Rais
wa Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe, anaapishwa rasmi leo kwa awamu ya
saba kama kiongozi wa taifa hilo, ikiwa ni siku chache baada ya mahakama
nchini humo kuthibitisha matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 31
mwezi uliopita, ambao matokeo yake yalipingwa na mpinzani wake, Morgan
Tsvangirai. Chama cha Tsvangirai, cha Movement for Democratic Change,
MDC, kimesusia sherehe ya kuapishwa kwa Mugabe katika uwanja wa mpira
mjini Harare.
No comments:
Post a Comment