Saturday, August 10, 2013

USHAURI WA BURE WA  KULINDA  USALAMA WETU TANZANIA. 
Mtu kama sheikh Ponda ni lulu na Almasi ambayo inaswaka na wengi wenye kutaka mambo yatibuke Tanzania watu kama hawa wanatakiwa walindwe kuliko hata Wabunge na Wajumbe wa Serikali za Mitaa ili watu waendelee vyema na Maisha yao ya kila siku  hii Ndio Njia Mbadala Maadui wapo wengi sana ambao wanataka Mambo yaende Kombo Tanzania Miongoni mwetu sisi wenyewe Sababu Angalia Uadui na chuki zilizopo katika harakati za  CCM vS CHADEMA , BAKWATA VS NON BAKWATA , WAISLAMU WA SIASA KALI VS WAISLAM POA , WAKRISTO VS WAISLAM hii ukiifikiria utaona umuhimu wa vyombo vya Usalama kuwa Makini zaidi ili Maisha yaendelee kwani wengi katika Viongozi watakuwa wanasakwa.

SOMA NA HII MUHIMU KWA KILA MTU .

KIFO NI WAJIBU WA KILA MUUMINI WA KIUME NA WAKIKE ( BINAADAMU) MTU YEYOTE ANAPOKUFA KUNA WATU MAALUM WA KUTOA TAARIFA ZA KIFO KATIKA FAMILIA MIMI NA WEWE KWELI NI NDUGU WA IMANI ILA RUHSA YA KUTANGAZA KIFO CHA MTU RUHSA HIYO HATUNA , JUU YETU TUSUBIRI NA WAPO WATAKAO PEWA MAJUKUMU YA KUSEMA WATASEMA NA TUTASIKIA KILA JAMBO M/MUNGU AMPONYE SHEIKH PONDA NA WAGONJWA WOTE WA KIISLAM.

TAARIFA YA POLISI KUHUSU KUPIGWA RISASI SHEIKH PONDA

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limekanusha kumpiga risasi Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislam Sheikh Ponda Issa Ponda. Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro ACP Faustine Shilogile amesema polisi walikwenda kumkamata lakini kwa kusaidiwa na wafuasi wake aliwatoroka na hawajui alipo. Jeshi hilo bado linamsaka na halina taarifa kama yupo hai au la . 
__________________________________________
Taarifa za Jeshi la Polisi kuhusu Shekhe Ponda.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wizara ya Mambo ya Ndani.
Jeshi la Polisi Tanzania.
Dar es salaam agosti, 10, 2013

1. Mnamo tarehe 10, Agosti, 2013, majira ya saa 8 mchana, maeneo ya shule ya msingi ya kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro kulifanyika kongamano la Baraza la Eid lililoandaliwa na Umoja wa wahadhiri mkoani Morogoro,
Dakika chache kabla ya kongamano hilo kumalizika alifika Shekhe Ponda issa Ponda alizungumza kwa muda mfupi.

2. Kongamano hilo ambalo lilifungwa majira ya saa 12:05 jioni,
Ambapo watu walianza kutawanyika, baadhi yao wakiwa wamezingira gari dogo alilokuwa amepanda Shekhe Ponda baada ya kutoka katika eneo hilo, askari wa Jeshi la Polisi walilizuia gari hilo kwa mbele kwa nia ya kutaka kumkamata Shekhe Ponda ambaye anatuhumiwa kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi sehemu mbalimbali hapa nchini yenye mlengo wa kusababisha uvunjifu wa amani.

3. Baada ya askari kutaka kumkamata, wafuasi wake walizuia ukamataji huo kwa kuwarushia mawe askari wa Jeshi la Polisi, kufuatia na purukushani hizo askari walipiga risasi hewani kama onyo la kuwatawanya.

4. Katika vurugu hizo, wafuasi hao walifanikiwa kumtorosha mtuhumiwa, hivi sasa imethibitishwa kuwa Shekhe Ponda yupo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili akitibiwa majeraha katika bega la mkono wa kulia linalodaiwa alilipata katika purukushani hizo.

5. Kufuatia na tukio hilo timu inayoshirikisha wajumbe toka jukwaa la haki jinai ikiongozwa na CP Issaya Mngulu imeanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

SSP Advera Senso

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania.

TETESI : SHEIKH PONDA APIGWA RISASI MOROGORO LEO

Habari zilizo enea katika Mitandao ya Kijamii Facebook kwa Muda huu zinaeleza  kuwa Sheikh Ponda Issa Ponda kapigwa risasi mkoani morogoro leo. 

Inasemekana sheikh Ponda alipigwa risasi baada ya kushuka kwenye tax kwa ajili ya kuhutubia mhadhara katika eneo la kiwanja cha ndege.

 Vyanzo cha habari vinasema risasi hizo zimempiga bega la kushoto. (Inna lillah wa inna illayhi rajioun).

Tunaendelea kufatilia Taarifa hizi tuwaeleza zaidi ukweli wake Jee ni sahihi yaliyotokea ....

MUENDELEZO WA HABARI.
 
VYANZO VINGI VYA HABARI TULIVYO WASILIANA NAVYO VINASEMA KUWA NI KWELI AMEPIGWA RISASI BEGANI ILA POLISI MKOA WA MOROGORO WAMEKANUSHA AMA HABARI WANAZOSEMA BAADHI KUWA AMEFARIKI SI ZA KWELI  INSHA ALLAH tunazidi fatilia ... 

AZHAR SHAREEF KILA PEMBE YA DUNIA

 Mwalimu Mkuu wa Markazi Islamiyah - Changombe akiongea na Waumini wa Kiislam katika Swala ya Eid , Mnazi Mmoja Dar es salaam  , Jana.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam akisalimina na Baadhi ya Waumini baada ya kumaliza Swala ya Eid.

Azhar Shareef ni Miongoni mwa Vyuo vikubwa duniani ambavyo vina historia ndefu sana katika Malezi ya Elimu ya Dini.

Azhar Shareef Makao Makuu yake yapo  Cairo , Misri na Miongoni mwa harakati zake ni kupeleka Walimu/Wahadhiri katika Nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya.
Ofisi za Makao makuu ya Azhar.


Tawi la Azhar Shareef kwa nchini Tanzania lipo Changombe ( Barabara ya Uwanja wa Taifa) vile vile yapo Matawi madogo katika  Mikoa ya Arusha na Iringa.

Tawi hili la Azhar Nchini Tanzania hutoa nafasi za Masomo ya Juu kwa baadhi ya Wanafunzi ( kuwapeleka Nchini Misri) ili kujiendeleza zaidi .

Mpaka leo wametoa Vijana wengi sana Na Masheikh wengi Tanzania Miongoni Mwao ni Marehemu Sheikh Suleiman Gorogosi
, Sheikh Muhidin Hassan , Sheikh Yahya Mkali n.k 

Kuna Changamoto kubwa sana Vijana wanaomaliza chuo Nchini Misri wanaporudi nyumbani kujiunga Moja kwa moja katika kazi za Daahwa kwa kukosa viunganishi kutokana na Maisha ya nyumbani na Maisha ya elimu wanayo pitia .

Kupitia KKIISLAM BLOG mengi tutawaletea yanayo husu Wana AZHAR nchini Tanzania na Misri kwa ajili ya kufikia Malengo ya Maendeleo Insha Allah. 

Yakiwemo Historia ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Azhar Shareef , Historia ya Umoja wa Wanafunzi wasomao Nchini Misri na Changamoto wanazo kutana nazo, Umoja wa Waliosoma Azhar Nchini Tanzania na Changamoto wanazo kumbana nazo, yote haya InshaAllah yatawajia karibu.
Tuwe pamoja.

FUNGA YA SITA BAADA YA RAMADHAN

Funga ya Sita ni Sunna inayopatikana katika Mwezi huu wa Shawaal baada ya Kumaliza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani  Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani anasema "Atakeyefunga Mwezi wa Ramadhani kisha akafuatilia (kufunga) siku sita katika mwezi wa Shawaal (anakuwa) kama aliyefunga maisha yake yote,”

Na hii ni kwa sababu mtu anapofunga mwezi mmoja wa Ramadhani, anapata thawabu ya kufunga miezi kumi, kwa sababu mtu anapotenda Jema moja hulipwa kumi badala yake. Na anapofunga siku sita katika Shawwal, anakuwa mfano wa aliyefunga siku sitini. Ukijumlisha funga ya Ramadhani na funga ya sita, unapata miezi kumi na miwili, na kwa ajili hiyo anakuwa mfano wa aliyefunga mwaka mzima. Na mtu anapoendelea hivyo maisha yake yote anakuwa mfano wa anayefunga maisha yake yote”.
 
NAMNA YA KUFUNGA.

Imam Annawawi ambae ni katika Maulamaa wakubwa wa madhehebu ya Imam Shafi anasema;

"Ni vizuri kufunga siku sita mfululizo mara tu baada ya kumalizika sikukuu ya mwanzo, na atakayefunga siku sita mbali mbali katika mwezi wa Shawaal , pia inakubaliwa”.

Amma Imam Ahmed bin Hanbal anasema;
“Ukifunga mfululizo au ukizifunga siku sita tofauti katika mwezi wa Shawaal yote ni sawa tu.”

UZINDUZI.

Maulamaa wanasema kuwa;
‘Lazima mtu atimize Ramadhani yake kwanza, ndiyo aweze kufunga sita. Yaani ikiwa mtu anadaiwa katika Ramadhani, basi lazima alipe kwanza deni lake lote kisha ndio afunge sita.’

Na hii ni tafsiri ya kauli ya Mtume  (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani aliposema;
ATAKAYEFUNGA Mwezi wa Ramadhani KISHA akafuatilia (kufunga) siku sita…”

Wakasema kuwa kutokana na kauli hii, Mtume  (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani hapa anasisitiza kuwa mtu lazima kwanza afunge Mwezi wa Ramadhani, KISHA afunge sita. Na ikiwa mtu ana deni la kufunga, basi huyo anakuwa hakufunga mwezi wa Ramadhani, na kwa ajili hiyo ikiwa anazitaka thawabu zilizotajwa katika hadithi hiyo, basi inampasa kulipa deni lake kwanza, kisha ndiyo afunge sita.
 
M/Mungu ndiye Mjuzi .