Monday, August 19, 2013


MAHAKAMA YA MISRI YAAMURU MUBARAK AACHIWE HURU


Mahakama ya Misri imeamuri kiongozi wa zamani, Hosni Mubarak, kuachiliwa huru baada ya mahakama hiyo kusema kuwa hakupatwa na hatia katika kesi iliyokuwa imebakia ya ubadhilifu.

Kwa mujibu wa wakili wake na duru za mahakama za Misri, leo Jumatatu korti imeamuru Mubarak aachiliwe huru katika kesi ambayo yeye na watoto wake wawili Alaa na Gamal walikuwa wakituhumiwa kufanya ubadhilifu wa fedha za umma.

Taarifa hiyo inasema kwamba, Mubarak anaweza kuachiliwa huru wiki hii, lakini watoto wake wawili wataendelea kushikiliwa. Huko nyuma pia iliamriwa kwamba kiongozi huyo wa zamani aachiliwe huru katika kesi nyingine mbili ambapo alishitakiwa kuhusika katika mauaji ya waandamaji wakati wa harakati za maandamano ya mwaka 2011 ambayo yalimuaondoa madarakani na pia kujilimbikizia mali kinyume cha sheria.

Wamisri wengi wanaamini kuwa Mubarak aliyekuwa kibaraka mkubwa wa Marekani na Israel wakati wa utawala wake anapaswa kuhukumiwa kifo kutokana na kuwaua waandamanaji.

CHANZO: IRIB

No comments:

Post a Comment