MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AZURU NEBRASKA NCHINI MAREKANI
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Founder, Benefactor and Chief Executive Officer wa Taasisi ya Opportunity Education Bwana Joe Ricketts kwenye uwanja wa ndege katika mji wa Omaha uliopo katika Jimbo la Nebraska nchini Marekani tarehe 27.9.2013
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Kate Stephens, 7, mara baada ya Mama Salma kutua kwenye uwanja wa ndege wa Omaha huko Nebraska nchiniMarekani tarehe 27.9.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyeshwa na Bwana James Ricketts, President and Chief Operations Officer, wa Taasisi ya Oppoturnity Education shughuli mbalimbali za kununua na kusafirisha vifaa vya elimu kwenda kwenye shule katika nchi mbalimbali hapa duniani ikiwamo Tanzania wakati Mama Salma alipotembelea Taasisi hiyo yenye Makao Makuu yake huko Omaha katika Jimbo la Nebraska nchini Marekani tarehe 27.9..2013.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya ngao kutoka kwa Bwana Joe Ricketts, Founder, Benefactor and Chief Executive Officer wa Taasisi ya Opportunity Education iliyoko huko Omaha nchini Marekani. Bwana Ricketts alitoa zawadi hiyo kwa kutambua mchango mkubwa sana alioufanya Mama Salma binafsi na Taasisi yake ya WAMA Foundation katika masuala ya elimu. Afya na uwezeshaji kwa akina mama..
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia waalikwa waliohudhuria Gala to support Global Education iliyoandaliwa kwa ajili ya kumtunuku tuzo maalum Bwana Joe Ricketts kwa juhudi zake za kuboresha elimu duniani hasa katika nchi zinazoendelea.
PICHA NA JOHN LUKUWI
No comments:
Post a Comment