Monday, September 23, 2013

MAZISHI YA MMOJA WALIOFARIKI KATIKA UVAMIZI WA JENGO LA KIBISHARA LA WESTGATE - NAIROBI - KENYA

Waombolezaji wakifanya mazishi ya mmoja wa marehemu aliyeuawa katika shambulio la ugaidi jijini Nairobi.
Mmoja wa majeruhi katika tukio hilo akisaidiwa na wananchi.
Wanausalama wakitoa msaada kwa mama huyu na mwanaye.
UVAMIZI wa duka kubwa la Westgate jijini Nairobi ulioanza Jumamosi iliyopita na kusababisha makumi kadhaa ya mauaji na majeruhi ya watu waliokutwa sehemu hiyo, umekuwa ukifanyika bila kujali dini wala utaifa wa watu waliozingirwa sehemu hiyo.
Miongoni mwa watu ambao wameonyesha ujasiri  katika juhudi za kuwaokoa waathirika wa shambulio hilo la kigaidi ni Waislam ambao, kwa kutumia silaha zao halali, walipambana vikali na magaidi hao na hivyo kutoa mwanya kwa mateka wengi kuondoka sehemu hiyo ya mauaji.
Watu hao walioshiriki katika kuokoa maisha ya mamia ya Wakenya na watu wa mataifa mengine wasio na hatia ni Abdul Yusuf na Ali ambao walijitoa mhanga maisha yao kwa kushirikiana na Waislam na Wakenya wengine katika juhudi za uokoaji , Katika shambulio hilo ambalo baadhi ya waliokufa wameanza kuzikwa, lilifanywa bila kulenga watu wa jamii yoyote kwani waliokumbwa na vifo na waliojeruhiwa kwa mamia ni watu wa dini na mataifa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment