Wednesday, August 21, 2013

JK APANGUA MAKATIBU WAKUU
Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko katika nafasi za ukatibu mkuu na unaibu katibu mkuu katika wizara mbalimbali kwa kuwateua makatibu na manaibu wapya na kuwahamisha wengine kutoka wizara moja kwenda nyingine.

Haya yanatajwa kuwa mabadiliko makubwa tangu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 na wengi wa sasa wametemwa.

Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu saa 10 jioni, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alitangaza mabadiliko hayo kama ifuatavyo:

MAKATIBU WAKUU

Jumanne Sagini amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) awali alikuwa Naibu Katibu Ofisi wa Waziri Mkuu - TAMISEMI.

Dk. Servacius Likwalile amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha,awali alikuwa Naibu Katibu

Dk. Patrick Makungu- Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika wizara hiyo

Alphayo Kitanda- Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, awali alikuwa Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.

Dk. Shaaban Mwinjaka - Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi,awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko,

Dk.Uledi Mussa-Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, awali alikuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Profesa Sifuni Mchome- Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, awali alikuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.

Charles Pallangyo - Katibu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu

Anna Maembe -Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo

Sihaba Nkinga- Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo

Sophia Kaduma- Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.


NAIBU MAKATIBU WAKUU WAPYA WALIOTEULIWA NI:

Angelina Madete- Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,

Regina Kikuli -Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,

Zuberi Sumataba -Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI anayeshughulikia suala la elimu

Edwin Kiliba -Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI.

Dk. Yamungu Kayandabila -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika,

Profesa Adolf Mkenda -Naibu Katibu Mkuu ya Fedha anayeshughulikia sera,

Dorothy Mwanyika -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha anayeshughulikia Fedha za Nje na Madeni.

Rose Shelukindo -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,

Dk. Selassie Mayunga -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,

Monica Mwamunyange -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi,

Consolata Mgimba -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Profesa Elisante ole Gabriel Laizer -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Armantius Msole -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

WALIOPEWA UHAMISHO NI:

John Mngondo amehamishiwa Wizara ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ametoka Wizara ya Uchukuzi,

Selestine Gesimba - Wizara ya Maliasili na Utalii anatoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,

Injinia Ngosi Mwihava anahamia Wizara ya Nishati na Madini kutokea Ofisi ya Makamu wa Rais.

Maria Bilia -Wizara ya Viwanda na Biashara kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi .

Nuru Milao anahamia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na W-atoto kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

No comments:

Post a Comment