DINI NI NASIHA
Kutoka kwa Abu Ruqayyah Tamim Ibn Aus AddarryRadhi za M/Mungu zimshukie Juu yake amesema kuwa Bwana Mtume Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani kasema:
Dini
ni nasiha. Tukauliza: Kwa nani? Akasema kwa Allaah (Kukiri Uungu wake
na kwamba Hana mshirika), Kitabu chake (Kukubali kuwa ni maneno ya Allah
yasiyo na shaka), na Mtume wake (Kumkubali na kukubali ujumbe aliotumwa
nao), na kwa Viongozi wa Waislamu (Kuwatii na kuwafuata katika mema na
kuwaasa katika yale wanayokwenda nayo kinyume), na watu wa kawaida(kuusiana mema na kukatazana mabaya kwa njia nzuri).
Hadithi hii Imesimuliwa na Imamu Muslim
No comments:
Post a Comment