLATUL - QADIR) ambao unapatikana katika Mwezi 21,23,25,27,29.

Wanawazuoni wengi wameichagua na kumili katika siku hii ya Mwezi 27 na M/Mungu Ndiye Mjuzi zaidi wa Siku hiyo.

VIGAWANYO VYA ITIKAFU

Itikafu imegawanyika Sehemu mbili
1.Itikafu ya Sunna
2.Itikafu ya wajibu.

Itikafu ya Sunna ni itikafu ambayo Mja anajitole kwa huko kukaa kwake itikafu, kwa ajili ya kujikurubisha kwa M/Mungu na kujipatia thawabu.

Vile vile kwa ajili ya kumuiga Menendo wa Mtume Muhammad (S.A.W) Rehma za na Amani zimshukie Juu yake.

Muda wa Ibada wa Sunna hii imetiliwa Mkazo sana katika Kipindi hiki cha Ramadhani.

ITKAFU YA WAJIB
Ni itikafu ambayo Mja kaji wajibisha yeye mwenyewe.

Nayo inakuwa ima kwa Nadhiri ambayo haijaegemeshwa juu ya jambo lolote, Mfano: Nimetia nadhiri kwa ajili ya Allah kwa kukaa itikafu siku tatu.
Au inakuwa kwa nadhiri inayokuwa imeegemeshwa juu ya jambo fulani, Mfano:Iwapo Allah atamponya Mgonjwa wangu nitakaa itikafu kwa ajili ya Allah Muda wa siku moja.

Dalili
Mtume (S.A.W) Rehma za M/mungu zimshukie juu yake na Amani anasema "Yule atakaye tia Nadhiri ya kumtii Allah basi na amtii) Kama alivyosema Mtume hadithi imepokelewa na Bukhari.

Ndugu yangu katika Uislam huu Ni Mwanzo na IshaAllah kwa uwezo wake Allah tutakuwa ni Mwenye kuendelea na Maelezo ya Ibada hii ya Itkafu kwa uwezo wake Muumba.

Dua zenu za kheri msitusahau M/MUNGU azipokee funga zetu na Ibada zetu kwa Ujumla.Amiin ...

Na : Ghalib N Monero l Azhariy .

Vijana wa Qur an kutoka Nairobi , Kenya na Dar es salaam Tanzania .

Mshindi wa mashindano ya Quran Juzuu 30 , 
Umri wa miaka 15 
Jina  Abdulhalim  wa Madrasatul Bushra NAIROBI.

Mashindano hayo hufanyika kila Ramadhani Uwanja wa Makadara Mombasa Amepata zawadi ya Hajj yake na Mzazi wake na Dollar 350 za Marekani na Shillingi elfu 30 pesa Taslimu za KENYA.
Mshindi wa kwanza  Juzuu 30 wa Mashindano ya Qur-an ya 14 yanayoandaliwa na Taasisi ya Al-hikma education centre chini ya usimamizi wa Sh. Nurdin Kishki.

Jina: Suleyman Omary  Umri 13
Madrasa : Al-hikma primary english medium (Markaz Al-hikma) darasa la 6.

Mashaa Allaah!


Allah ajaalie Quran kuwa hoja kwetu na wala sio juu yetu.

Zakkatul Fitri


SOMA UJUMBE HUU MPAKA MWISHO MUHIMU .


Zakkatul Fitri

Ndugu yangu kumbuka kwamba kutoa Zakatul Fitri ni Wajibu kwa kila Muislam,Mwanamume, Mwanamke,Mkubwa, Mdogo, Muungwana (huru) au Mtumwa).

Inapasa kwa Muislam ikiwa atakuwa na uwezo wa kumiliki chakula na ziada siku ya Iddi na Usiku wake Itampasa atoe yeye na wale ambao wako Chini yake Kimalezi na Ungalizi.

Ikiwa Mtu anajitegemea Mwanamke / Mwanaume italazimika wao wenyewe kujitegemea katika kutoa Zakkah hizo.

Wakati wa kutolewa Zakkah hiyo Inatakikana itolewe Zakkatul Fitri kabla ya Swala ama itakayo tolewa baada ya swala haiesabiki kuwa ni Zakkatul Fitri bali Ni Sadaka kama Sadaka Nyengine.

Lengo la kutolewa Zakkatul Fitri

1.Kuwawezesha Waislam wasio kuwa na uwezo katika Siku hii kufurahi kama unavyofurahi wewe na Watu wako (Ahlubait)

2.Ibada

3.Zakaatul fitri hutolewa kwa ajili ya kusahihisha saum na hufidia ktk makosa madogo madogo

Zimepokewa hadithi tofauti katika Suala hili tuisome hadithi hii ya Ibn Umar Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani Amesema " Amefaradhisha Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani Zakkah ya fitri (Ya kumalizika Ramadhani) Pishi ya Tende au Pishi ya Shairi kwa Mtumwa na Huru (Muungwana), Mume na Mke, Mdogo na Mkubwa katika Waislam, na akaamrisha (hiyo zakkah ya fitri) itolewe kabla ya kutoka watu kuelekea katika Swalah (ya iddi).Kama alivyosema Mtume hadithi hii imepokewa na Maimamu wawili Bukhari na Muslim.

KIASI KINA CHOTOLEWA CHA ZAKKATUL FITRI
Kwa Mujibu wa Hadithi tuliyo itanguliza ikiwa ni Pishi ya Chakula Maarufu katika Mji uliopo inakuwa ni sawa na Kilo mbili na Gramu mia nne (2.4 kg) takribani kwa nafaka kama mchele na mfano wake) ( au thamani yake kwa baadhi ya wanachuoni )

Wenye kustahiki Zakkah hizi ni watu Maskini wasio na uwezo katika Waislam katika Sehemu Unayoishi.

KIFO NA UHAI NINI KIMETANGULIA KUUMBWA



M/Mungu Subhanahu Wataa3la anasema "Vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu na hali mlikuwa wafu akakufufueni! Kisha atakufisheni, tena atakufufueni, kisha kwake mtarejeshwa?."Qur an Suratul Baqara Aya ya 28.

M/Mungu kaanza Kutuumbia Kifo kisha Ukaumbwa Uhai Hii ni dalili kwamba tuishi Maisha yote ya Dunia lakini Siku ikifika Tutaiacha hii Dunia.

M/Mungu anasema tena katika Qur an " AMETUKUKA ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.

Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha." Qur an Surat Al Mulk aya ya 1-2.

Ukiangalia Aya ya Pili utaona kuwa Mauti ndio Mwanzo kuumbwa kabla ya Uhai hii ni dalili ya kuwa Mauti yapo kama Mlango kuingia katika Mlango huo ni lazima.

Maandalizi mema ya Safari hii ni kufanya Matendo Mema ili kupata Radhi zake M/Mungu Pekee .

Mshairi Mmoja atukumbusha kwa kutwambia

LAU INGEKUWA DUNIA INABAKI MILELE NA WATU WAKE

BASI ANGE BAKI MTUME MUHAMMAD (S.A.W) YU HAI MILELE DAIMA.

Tujiandae na Safariii Ndugu zangu Wapendwa .

M/MUNGU ATUPE MWISHO MWEMA NA ATUKUTANISHE NA WAJA WAKE WEMA PEPONI SISI NA WAZAZI WETU NA WAISLAM WOTE KWA UJUMLA . AMIIN AMIIN AMIIN

LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO)


Dhumuni kuu la kuandika Makala hii Nikutaka kukumbushana Siku hii Muhimu katika Siku ambazo Ndio zimeufanya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani kuwa Mwezi Mtukufu nayo Ni Siku ya LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO) ambayo ipo katika Kumi hili la Mwisho ambalo tumelianza.

LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO) NI USIKU AMBAO UNAPATIKANA NDANI YA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI NDANI YA KUMI LA MWISHO MTUME (S.A.W) LILIPOKUWA LIKIINGIA KUMI LA MWISHO ALIKUWA AKIZIDISHA IBADA KWA SANA NA KUWA AMSHA WATU WAKE ( ALHAL BAYTI ) KWA AJILI YA KUFANYA IBADA ZAIDI KATIKA KUMI HILO.

LAYLATU QADIR SI MWEZI 27 TU ILA WENGI WA WANACHUONI WAMEJITAHIDI KUWA HIYO NDIO SIKU YA LAYLATUL QADIR

SIKU HII HUENDA IKAPATIKANA NDANI YA MWEZI 21 , 23 , 25 , 27 , 29 , NI JUU YETU NDUGU ZANGU KUITAFUTA SIKU HII KWA KUFANYA
IBADA KWA WINGI NDANI YA KUMI LA MWISHO ILI M/MUNGU ATUWEZESHE KUIDIRIKI SIKU AMBAYO UBORA WAKE KWA WENYE KUUDIRIKI USIKU HUU KWA IBADA NI ZAIDI YA MIEZI 1000 NA HUSHUKA MALAIKA NDANI YA SIKU HIYO KWA IDHINI YA M/MUNGU NA MALAIKA JIBRIL HUSHUKA.

NI JUU YETU KUHAMASISHANA NAKUKUMBUSHANA KUWA SIKU HII NI SIKU MOJA NA NI MUHIMU SANA ILI KUPATA KUMUOMBA M/MUNGU .

Katika Mambo ambayo yame kokotezwa (Sunnah) katika Kumi hili la Mwisho Ni Kikazi cha Itkafu na Maana ya ITKAFU KI SHAARIA ni Kushikamana na Msikiti na kukaa ndani yake pasina ya kutoka kwa ajili ya kujikurubisha(kuwa karibu) kwa M/Mungu Mtukufu .

Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu katika kila Mwaka ndani ya kumi la mwisho la Ramadhani na Mwaka alio fariki alikaa itikafu muda wa siku ishirini Kama ilivyo pokelewa na Bukhari.

Vile vile Maswahaba wa Mtume na Wake zake walikaa nae itikafu na walikaa Itikafu baada ya mtume kufariki.


M/MUNGU AKIKUBARIKI KUIDIRIKI USIKU HUU WA CHEO SOMA DUA HII KWA MAELEKEZO YA MAMA AISHA
alimuliza Mtume Jee? tukiidiriki LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO) tufanye nini ? Mtume akajibu kithirisha kusema ALLAHUMA INNAKA AFUWUN TUHIBUL AFWAA FA'AFUANNAA ". Kama alivyosema Mtume

MUNGU NDIYE MJUZI WA HII SIKU NI JUU YETU NA FAMILIA ZETU KUZIDISHA IBADA .


JUMUIYA YA KUHIFADHISHA QUR’AN TUKUFU TANZANIA NA TANZANIA MUSLIM HAJJ TRUST.

WANAWAKARIBISHA WAISLAM WOTE KATIKA
MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR’AN TUKUFU YA KIMATAIFA

FAINALI KWA WASICHANA


Saa 3:00 ASUBUHI
Ukumbi: Star Light Hotel Hall
(Waalikwa Wanawake tu).


FAINALI KWA WANAUME

Jumapili , Tarehe 04 Agosti 2013,
Saa 3:00 ASUBUHI
Ukumbi:Diamond Jubilee Hall
(Waalikwa Wanaume na Wanawake).

Changia kuendeleza kuhifadhisha QUR’AN Tukufu Tanzania kupitia Mtandao wetu www.quran.or.tz

Tunawashukuru na kuwatakia Funga Njema yenye Baraka na kukubaliwa Dua zetu ambazo tunazo ziomba , Amiin .

Kwa Niaba ya Kamati ya Maandalizi.