Wednesday, September 25, 2013

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA MONMOUTH HUKO NEW JERSEY-MAREKANI

IMG_2505Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokelewa rasmi na Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth kilichoko huko New Jersey nchini Marekani mara tu baada ya kuwasili chuoni hapo tarehe 24.9.2013. Mama Salma yupo nchini Marekani akifuatana na Rais Jakaya Kikwete anayehudhuria Mkutano wa 68 wa Umoja wa Mataifa unaofanyika New York.IMG_2528Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Chuo Kikuu cha Monmouth baada ya kuwasili chuoni hapo. Kulia kwa Mama ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi akifuatiwa na Naibu Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ramadhani Mwinyi, na Ms Janet Mahoney,wa Chuo Kikuu cha Monmouth na kushoto kwa Mama Salma ni Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu hicho, Bwana Saliba Sarsar, Makamu Rais wa Chuo cha Monmouth anayeshughulikia mahusiano ya kimataifa na Mwisho ni Bwana John McLaughlin, kutoka Shirika la Footprints for Education International la nchini Marekani.
IMG_2564Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongoza kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth hasa katika masuala ya kuwaongezea uwezo wauguzi na wakunga. Mama Salma Kikwete aliongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.IMG_2619Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akijadiliana jambo na Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth baada ya Mama Salma kumkabidhi Jarida litolewalo na Taasisi ya WAMA .
PICHA NA JOHN LUKUWI. 

No comments:

Post a Comment