Mkuu
wa Chuo Cha Ualimu Vikindu Bi.Theodosia Rwechungura akiteta jambo na
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais Kikwete alipokwenda chuoni
hapo Kukagua ujenzi na Kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la
Utawala na Mabweni chuoni hapo.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi
Mkoani Pwani kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkuu wa Chuo Cha ualimu Vikindu Bi.
Theodosia Rwechungura wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua
ujenzi wa Jengo la Utawala na Mabweni katika Chuo hicho huko
Vikindu,Wilaya ya Mkuranga,Mkoani Pwani jana.Kushoto ni Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete na kulia ni Waziri Wa Elimu Dkt.Shukuru Kawambwa.
No comments:
Post a Comment