Thursday, August 22, 2013

SWALA YA IJUMAA

M/Mungu Mtukufu anasema  katika kitabu chake kitukufu :-
(Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye utajo wa Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua.
Na itakapo kwisha Sala, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu,
na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi  ili mpate kufanikiwa) Qur-ani 62:9-10

Na Mtume(S.A.W) Rehema za M/Mungu zimshukie Juu yake na amani  anasema:
(Watu wataachana na tabia yao ya kuacha (kuto hudhuria)  swala ya ijumaa,au Mwenyezi Mungu atapiga muhuri katika nyoyo zao,kisha watakuwa miongoni mwa watu  wenye kujisahau) Kama alivyosema Mtume  Hadithi imepokelewa na Imamu Muslim.

M/Mungu atapiga muhuri katika nyoyo zao, na kuwa ni watu wasio ikubali haki kwa sababu
mioyo yao haipo tayari kuipokea haki kutokana na kupigwa muhuri huo.

Twamuomba Allah atuongoze katika njia iliyo nyooka!
Tuwe ni miongoni mwa watu wenye kuisikia haki na kuifuata!

Ewe Mola zisikie Dua zetu ... Amiin

No comments:

Post a Comment