Tuesday, September 17, 2013

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE JIMBO LA KISESA (SIMIYU)

1a
Katibu Mkuu Ndugu  wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kisesa Mh.Luhaga Mpina mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mwandoya tayari kwa kufanya ziara yake katika jimbo la Kisesa Wilayani Meatu Mkoa mpya wa Simiyu , ambapo amepokelewa na wananchi na kufanya shughuli mbalimbali katika jimbo hilo ikiwa ni pamoja na kukagua miradi ya maendeleo kuzungumza na waenyeviti wa mashina na matawi ya  chama cha Mapunduzi na kunalizia ziara yake katika jimbo hilo kwa kufanya mkutano wa hadhara katika kata ya Mwasengela, Ziara hiyo ina lengo la kimaisha Chama, Kuamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na Kuhimiza serikali katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho, Ndugu Abdulrahman Kinana amewasili katika jimbo la Bariadi ambapo ataendelea na ziara yake leo na kumalizia kesho Kabla ya Kuanza ziara nyingine kama hiyo mkoa wa Mara.
2a
Katibu Mkuu Ndugu  wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama katika jimbo hilo mara baada ya kuwasili jimboni Kisesa Jana.
3a
Wananchi wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM katika kijiji cha Mwasengela jimboni Kisesa Jana.
4a
Katibu Mkuu Ndugu  wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana wa kwanza  kulia akiongozana na Nape nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi  na viongozi wa Jimbo la Kisena na Wilaya ya Meatu kuelekea katika eneo la mkutano mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mwandoya. oKatibu Mkuu Ndugu  wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwandoya hawapo pichani mara baada ya kuwasili kijijini hapo Jana
6a
Kijiko kikiendelea na uchimbaji wa mtaro utakaojengwa nguzo za daraja la mto wa Mongobakima kata ya Mwasengela ambapo ujenzi wa daraja hilo umeanza.
7a
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Pasons Company Limited wakiendelea na kazi katika ujenzi wa daraja hilo.
8a
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Meatu Bw.John Wanga akizoma taarifa ya ujenzi wa daraja la Mongobakima  kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipotembelea ujenzi wa daraja hilo Jana.
9a
Katibu Mkuu Ndugu  wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinanapamoja na ujumbe wake wakishuhudia ujenzi wa daraja hilo. 
10a
Mkandarasi wa daraja hilo Bw,. George wa kampuni ya Pasons Company Limited akifafanua jambo kwa  Katibu Mkuu Ndugu  wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana wakati alipokagua ujenzi wa daraja hilo Jana, kushoto nia Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM na kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani
11a
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kutoka kushoto akiwasili katika kata ya Mwasengela pamoja na ujumbe wake
12a
Wananchi wakipunga mikono kuupokea ugeni huo
14a
Ugeni huo ukielekea eneo la mkutano wa hadhara.
15a
Katibu Mkuu Ndugu  wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana akiwapungia wananchi mkono mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano.
16a
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mh. Rosemary Kirigini akizungumza na wana Mwasengela
17a
Mh Luhaga Mpina Mbunge wa jimbo la Kisesa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kata ya Mwasengela.
18a 19a
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kata ya Mwasengela leo.
29a
Katibu Mkuu Ndugu  wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mwasengela jimboni Kisesa Wilayani Meatu katika mkoa wa Simiyu kushoto ni Mbunge wa jimbo la Kisesa Mh Luhaga Mpina.


PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-KISESA SIMIYU.

No comments:

Post a Comment