Wednesday, September 18, 2013

MTANZANIA AYEDAIWA KUWATUNZA RAIA WA NIGERIA AFIKISHWA MAHAKAMANI

PIX-43MNA MAGRETH KINABO – MAELEZO
OFISI   ya Uhamiaji mkoa wa Dares Salaam imemfikisha mahakamani Mtanzania anayedaiwa kuwatunza raia watano kutoka   Nigeria  wanaoishi nchini bila kibali halali baada ya kuwapiga na kuwazuia kufanya kazi maofisa wa uhamiaji kwenye ofisi za Serikali.
 Hayo yalisemwa leo na  Ofisa wa Uhamiaji wa Mkoa wa Dares Salaam Grace  Hokororo wakati akizungumza na mwandishi wa Idara ya Habari –MAELEZO   ofisini kwake ambapo alisema Mtanzania huyo alifikishwa leo(jana) katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu baada ya kutenda kosa hilo jana majira ya saa 1:00 jioni.
 Alimtaja Mtanzania huyo kuwa ni Christopher Kanyala mwenye umri unaokadiriwa kuwa kati miaka 29 hadi 34 mkazi wa Sinza na anadaiwa kuwa aliwakutumikia Jeshi la Polisi nchini, ambapo kesi yake na raia hao watano wa Nigeria itatajwa kesho katika mahakama hiyo.
Akizungumzia kuhusu suala hilo , Grace aliwataka wananchi   wasipende kuishi na raia ambao ni wageni na hawajaripoti katika ofisi za uhamiaji kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria. Huku akiwataka raia wa kigeni kuripoti katika ofisi hizo mara baada ya kuwasili nchini  ili waweze kufuata  taratibu za kisheria.
Aidha  alisema  operesheni ya kuwakamata wahamiaji haramu inaendelea vizuri.
 Grace alisema kwa upande wa wahamiaji haramu kutoka Malawi walijitokeza kwa hiari mpaka leo mchana idadi yao imefikia 1,863 tangu zoezi hilo lilipoanza.
Aliongeza kuwa opresheni hiyo imehusisha mataifa 31 ambapo alitaja baadhi yake kuwa ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda,Italia, Singapore Ethiopia,Libya Yemeni,Somalia,Komoro, Ujerumani, Afrika Kusini,Uturuki, Nigeria, Cameroon,Liberia na Bokinafaso., Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo(DRC) na India.
 Alisema jumla ya raia hao wa mataifa mengine waliokamatwa ni 502.

No comments:

Post a Comment