Saturday, August 31, 2013

BUNGE LA TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA MABUNGE YA SADC




Mahmoud Ahmad Arusha
Bunge la Tanzania kupitia kamati yake ya hesabu za serekali (PAC)litakuwa mwenyeji wa mkutano wa 10 wa umoja wa kamati za mabunge za hesabu za serekali kutoka nchi wanachama wa SADC ujulikanao kama Southern African Development community oganization of public Account Commitees(SADCOPAC).
Mkutano huo wa siku sita utafunguliwa rasmi tarehe 2-6september mwaka huu na kubeba kauli mbiu “ukuzaji wa uwezo wa mabunge kusimamia matumizi ya rasilimali za umma ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa katika mkutano huo.
Akizngumza na vyombo mbalimbali vya habari jijini hapa mwenyekiti wa SADCOPAC Sipho Makama amesema kuwa mkutano huo utawashirikisha zaidi ya wajumbe 300 ambao ni wabunge kutoka kamati za hesabu za serekali,wakaguzi na wadhibiti wa hesabu za serekali,wahasibu wakuu wa serekali,makatibu wa kamati za PAC,Maspika wa mabunge ya SADC pamoja na wahisani kutoka Taasisi mbalimbali za kimataifa.
Aidha alisema kuwa wakati wa ufunguzi wa mkutano huo pia utazinduliwa umoja kama huo kwa ngazi ya Afrika ujulikanao kama AFROPAC pamoja na mambo mengine mkutano huo utatoa fursa kwa wajumbe kujadili mbinu mpya za kuwezesha kamati hizo pamoja na ofisi ya CAG kufanya ukaguzi unaolenga kubainisha thamani ya fedha za miradi inayotekelezwa.
Huku akitanabaisha kuwa manunuzi yanaofanywa katika kanda ya SADC ambapo siku hiyo ya ufunguzi Tanzania itawasilisha mada juu ya jukumu la kamati za hesabu za serekali katika kukabiliana na usafirishaji wa fehda haramu na ukwepaji kodi.
“Hapa majukumu ya kamati zetu kwenye umoja wetu yanatakiwa kwenda na wakati katika kukabiliana na changamoto za matumizi mabaya ya madaraka na fedha za umma”amesema Sipho.

No comments:

Post a Comment