Sunday, August 11, 2013

MUENDELEZO MPYA  WA MKASA WA SHEIKH ISSA PONDA

Assalam Alaykum
Ndugu Waislamu na Wote Wapenda Amani

Napenda kuwapa up-date ya Mtihani wa Sheikh wetu, Ponda Issa Ponda

Mchana huu amepelekwa Hospitali moja ya Jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi (maana risasi bado iko mwilini)

Jina la Hospitali litatajwa jioni ya leo Katika Msikiti wa Mtambani, in Shaa Allah

Anaejua jina hilo anaombwa ASILITAJE MPAKA MUDA HUO ili watu wasiiende Hospitali kabla ya kuhudhuria Kongamano la Alaasisiri ya leo (soma chini)

PIA,

Ndugu Waislamu MNAOMBWA LEO SAA 10.00 ALAASIRI MUHUDHURIE KONGAMANO KUBWA litakalofanyika Katika Msikiti wa Mtambani, Kinondoni, Dar es Salaam, mara tu baada ya Swala ya Alaasir (saa 10.15 jioni)

Vile vile mnaombwa kutuma taarifa hii kwa email na kutumia sms ili wengi wahudhurie kwa wingi

Zaidi ya hayo, tuongeze Dua kwa Sheikh Ponda na Familia yake katika kipindi hiki kigumu zaidi

___________________________________________________________

Shura ya Maimamu chini ya Sheikh Kundecha Musa Kundecha imeitaka serikali kuunda tume huru kufanya uchunguzi kuhusu kadhia ya kujeruhiwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Sheikh Ponda


Katika mkutano wake na waandishi wa habari katika Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam, Amiri Kundecha aliyeongozana na wakili wa Sheikh Ponda, Bwana Nassoro Juma, ameitahadharisha serikali kuwa inaelekea kupoteza imani yake kwa wananchi, hususan Waislamu, kutokana na dalili zote kuonesha kuwa polisi ndio waliohusika na tukio hilo.
 

Jeraha alilopata


Tamko  hili pia Limeungwa mkono na Baraza kuu la Waislamu Tanzania Bakwata la kuundwa tume huru ya Uchunguzi wa tukio hili hayo yamesemwa na Sheikh Alhad Mussa Salum Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam kwa Niaba ya Mufti wa Tanzania katika kUPINGA KITENDO KILICHOTOKEA KWANI JESHI LA POLISI LILIKUWA NA UWEZO WA KUMKAMATA NA KUFIKISHA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA,
Sheikh Hamid Massoud Jongo Imamu wa Msikiti Manyema , Siku ya Eid el Fitr Siku ya Ijumaa Tarehe 9 -8- 2013 , katika Uwanja wa Mnazi Mmoja.
                     
 MUENDELEZO WA HABARI YA TUKIO LA SHEIKH PONDA MOROGORO.

Moja ya Habari ambayo inaeleza Jinsi Mkasa wa Sheikh Ponda ulivyotokea  Jana  Jumamosi Augosti 10, mwaka huu majira ya saa 12: 15 za jioni eneo la barabara ya Tumbaku karibu na Fire, mara baada ya kumaliza kwa Kongamano la Kiislamu lililofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege, Kata ya Saba Saba , Manispaa ya Morogoro.
 

Shekhe  Ponda alishiriki katika Kongamano hilo lililoandaliwa na Umoja wa Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu Mkoani Morogoro na kufanyika siku ya Idd Pili kuanza saa nane mchana hadi kumi na mbili jioni ya siku hiyo. 
 

 Kongamano hilo lilipata baraka zote na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, ambalo lilitoa  masharti kadhaa ya kuzingatiwa na wazungumzaji ikiwa ni kutokashifu dini nyingine wala viongozi wa serikali. 
 

Sakata la kutaka kutiwa mbaroni kwa Shekhe Ponda lilikuja baada ya yeye kudaiwa kukiuka masharti ya Mahakama aliyopewa baada ya kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje wa  kutakiwa asitende kosa lolote la jinai anapotumikia adhabu hiyo. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maadalizi ya Kongamano hilo, Ustaadhi Idd Msema, alidai kuwa Shekhe Ponda baada ya kutoka ndani ya gari eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege aliofika mita chache katika barabara ya Tumbaku alitelemka na wakati akitaka kuingia garini ilifyatuliwa risasi iliyompiga begani. 
 

Ustaadh Msema alidai kuwa baada ya kupigwa risasi begani waumini waliokuwa wameambatana naye walimchukua na kumpakiza kwenye Piki Piki hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kupoatiwa matibabu. 
 

 Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, baada ya kufika hospitali, waliona anacheleweshwa kpatiwa matibabu na ndipo walipoamua kumwondoa na kumpekea kwenye Hospitali binafsi ambayo hakupenda kuitaja. 
 

Akizungumzia kwa kina hali ya Shekhe Ponda baada ya kujeruhiwa huko, alisema kuwa yu hai licha ya kuumia vibaya begani na kwamba wanatarajia kumpekela eneo jingine hususani Jijini Dar es Salaam kupata matibabu zaidi.
 

Alisema viongozi wa Umoja huo hauwezi kuweka wazi sehemu anakotibiwa kwa kuwa jambo hilo ni la kiusalama zaidi hasa wakati huu ambapo kumekuwa na sinto fahamu.
 

Baadhi ya walinzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro waliozungumza juu ya tukio hilo , walikiri kuwa Shekhe Ponda aliletwa hapo kwa usafiri wa Piki piki zikiambatana na nyingine zaidi ya 50 na kuishia getini. 
 

Walisema walimwingiza adi mapokezi na kwamba walipoona umati mkubwa upo getini waliamua kutoa taarifa Polisi kuwa wamevamiwa na watu ambapo muda si mrefu Polisi wa FFU waliwasili na gari lao Hospitalini hapo.  
 
Hata hivyo walinzi hao walisema, baada ya kuona Askari wamefika Hospitalini hapo, baadhi ya wafuasi wa Shekhe Ponda waliamua kumnyanyua na kumbeba mabegani na kutoka naye mlango mwingine wakimlazimisha mlinzi kuwafungulia mlango na baadaye wakatokomea naye kwa usafiri wa Pikipiki kusikojulikana. 
Kufikishwa kwa Sheshe Ponda katika Hosipitali ya Rufaa kulithibishiwa pia na Mwenyekiti huyo ambaye alidai  kuwa waliamua kumwondoa baada ya kuchekewa  kupatiwa huduma. 
 
Baada ya tukio hilo, uvumi ulisambaa meneo mbalimbali nchini ukidai kuwa Shekhe Ponda amepigwa risasi na Polisi na kufariki dunia. 


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Feustine Shilogile akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi majira ya saa tatu usiku wa Augosti 10, baada ya kutokea kwa tukio hilo, alisema kuwa hapakuwa na taarifa juu ya kutokea kifo cha Shekhe Ponda. 
 

“ Nimepigiwa simu zaidi ya 50 , zikiulizia jambo hili...kuwa Ponda amefariki dunia ...Binafasi nami ninazisikia , ujumbe umesambazwa kwenye simu za watu mbalimbali...tumezunguka kila mahali hakuna kifo wala maiti yake ...na vijana wangu wanaendelea kulifuatilia suala hili” alisema Kamanda huyo. 

Juhudi za kufuatilia sakata la uvumi kifo cha Shekhe Ponda uliendelea kufanyiwa kazi na Ripota wetu huyu na usiku wa saaa tano Mwenyekiti wa Kamati huyo aliweka wazi kwa kusema kuwa Shekhe Ponda yu hai isipokuwa ameumia vibaya sehemu ya bega . 
 

 “ Nipo katika eneo ambalo Shekhe Ponda anapatiwa matibabu...sehemu ambayo hatuwezi kupataja kiusalama , isipo kuwa ameumia vibaya kwenye bega lake.

 "Lakini yu hai wala hajafa” alisema Msema. 


UKWELI WA YOTE YALIYOTOKEA M/MUNGU NDIYE MJUZI SUBRA KWA WATANZANIA NA WAISLAMU WOTE KWA UJUMLA M/MUNGU AMPONYE SHEIKH PONDA KWA  HARAKA , KKIISLAM BLOG INAPINGA KWA NGUVU ZOTE MATUKIO KAMA HAYA ILI KULINDA AMANI YA NCHI.
PICHA ZA MUHADHARA JANA MOROGORO
Shekh Ponda akizungumza kwenye Kongamano , Augosti 10, mwaka huu mjini Morogoro

akitambulishwa jukwaani Shekh Ponda.


Askari wa FFU wakijisongeza kati kati ya uwanja mara baada ya muda wa kongamano kumalizika.
Shekh Ponda akikaribishwa kwenye jukwaa kuu baada ya kuwasili kwenye viwanja vya shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege , mjini Morogoro
Kikosi cha FFU uwanjani
 Shekh Ponda akisalimiana na Mhadhiri wa Mihadhara nchini, Ustaadhi Abubakari
Shekh Ponda akiteta jambo na baadhi ya Viongozi wa umoja wa Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu Mkoa wa Morogoro
 Shekhe Ponda akiwa meza kuu kwenye kongamano hilo

 Shekhe Ponda akiwa amezingirwa na waumini

Waumini katika Kongamano hilo.

Waumini wa Dini ya Kiislamu wa mjini Morogoro wakimsikiliza Shekh Ponda

Waumini wa Kiislamu wakitawanyika uwanjani baada ya muda wa kongamano kufikia tamati.