Friday, August 30, 2013

MADHARA NA FAIDA ZA SIMU YA MKONONI.

Simu yako ni HATARI SANA kwenye Afya yako.
Fahamu MADHARA yatokanayo na simu yako na JINSI YA KUYAPUNGUZA.

Simu tunazozitumia hutoa mionzi (radiations) hatari sana ijulikanayo kama "Electromagnetic waves" wakati wa kupiga/kupokea simu, kuperuzi Internet, nk..

Madhara ya Mionzi hii;

1. Husababisha Saratani ya Ubongo (Brain Cancer) na ngozi (Skin Cancer).
2. Husababisha hitilafu kwenye Ubongo na hii hupelekea kupoteza kumbukumbu, uwezo mdogo wa kupambanua mambo na umakini (Concentration).
3. Husababisha upungufu wa mbegu za kiume na hata utasa (Impotence) kwa wanaume.
4. Huongeza shinikizo la damu.

Jinsi ya kupunguza Athari zitokanazo na Mionzi hii hatari;

1. Weka vifaa maalum vya kupunguza mionzi (Radiation absorbers) kwenye simu yako. Vinapatikana madukani.
2. Usipende kuweka simu mfukoni endapo huitumii. Wakati wa kulala weka mbali angalao SM 30 kutoka ulipo.
3. Simu iwapo mfukoni, upande wa Vitufe na kioo cha simu ndio kielekee mwili wako!
4. Tumia "headsets" au "Kipaza sauti (Loud Speaker). Hii hukusaidia kuwa mbali na mionzi wakati wa kupiga/kupokea simu.
5. Usiitumie simu yako iwapo ina "bar" moja au mbili za "network" (Low Network Signal). Wakati huu simu inafanya kazi kupita kiwango cha kawaida hivyo huongeza wingi wa mionzi.
6. Wakati wa kupiga simu, subiri ipokelewe ndio uisogeze karibu ya mwili (mf. Masikioni).
7. Iwezekanapo, penda kuwasiliana kwa ujumbe wa sauti (text msg) kulipo kupiga simu.

Simu ni muhimu sana katika Maisha yetu ya sasa. Hutuunganisha na ulimwengu uliogubikwa na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
Sanjari na hili, tunapaswa kuwa makini katika juhudi za kujaribu kepuka Madhara yatokanayo na simu kama ilivyoainishwa hapo juu.

Source: Internet

Prepared by;
••Athanas Chriss••

No comments:

Post a Comment