Thursday, September 19, 2013

RAIS KIKWETE ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA, WASHINGTON DC‏

Raus Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mama William alipokuwa akiingia chumba cha mikutano cha Nyerere.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa Mabalozi wa Heshima.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Balozi wa Heshima Hon. Kjell Bergh kutoka Minnesota.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Balozi wa Heshima Hon. Ahmed Issa kutoka California.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Balozi wa Heshima Hon. Robert Samuel Shumake kutoka Michigan.
 Rais Dkt Jakaya Kikwete akitembea kwa miguu kutoka hotelini kwake kuja kwenye Ubalozi wa Tanzania Marekani siku ya Jumatano Sept 18, 2013 na kukutana na Mabaozi wa Heshima ambao jana Jumatano walisaini mikataba ya kuwa rasmi Mabalozi wa heshima wataofanyakazi wakiiitangaza Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya uwekezaji, Utalii na mambo mengine yatakayosaidia kuinua uchumi wa Tanzania.
Rais Dkat Jakaya Kikwete akisalimiana na Maafisa Ubalozi wakiwemo wafanyakazi mara tu alipoingia Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo barabara ya 22, Washington DC.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akitia saini kitabu cha wageni Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni huku Mhe. Bernard Membe na Mhe. Balozi Liberata Mulamula wakishuhudia.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongea machache kuwashukuru Mabalozi wa Heshima kwa kukubali kwao kuitangaza Tanzania nchini Marekani na kusema sio kazi rahisi lakini ana Imani nao na aliwatakia kila la kheri ya kuwa na nia thabiti ya kuitangaza Tanzania nchini Marekani.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Balozi wa Heshima Hon. Robert Samuel Shumake kutoka Michigan.

(Picha kwa hisani ya Vijimambo Blog)

No comments:

Post a Comment