Saturday, August 17, 2013

HAKIKA HALALI IKO WAZI NA HARAMU IKO WAZI


 Kutoka kwa  Abu Abdullah An-Nu’uman Ibn Bashiyr  Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake , alisema: Nilimsikia Mtume Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani  akisema : Halali iko wazi na haramu iko wazi, baina yao ni vitu vyenye shaka ambavyo watu wengi hawajui.
   Kwa hivyo, yule anayeepuka vyenye shaka  anajisafisha nafsi yake kwenye dini yake na heshima yake, lakini yule anayetumbukia katika mambo yenye shaka, huanguka katika haramu, kama mchunga anayechunga pembezoni mwa mpaka, mara  huingia ndani (ya shamba la mtu).  Hakika kila mfalme ana mipaka yake, na mipaka ya M/Mungu Mtukufu  ni makatazo Yake. 
Na hakika katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama kikitangamaa, kiwiliwili chote kitakua kizima, kikharibika kiwiliwili chote huharibika.
 Basi jua (kipande hicho cha nyama) ni moyo.

Hadithi hii imesimuliwa na Imamu Bukhari na Muslim.
----------------------------------------------------------------
"إن الحلال بين وإن الحرام بين"
عَنْ أبي عَبْدِ اللهِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُما قَالَ : سمعتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: 
 إن الْحَلالَ بَيِّنٌ وَإنَّ الْحَرَامَ بَيِّنٌ وَبَيْنَهُما أمورٌ مُشْتَبِهَاتٌ لا يَعْلَمُهُنَّ كَثيِرٌ مِنَ الناسِ، فَمَنِ اتَّقَى الشُّبُهَاتِ فَقَد اسْتَبْرَأَ لِدِينِهِ وَعِرْضِهِ، وَمَنْ وَقَعَ في الشَّبُهاتِ وَقَعَ في الْحَرَامِ، كالرَّاعِي يَرْعَى حَوْلَ الْحِمَى يُوشِكُ أَنْ يَرْتَعَ فِيهِ، أَلا وَإنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمىً أَلا وَإنَّ حِمَى الله مَحَارِمُه، أَلا وَإنَّ في الجَسَدِ مُضْغَةً إذَا صَلَحَتْ صَلَحَ الْجَسَدُ كُلُّهُ وإذَا فَسَدَتْ فَسَدَ الْجَسَدُ كُلُّهُ، أَلا وَهِيَ الْقَلْبُ.
  رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ  وَمُسْلِمٌ

No comments:

Post a Comment