
Kulingana na utafiti uliofanywa na mwandishi wa makala hii katika vijiwe, baadhi ya vijana wamebuni utamaduni wa kufanya mazoezi ya kubeba dawa za kulevya tumboni kwa kumeza mbilimbi bila kutafuna, ili iwapo itatokea nafasi ya aina hiyo muda wowote, wawe tayari kuingia kazini. Uchunguzi uliofanywa maeneo ya Kinondoni, Magomeni, Vingunguti, Manzese, Msasani, na Temeke, umegundua zao la mbilimbi limekuwa likitumika kama kifaa cha kupima uwezo wa mbebaji wa dawa za kulevya.
Kulingana na utafiti uliofanywa na mwandishi wa makala haya katika vijiwe, baadhi ya vijana wamebuni utamaduni wa kufanya mazoezi ya kubeba dawa za kulevya tumboni kwa kumeza mbilimbi bila kutafuna, ili iwapo itatokea nafasi ya aina hiyo muda wowote, wawe tayari kuingia kazini.
Uchunguzi uliofanywa maeneo ya Kinondoni, Magomeni, Vingunguti, Manzese, Msasani, na Temeke, umegundua zao la mbilimbi limekuwa likitumika kama kifaa cha kupima uwezo wa mbebaji wa dawa za kulevya.
Sababu kubwa ya kutumiwa kwa mbilimbi ni ukweli kwamba ukubwa wa kete za dawa za kulevya unakaribiana na ule wa zao hilo (mbilimbi).
Mwandishi alishuhudia vijana wakiwa katika makundi ya watu 10 hadi 15, kwa nyakati tofauti wakiwa natika vijiwe wakishindana kumeza mbilimbi bila kutafuna. Kuna baadhi walionekana kuwa na uwezo wa kumeza mpaka mbilimbi 30 kwa robo saa, huku wengine wakienda mbali zaidi ya hapo, japo wengine walionekana kushindwa.
Kwa mujibu wa maelezo yao ni kwamba ukifikia hatua hiyo, unapewa cheo cha Punda, jina linalomaanisha kuwa uko tayari kubeba mzigo na kusafirisha kwenda nchi yoyote utakayotumwa.
Kwa mujibu wa vijana hao, wale wanaoonekana kumeza mbilimbi hizo ndio huchukuliwa, na kutengenezewa pasi za kusafiria na kuendelea kupewa miongozo mingine. Kutokana na mazoezi hayo, inasemekana hata upatikanaji wa zao hilo ambalo mara nyingi hutumika kutengeneza chachandu, umeanza kuwa wa taabu hasa baada ya bei yake kupanda tofauti na awali.
Baadhi yao huwalazimu watumiaji kuagiza tunda hilo kutoka katika Mkoa wa Tanga, na wengine Mombasa, Kenya ambako hupatikana kwa wingi.
“Kwa Dar es salaam, Mbilimbi zinapatikana Kisutu tu kwa sasa na kwa baadhi ya watu ambao wamepanda miti labda uani kwao na sio kubwa kama zile ambazo tunatakiwa kumeza kwa hiyo inabidi sasa kuanza kuingia mikoani kuzisaka”, alisema mmoja wa vijana waliokutwa maeneo ya Feri, Dar es Salaam.
Inasemekana kutokana na uhaba wa matunda hayo ambayo hustawi sana katika mikoa ya Pwani, wakazi wengi wa Jijini Dar es Salaam wameanza kulima miti hiyo ndani ya uzio wa nyumba zao ili kuweza kuhudumia wateja wao kwa ukaribu.
Maeneo ya Magomeni Mikumi yanatajwa kuwa maarufu kwa zao hilo, wakazi wengi hasa kinamama wamekuwa wakipanda zao hilo ndani ya uzio wa nyumba zao na kulihudumia ipasavyo ili kupata matunda yenye ukubwa unaotakiwa kwa ajili ya matumizi ya vijana wanaofanya mazoezi ya kubeba mzigo. Hata hivyo si wote wanaopanda mbilimbi kwa ajili ya kujifanyia mazoezi ya dawa za kulevya.
CHANZO CHA MAKALA : MWANANCHI
No comments:
Post a Comment