Friday, August 09, 2013

SWALA YA EID ZANZIBAR LEO

Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji ,akiswalisha Swala ya Idd el Fitri,ambayo kitaifa iliwaliwa leo katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja leo katika kufuatia kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Imamu Mkuu wa Msikiti Masjid  Mushawal Mwembeshauri Sheikh Mziwanda Ng’wali Ahmed,akitoa hutuba ya swala ya idd el fitri,katika viwanja vya maisara Suleiman Mjini Ungujaleo katika kusherehekea sikukuu hiyo kwa wailamu wote Duniani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Amani Abeid karume wakati wa Swala ya Idd el Fitri iliyosaliwa Kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman,Mjini Unguja.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa katika swala ya Idd el Fitri,iliyoswaliwaa kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja,kufuatia kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
[Picha na Ramadhan  Othman Ikulu.]

No comments:

Post a Comment