Pages
MWANZO
MAKALA
FIQH
SIRA
IJUMAA
AZHAR SHAREEF
PICHA NA MATUKIO
TASFIRI YA QUR AN
UTAMBULISHO.
LIKE OUR PAGE ON FACEBOOK
Sunday, September 22, 2013
ABDULRAHMAN KINANA AMJULIA HALI MKUU WA MAJESHI MSTAAFU JENERALI MUSUGULI BUTIAMA, AENDELEA NA ZIARA WILAYANI SERENGETI
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Jenerali David Musuguli Mkuu wa Majeshi Mstaafu wakati alipomtembelea na kumjulia hali Mjini Butiama leo, wakati akiondoka wilayani humo kuelekea Mugumu Wilaya ya Serengeti kuendelea na ziara yake ya kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho, Jenerali Musuguli alionekana kuwa na bashasha wakati alipomuona Abdulrahman Kinana pengine ni kutokana na utendaji kazi wa katibu mkuu huyo wa CCM, ambapo alisikika akisema huyu ni kijana wangu huku wakiwa wameshikana mikono wakiingia ndani kwa mazungumzo ya faragha.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MUGUMU SERENGETI
Jenerali David Musuguli Mkuu wa Majeshi Mstaafu akisalimiana na Nimrod Mkono Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi CCM.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali David Musuguli nyumbani kwake Butiama.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo huku Mkuu wa Wilaya ya Butiama Angelina Mabula akisikiliza kwa makini.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Jenerali David Musuguli wakiingia ndani huku wakiwa wameshikana mikono.
Jenerali David Musuguli akipiga picha ya kumbukumbu na
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana, na maofisa kadhaa ambao ameongozana nao katika msafara huo, kushoto ni Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Nimrod Mkono.
Jenerali David Musuguli akipiga picha ya kumbukumbu na
waandishi wa habari
, kushoto ni Nimrod Mkono Mbunge wa Musoma vijijini.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na
Jenerali David Musuguli wakati alipomtembelea nyumbani kwake leo.
Jenerali David Musuguli
akiagana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi huku wakionekana kufurahia jambo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika kata ya Isenye wilaya ya Serengeti
Akisalimiana na na wana CCM walipokuwa wakimlaki leo
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana aki
angalia kikundi cha ngoma wakati kikitumbuiza.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nata wilayani Serengeti leo.
Wimbo wa taifa
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Nata wakiimba wimbo wa taifa.
Mwalimu Mwema Machage wa Darasa la Kompyuta katika shule ya sekondari ya Nata akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakati alipokagua shule hiyo
Mwalimu Peter Simon wa shule ya Sekondari ya Nata wilayani Serengeti akielezea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jinsi wanavyowafundisha wanafunzi wake somo la sayansi wakati alipotembelea maabara ya shule hiyo.katikati ni mwanafunzi wa kidato cha nne Silvesta Joseph
mwanafunzi wa kidato cha nne Silvesta Joseph akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM kuhusu wanafunzi hao wanavyojifunza jinsi ya kutengeneza sabuni katika maabara hiyo ya shule.
Wananchi wakimpungia mkono Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Kinana akizungumza na wananchi katika kata ya Isenye
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mgorole na Mzee Nyangarisi Kumari kuwa mmoja wa wazee wa heshima wa kimila wa kabila la Kiikoma tukio hilo limefanyika katika kata ya Bukore.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kutawazwa mzee wa heshima wa kabila la Kiikoma katika kijiji cha Bukore wilayani Serengeti
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment