MUENDELEZO MPYA WA MKASA WA SHEIKH ISSA PONDA
Assalam Alaykum
Ndugu Waislamu na Wote Wapenda Amani
Napenda kuwapa up-date ya Mtihani wa Sheikh wetu, Ponda Issa Ponda
Mchana huu amepelekwa Hospitali moja ya Jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi (maana risasi bado iko mwilini)
Jina la Hospitali litatajwa jioni ya leo Katika Msikiti wa Mtambani, in Shaa Allah
Anaejua jina hilo anaombwa ASILITAJE MPAKA MUDA HUO ili watu wasiiende
Hospitali kabla ya kuhudhuria Kongamano la Alaasisiri ya leo (soma
chini)
PIA,
Ndugu Waislamu MNAOMBWA LEO SAA 10.00
ALAASIRI MUHUDHURIE KONGAMANO KUBWA litakalofanyika Katika Msikiti wa
Mtambani, Kinondoni, Dar es Salaam, mara tu baada ya Swala ya Alaasir
(saa 10.15 jioni)
Vile vile mnaombwa kutuma taarifa hii kwa email na kutumia sms ili wengi wahudhurie kwa wingi
Zaidi ya hayo, tuongeze Dua kwa Sheikh Ponda na Familia yake katika kipindi hiki kigumu zaidi
___________________________________________________________
Shura
ya Maimamu chini ya Sheikh Kundecha Musa Kundecha imeitaka serikali
kuunda tume huru kufanya uchunguzi kuhusu kadhia ya kujeruhiwa kwa
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa
Ponda.
 |
Sheikh Ponda |
Katika mkutano wake na waandishi wa habari katika
Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam, Amiri Kundecha aliyeongozana
na wakili wa Sheikh Ponda, Bwana Nassoro Juma, ameitahadharisha serikali
kuwa inaelekea kupoteza imani yake kwa wananchi, hususan Waislamu,
kutokana na dalili zote kuonesha kuwa polisi ndio waliohusika na tukio
hilo.
 |
Jeraha alilopata |
Tamko hili pia Limeungwa mkono na Baraza kuu la Waislamu Tanzania Bakwata la kuundwa tume huru ya Uchunguzi wa tukio hili hayo yamesemwa na Sheikh Alhad Mussa Salum Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam kwa Niaba ya Mufti wa Tanzania katika kUPINGA KITENDO KILICHOTOKEA KWANI JESHI LA POLISI LILIKUWA NA UWEZO WA KUMKAMATA NA KUFIKISHA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA,
No comments:
Post a Comment