M/MUNGU MTUKUFU NI MWEMA ANAKUBALI KILICHO CHEMA TU.
Kutoka kwa Abu Hurayra Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani amesema: Amesema Mtume Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani,
M/Mungu Mtukufu ni Mwema na anakubali kilicho chema tu.(hakubali kisicho chema au kizuri).
Na Hakika ya M/Mungu Mtukufu ameamrisha Waislamu kufanya yale aliyowaamrisha Mitume, amesema M/Mungu Mtukufu "Enyi Mitume Kuleni katika vitu vyema na mfanye yaliyo sawa" . M/Mungu Mtukufu amesema :" Enyi mlioamini kuleni katika vitu vyema ambavyo
tumekuruzukuni” Kisha akataja (kisa cha yule) mtu aliyesafiri safari
ndefu, kachafuka na kajaa mavumbi na huku anayanyua mikono yake mbinguni
akisema "Ewe Mola! Ewe Mola! Nipe kadhaa, nikinge na kadhaa wakati
chakula chake cha haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na kivazi
chake ni cha haramu, na anashibishwa na haramu, je, vipi atajibiwa
(dua zake?).
Hadithi Imepokelewa na Imamu Muslim
No comments:
Post a Comment