
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Karatu baada ya kuwasili kwenye Lodge ya Bashay Rift akiwa njiani kuelekea Enduleni wilayani Ngorngoro, Septemba 19, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kushoto) wakipokea salamu maalum kutoka kwa wasichana wa Kibarabaig baada ya kuwasili katika kijiji cha Enduleni wilayani Ngorongoro Septemba 9, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya cha Enduleni wilayani Ngorongoro Septemba 19, 2013.
Baadhi ya Wazee wa Kimasai wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alizungumza nao kwenye Kituo cha Afya cha Enduleni wialyani Ngorongoro Septemba 19, 2013.
Mwananchi wa Kijiji cha Enduleni wilayani Ngorongoro akinyosha mkono kuomba kumuuliza swali Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye alihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hichoSeptemba 19, 2013.
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments:
Post a Comment