Saturday, August 31, 2013

SERIKALI IMETUPUUZA-MUFTI

  
MUFTI WA TANZANIA SHEIKH SHAABAN ISSA SIMBA.

 JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA,MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA AMBAYE TUME YAKE INALALAMIKIWA NA WAISLAMU KWAMBA IMEWAPUUZA WAISLAMU.
  • TUTAENDELEA KUDAI.
  • ATAKA MAKABURI YASIMAMIWE NA WAISLAMU SIYO HALMASHAURI.
Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limesema Serikali kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba  nchini imewapuuza Waislamu wa Tanzania.

Hayo yamesemwa Jana na Mufti wa Tanzania Sheikh Shaaaban Issa Simba ofisini kwake.

"Tukiwa ni Waislamu tuna haki ya kutoa maoni yetu au mapendekezo yetu kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na wanawajibu wa kutusikiliza,sisi mbali ya mambo mengine lakini pia tulipendekeza kwa tume iingize katika katiba madai ya miaka mingi ya kwamba Waislamu warudishiwe Mahakama ya Kadhi,lakini cha kushangaza rasimu ya katiba haionyeshi mapendekezo haya ya Waislamu"mwisho wa kumnukuu.


Mahakama ya kazi kwetu ni jambo la msingi sana (Ibada) na hii inawahusu Waislamu tu,asiyekuwa Muislamu hadhuriki kwa lolote,leo tume wanapolipuuza hili hali ya kuwa tulilipendekeza,ni dalili ya wazi kwamba Waislamu wa Tanzania tunapuuzwa.

"Naomba ieleweke,hitajio kubwa kwa waislamu ni kuwepo kwa Mahakama ya kadhi ambayo katiba ijayo itatambua uwepo wake,nimepitia rasimu yote nimekuta Mahakama kuu,Mahakama ya rufaa,Mahakama ya mkoa na Mahakama ya wilaya,lakini Mahakama ya kadhi hakuna,alisema kwa masikitiko makubwa" 

Aliendelea kwa kusema kwamba pamoja na kupuuzwa lakini nafasi bado ipo kwani mchakato unaendelea na wakiwa ni waislamu wataandika tena mapendekezo yao bila ya kutumia hasira.

Mufti alienda mbali zaidi kwa kumkumbusha kwamba zamani kulikuwa na makaburi kwa daraja tofauti,ambapo makaburi ya daraja la kwanza yalikuwa ni ya wazungu,daraja la pili yalikuwa ni wahindi na daraja la tatu yalikuwa ya watu wote hivyo kutaka katiba ijayo iainishe kuwa na makaburi ya Waislamu yatasimamiwa na Waislamu wenyewe badala ya sasa makaburi ya Waislamu kusimamiwa na Halmashauri.

Kwa muda mrefu waislamu wa tanzania wamekuwa wakidai kurejeshewa mahakama ya kadhi ambayo ilifutwa na serikali ya awamu ya kwanza.

katika hali ya kusiskitisha serikali ilionyesha matumaini ya kurejesha hilo lakini ilifyata mkia baada ya maaskofu kuipinga.

MUFTI WA  TANZANIA SHEIKH SHAABAN ISSA ALIPOMTEMBELEA WAZIRI MKUU MHE MIZENGO PINDA.

Habari na Munira Blog. 

No comments:

Post a Comment