Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Nyamatenda kata ya Shigala akiwa amesimama na balozi wa Shina namba 1 Sofia Kayenze. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na balozi wa Shina namba 1 Sofia Kayenze wakila chakula cha pamoja cha asili Michembe na Karanga. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi pikipiki kiongozi wa Kikundi cha Bodaboda Gasper Mabula wa kata ya Nyashimo wilaya ya Busega ,Pikipiki mbili zimekabidhiwa ikiwa sehemu ya ahadi ya mbunge wa Busega Dk. Titus Kimani. Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisimikwa kuwa mshauri mkuu(Mnang'oma) na wazee wa wilaya ya Busega katika eneo alilolala Rais Julius Kambarage Nyerere katika matembezi ya kuunga mkono Azimio la Arusha 20.02.1967. Katibu MKuu akishiriki kujenga ofisi ya kata ya CCM Mwamanyili.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikutana na rafiki Deogratius Mtale yake aliyesoma nae shule ya msingi West Meru mwaka 1967 Kinana na rafiki yake huyo wamekutana leo katika kijiji cha Mwanandi kata ya Mwamanyiri,wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
No comments:
Post a Comment