MATENDO YANAYO PENDEZWA ZAIDI KUYAFANYA PAMOJA NA HUKUMU NA ADABU NDANI YA SIKU HII
1.Swala ya ijumaa ni faradhi kwa kila muislamu mwanaume aliye baaleghe,mzima wa afya , huru na mkazi wa mji.
1.Swala ya ijumaa ni faradhi kwa kila muislamu mwanaume aliye baaleghe,mzima wa afya , huru na mkazi wa mji.
Wala hailazimu kwa mwanamke,mtoto mdogo,msafiri ,mgonjwa na mtumwa. Iwapo kama watahudhuria basi watapata thawabu.
Na kutokana na uchache wa maarifa juu ya dini siku hizi katika maeneo mengi ,basi twawashauri wanawake kujitahidi kuhudhuria swala ya ijumaa ili waweze pata japo mawili matatu.Maradhi ni miongoni mwa nyudhuru za kusamehewa na swala ya ijumaa.
NB:Kwa wale ambao swala ya ijumaa si faradhi kwao waswali swala ya adhuhuri kama ilivyo katika siku nyingine za kawaida.
2.Yapendezwa kwa imamu kusoma suurat Al Sajida na Al in saan katika swala ya alfajiri.
3.Kuzidisha kumswalia mtume-Swalla Allahu alayhi wasallam-
4:Kuoga ndani ya siku hii ni sunna
Kwani Mtume rehema na amani ziwe juu yake anasema (إذا جاء أحدكم إلى الجمعة فليغتسل )
(Mwenye kuelekea msikitini kwa ajili ya swala ya ijumaa basi aoge) kama alivyosema Mtume.
(Mwenye kuelekea msikitini kwa ajili ya swala ya ijumaa basi aoge) kama alivyosema Mtume.
5.Kupiga mswaki kujipaka manukato(kwa wanaume) na kuvaa nguo nzuri.
6.Inapendezwa vile vile kuelekea msikitini mapema , Sunna hii yakaribia kufa twamuomba Allah amrehemu kila mwenye Kuihuisha.
No comments:
Post a Comment