Kumbukumbu ilikuwa Siku ya Jumatano, August 22, 2012 , Songea.
HABARI ZAIDI KUHUSU CHUO HICHO.
Aidha katika uzinduzi wa Chuo hicho kinachotarajiwa kuanza kupokea
wanachuo januari ya Mwaka huu 2013 Vijana wa Kiislamu wametakiwa kujitokeza
kusoma Chuoni hapo ili kupata maadili mema katika kipindi hiki ambacho
maadili yameporomoka.
Wito huo umetolewa juzi na Mufti Simba baada ya kuweka jiwe la Msingi
katika Chuo hicho na kuwataka vijana kwa ujumla kuachana na mambo ya
kihuni na kufuata miongozo ya Qur ani tukufu.
Aliipongeza jamii ya watu wa kijiji cha Mgazini na Alhaji Kayombo
kwa kueneza uislamu kwa vitendo na kuwataka waislamu wengine kuiga mfano
huo.
Kwa upande wake Mfadhili wa msikiti huo alisema kuwa hadi sasa amejenga
misikiti mitano sehemu mbalimbali Mkoani Ruvuma kueneza dini ya
kiislamu.Alisema katika Chuo hicho wanafunzi watakuwa wakisoma kwa
miajka mitatu na kuhitimu mafunzo.
CHANZO : Mwambije Blog BOFYA HAPA
CHANZO : Mwambije Blog BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment