DK SHEIN AONGOZA HARAMBEE MKOA WA KUSINI KARAFUU HOTEL
Baadhi ya Wananchi na wanachama Chama cha Mapinduzi walioalikwa katika hafla ya Harambee ya kukichangia Chama Mkoa wa Kusini Unguja iliyofanyika jana katika Hoteli ya Karafuu,Michamvi Wialaya ya Kati .
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini CCM Mohamed Raza Daramsi,akiimba wimbo usemao “Mpewa hapokonyeki” wakati kikundi cha Culture Muzicul Club kilipocharaza ala zake jana katika hafla ya Harambee ya kuchangia Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja huko Karafuu Hotel Michamvi Wilaya ya Kati.
Kikundi cha Burudani kikitoa burudani katika harambee hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akimkabidhi Fedha Tasilim Shilingi za Kitanzania Milioni Moja katibu wa Kikundi cha Culture Muzical Club Said Mwinychande,wakati wa hafla ya Harambee ya kuchangia Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja huko Karafuu Hotel Michamvi Wilaya ya Kati.
Mbunge wa Jimbo la Muyuni Mahadhi Juma,(kulia)akionesha Cheti alichokabidhiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,(katikati)kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe,kwa mchango wake alioutoa kwa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini katika hafla ya Harambee iliyofanyika jana Karafuu Hotel Michamvi,Wilaya ya Kati (kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Kati Vuai Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM
Zanzibar,akimakabidhi Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa Mkoa wa Kusini Unguja Jafar Sanya,cheti kwa kukichangia chama cha Mapinduzi katika hafla iliyofanyika huko Karafuu Hotel Michamvi Wilaya ya Kati,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akipokea fedha tasilim shingi za Kitanzania Milioni Moja kutoka kwa Mohamed Naushad,wakati wa Hafla ya kukichangia Chama cha mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja,huko katika Hoteli ya Karafuu Michamvi Wilaya ya Kati jana.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh,alipokuwa akitoa kauli ya kuchangia Shilingi Milioni Moja wakati wa Hafla ya kukichangia Chama cha mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja,huko katika Hoteli ya Karafuu Michamvi Wilaya ya Kati jana.
Kamanda wa UVCCM (M) Misungwi John Buyamba,akionesha picha baada ya kuinuua kwa Shilingi Milioni Moja fedha za Kitanzania katika hafla ya kuchangia Chama cha Mpainduzi Mkoa wa Kusini Unguja,iliyofannyika jana Karafuu Hotel Michamvi Wilaya ya Kati,(kulia Mkuu wa Wilaya ya Kati Vuai Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akitoa hutuba yake wakati wa hafla ya Harambee ya kukichangia Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja,huko Karafuu Hotel Michamvi Wi laya ya Kati jana,katika hotuba yake aliwashukuru Viongozi na wananchi kwa kuonesha moyo wao wa kujitolea katika chama.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha Culture musical Club,jana baada ya kumalizika kwa hafla ya Harambee ya kuchangia Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja huko Karafii Hotel Michamvi Wialaya ya Kati.
[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
No comments:
Post a Comment