Monday, August 05, 2013

SHARTI YA KWANZA YA KUSIHI IBADA NI UISLAM.

hukmu ya Funga ya asiyekuwa Muislamu

asiye kuwa Muislamu akifunga funga yake si sahihi 
kwanza anacho paswa kufanya ni kutamka Shahada Mbili ( Kukiri kwa Moyo na Kutamka kwa Ulimi ya kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa kweli isipokuwa M/Mungu na Mtume Muhammad (S.A.W) rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani ni Mtume wake.

kutamka kwake Shahada kuna muingiza Mtu huyo katika Uislamu na baada ya hapo Ndio anatakiwa Afunge Mwezi Mtukufu wa Ramadhani , Adumishe Swala na kutekeleza Nguzo zote za Uislamu na Ibada Nyengine. 

hivyo basi kwa wale ambao Mfano wako na wasaaidizi wa kazi au Marafiki ambao husema nao wanafunga ni bora kuwapa nasaha na kuwa ita katika Uislamu kwanza kwa Shahada baada ya hapo ndio watekeleze Ibada zao wakiwa katika Uislamu.

Rejea Qur an Sura ya 5 -  5
                       Sura ya 6 - 88
                       Sura ya 112 -1-4.

No comments:

Post a Comment