Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,akitia saini na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mafuta ya Shell ya uholanzi na Serikali za Afrika Mashariki Axel Knospe,(kushoto)makubaliano ya ushiriano katika sekta ya gesi na mafuta katika ukumbi wa ofisi ya kampuni hiyo Mjini Uholanzi alipokuwa katika ziara ya Kiserikali,ujumbe ulioongozwa na Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk.AliMohamed Shein.[Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]
Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,akibadilishana hati ya makubaliano baada ya kutia saini na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mafuta ya Shell ya uholanzi na Serikali za Afrika Mashariki Axel Knospe,(kushoto)makubaliano ya ushiriano katika sekta ya gesi na mafuta katika ukumbi wa ofisi ya kampuni hiyo Mjini Uholanzi alipokuwa katika ziara ya Kiserikali,ujumbe ulioongozwa na Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk.AliMohamed Shein.[Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mkurugenzi wa Kituo cha habari kwa wafugaji wa Ngo’mbe wa maziwa Reimond Van Gent,alipofika kuangalia familia ya ufugaji wa Ngo’mbe wa maziwa na utengenezaaji wa Jibini (Cheese) akiwa katika ziara nchini Uhiolanzi .[Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]
Hivyo ni vinoo vya Jibini (Cheese) vikiwa tayari kwa kuuzwa kwa watumiajai mbali mbali ambavyio vimwetengenezwa na Kaasboerderij captein, ambapo familia ya Watu wanne wenye kufuga Ngo’mbe wa maziwa katika mji wa Uholanzi wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,alipotembelea eneo hilo akiwa na ujumbe wake.[Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Frank Captein,namna ya utengeneza ji wa Jibini (Cheese)alipotembelea eneo hilo akiwa na ujumbe wake.[Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Frank Captein,wakati alipotembelea katika eneo maalum lililohifdhiwa Jibini (cheese) iliyokuwa imehifaddhiwa tayari kwa mauzo.[Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Frank Captein,wakati alipotembelea ndama wadogo jinsi wanavyolelewa katika famili ya BW.Captein,Nchini Uholanzi akiwa katika ziara ya kiserikali na ujumbe wake.[Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]
Ng’ombe wa Maziwa wanaofugwa na Familia ya BW.Captein jinsi wanavyopata matunzo na huduma bora za kiufugaji ,takribana Ngo’mbe hawa wanatoa Lita nyingi sana za maziwa ndiyo ambayo hutengenezewa hiyo Cheese au Jibini,[Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]
Rais wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na ujumbe wake walipotembelea katikaa kituo cha ufugaji wa ngombe wa maziwa kwa Familia ya Bw.Captein Nchini Uholanzi katika ziara ya Kiserikali. [Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]
No comments:
Post a Comment