Sunday, September 29, 2013

KONGAMANO LA NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KUDUMISHA AMANI TANZANIA, LAFANYIKA MKOANI KIBAHA

washiriki wakiwasili

Bi Shamim Khan na wageni wengine wakiwasili
mgeni rasmi mh. Ramadhan Madabida (kushoto) akikaribishwa
Sheikh wa mkoa wa Pwani, Mudhihir bin Said
Mshereheshaji wa Kongamano Bi Sakina Mshana katikati
Sheikh Suleiman Kilemile
Sheikh Hamis mtupa kadhi mkuu wa mkoa Pwani
baadhi ya washiriki wa kongamano hilo
Bi Halima Kiemba, Mkuu wa Wilaya ya Pwani
wanafunzi wa Wali Ul Asr

Kongamano la kuishi kwa amani limefanyika wiki iliyopita katika Ukumbi wa B-MERLIN uliopo Shirika la Elimu, mkoani Kibaha. Dhana kuu ya katika kongamano hilo ilikuwa ni, Nafasi ya Mwanamke wa Kiislamu katika kudumisha amani nchini.

Wandaaji wa Kongamano hilo ni Jumuiya ya Kinamama wa Kiislamu wa Tanzania Mkoa wa Pwani, ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Mh. Ramadhani Madabida, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam.  

Kongamano hilo lilifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Mwantumu Mwahiza, kabla ya ufunguzi huo ilisomwa Dua na sheikh mkuu wa mkoa wa Pwani Mudhihir Bin Said. Na kufuatiwa na Qurani tukufu iliyosomwa na Ustadh Mohamed Binde.

Mada zilizowasilishwa ni "Eleweko la amani na kuishi kwa kuvumiliana", "Nafasi ya mwanamke wa kiislamu katika kuleta na kudumisha Amani", na "Mchango wa vyama vya siasa,Vyombo vya Dola na Jamii katika kudumisha Amani"

Wengine waliohudhuria ni Muhammad Alqusuri,Mwenyekiti wa World Islamic Call Society (WICS), Sheikh wa Mkoa wa Pwani, Mudhihir Said, Kadhi mkuu wa Mkoa wa Pwani Sheikh Hamis Mtopa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkoa wa Pwani Bakwata, Sheikh Suleiman Nassor, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanazuoni Tanzania na Mwakilishi wa WICS, Sheikh Suleiman Kilemile, Mbunge wa Kibaha Mjini, Mh. Silvestry Koka na Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani.

Wengine ni Bi Halima Kiemba,Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Bi Shamim Khan Mwenyekiti wa JUWAKITA Taifa, Bi Rahma Mwacha,Makamu Mwenyekiti JUWAKITA mkoa Pwani na Bi Mwasiti Maggid aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Elimu Kibaha. 

Washiriki wengine waliokaribishwa ni kutoka JUWAKITA Taifa, WICS

Wakinamama toka misikiti ya Kibaha Pwani, JUWAKITA wilaya za mkoa wa Pwani, Wanafunzi wa kike wa chuo cha maafisa Tabibu (COTC) Kilichopo Shirika la Elimu Kibaha,Wanafunzi wa kike wa Shule/chuo cha Whipas, Wawakilishi toka madhehebu ya kikiristo ( Mapadre, wachungaji, masister), Wawakilishi toka vyama vya siasa mkoa Pwani, wabunge, madiwani, na madaktari wa Hospitali ya Tumbi. 

Chanzo cha habari kutoka    :-  BOFYA KWA HABARI ZAIDI

No comments:

Post a Comment