Mtoto Salma .
Aqiyqah ni jina lililopewa kichinjwa (mnyama) anaye chinjwa kwa mtoto mchanga aliyezaliwa awe ni wa kike au wa kiume.
Ni Sunnah si waajibu / lazima .
Dalili ya hili ni maneno ya Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani aliposema: "Atakayepata mtoto na akapenda amchinjie basi na afanye hivyo; kwa mwanamume mbuzi wawili na kwa mwanamke mbuzi mmoja".kama alivyosema Mtume.Hadith hii imepokewa na Maimaam Abuu Daawuud na An-Nasaaiy kutoka kwa
‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani).
Kauli ya Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani aliposema“na akapenda amchinjie” ni dalili
kuwa ‘Aqiyqah si lazima bali ni jambo linalopendeza Muislamu kulifanya.
Lakini kwa mwenye uwezo wa kufanya hivyo basi iliyo bora zaidi kwake ni
kufanya ama yule asiye na uwezo wa kufanya hivyo, basi si lazima kwake
maana Mwenyeezi Mungu Haikalifishi nafsi yoyote ila yale yaliyo sawa na
uwezo wake na pia Hakufanya uzito katika dini.
Imethibiti
kutoka kwa Mtume wa M/Mungu (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani amesema: “Kila mtoto azaliwaye anafungamana na ‘Aqiyqah yake,
anachinjiwa siku ya saba, ananyolewa kichwa chake na anapewa jina.”
Wanachuoni wamelizungumzia neno ‘kufungamana’ hapa kuwa linaweza kuwa
linamaanisha mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni :-
A.Anakuwa kama mwenye kujisikia uzito na unyonge na mwenye kukosa wepesi na furaha maishani hadi achinjiwe.
B.Ni deni lililo mithili ya Rehani ambayo hulazimiana na mtu hadi alilipe.
Miongoni mwa Sharti kuu za chenye kuchinjwa katika ‘Aqiyqah kiwe kimesalimika na aibu
mbalimbali kwa kifupi kabisa kichinjwa hichi kinafanana na kichinjwa cha
‘Eid Adhwhaa au Eid kubwa.
|
No comments:
Post a Comment