Wednesday, September 18, 2013

WATENDAJI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAPEWA MAFUNZO YA UZIMAJI MOTO

PIX 1Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Leonard Mponeza akiwaelekeza watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jinsi ya kutumia mitungi ya kuzimia moto. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi. Mafunzo hayo ya Kinga na Tahadhari ya Moto yalitolewa katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi).PIX 2Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wapili kulia) pamoja na watendaji wa wizara hiyo wakiingalia kwa makini chupa yenye dawa ya kuweka kwenye mitungi ya kuzimia moto. Kulia ni askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Leonard Mponeza ambaye alitoa mafunzo ya Kinga na Tahadhari ya Moto kwa maofisa hao katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam . (Picha na Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi).PIX 3Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akizima moto kwa utaalamu baada ya kupata mafunzo ya Kinga na Tahadhari ya Moto yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam . (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.).
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments:

Post a Comment