Friday, September 20, 2013

MIMI SI MSANII NA SIHITAJI MALUMBANO - MUFTI WA TANZANIA SHEIKH SIMBA



MUFTI wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Issa Shaban bin Simba amesema yeye si msanii kama anavyoshutumiwa na Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Mazungumzo kati ya Waislamu na Serikali, Sheikh Suleiman Kilemile.

Mufti Simba alisema shutuma anazotupiwa zinatokana na malalamiko yake kwa Serikali kuhusu kupuuzia suala la Mahakama ya Kadhi.

Kutokana na hali hiyo, Mufti Simba alisema yeye yupo sahihi na kwamba anayemshutumu atumie sheria badala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari.

Simba alisema anachofahamu ni kwamba kupatikana kwa Kadhi hakuhitaji ushirikishwaji wa taasisi zote za Kiislamu na kubainisha kuwa kama kuna kosa lililofanyika sheria ndiyo itatengua kitendawili hicho na si malalamiko.

“Huyo Sheikh Kilemile kama anadhani kulalamika ni dawa waulizwe Waislamu kuhusu Mahakama ya Kadhi na mimi sitaki kuendeleza mvutano kwenye vyombo vya habari,” aling’aka Mufti Simba.

Mufti Ni Msanii - Sheikh Kilemile


MWENYEKITI wa Kamati Ndogo ya Mazungumzo kati ya Waislamu na Serikali, Sheikh Suleiman Kilemile amedai kuwa Mufti Issa Shaban bin Simba ni msanii katika kupata Mahakama ya Kadhi.
Sheikh Kilemile alisema hatua ya kumuona Mufti Simba msanii imekuja baada ya kujitokeza akiilaumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kupuuza maoni ya Waislamu ya kutaka kuanzishwa kwa mahakama hiyo.

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari na kuongeza kuwa lawama zilizotolewa na Muft Simba ambaye ni mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), zinashangaza.

“Magazeti kadhaa ya hapa nchini Agosti 31, 2013, yamemkariri Mufti Simba  akilalamika kuwa Waislamu wanapuuzwa kuhusu madai yao ya kutaka Mahakama ya Kadhi hapa nchini.

“Muft Simba ameilaumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kupuuza maoni ya Waislamu ya kutaka kuanzishwa Mahakama ya Kadhi inayotambulika kikatiba hapa nchini,” alisema Sheikh Kilemile.

Alisema lawama zilizotolewa na Muft Simba zinashangaza kwa sababu zaidi ya miaka mitatu iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alimuagiza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda awasiliane na Bakwata ili kumtaka Simba aunde jopo la masheikh kutoka taasisi mbalimbali za Kiislamu ili liwe chombo cha kuwakilisha Waislamu wote nchini.

“Basi jopo likaundwa kama alivyoagiza waziri mkuu, na hadidu za rejea zikatengenezwa. Kiongozi wa jopo hilo alikuwa Muft Simba.

“Jopo hilo lilikubaliana kwa sauti moja kuwa masuala yote yanayohusu ufuatiliaji wa Mahakama ya Kadhi hapa nchini yatasimamiwa na jopo hilo tu na si vyenginevyo,” alisema.

Alifafanua kuwa baada ya kufanyika kwa vikao vingi chini ya uenyekiti wa Muft na vingine na Pinda mchakato huo ulionesha kufikia hatua nzuri.
Alisema kikao cha mwisho cha jopo hilo chini ya waziri mkuu kilihudhuriwa na baadhi ya watendaji wa Serikali na mawaziri kadhaa wakiwemo Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.   
“Kwa vile mahakama za kadhi zinapatikana pia katika nchi nyingine za kisekyula kama Uingereza, India, Kenya na hata Zanzibar, Wassira alimshauri waziri mkuu upatikane ujumbe utakaokwenda kutembelea nchi hizo na utakaokusanya wajumbe kutoka serikalini na jopo la masheikh kujionea taratibu za uendeshaji wa mahakama za kadhi katika nchi hizo ili utakaporudi nchini uweze kuelekeza jinsi ya kuziendesha mahakama hizo hapa nchini.
“Pinda alikubali na kuibariki rai hiyo. Aliamuru upande wa jopo la masheikh utoe wajumbe watatu na upande wa Serikali wajumbe wawili. Ilikubaliwa  kuwa gharama za kupeleka ujumbe huo Uingereza, India, Kenya na Zanzibar zilipwe na Ofisi ya Waziri Mkuu.

“Ujumbe huo ulitakiwa uwe umekamilisha ziara hizo kabla ya Aprili mwaka huu wa 2013,” alisema.

Sheikh Kilemile alidai kabla ya kufanikisha hayo, Muft Simba alipuuza yale maazimio ya kikao hicho na badala yake aliamua kuitisha mkutano wa viongozi wa Bakwata mjini Dodoma na kutangaza jina la kadhi wake mkuu pamoja na wasaidizi wake bila kushauriana na jopo la masheikh lililoteuliwa kushughulikia mchakato mzima wa kupatikana Mahakama ya Kadhi.   

“Mtaona alilolifanya Muft Simba ni usanii. Ni kwa sababu hao makadhi aliowateua hawapo kisheria na wala hawana mamlaka yoyote ya kiutendaji,  kisha Sheikh Simba anathubutu kuinyoshea kidole Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Serikali, eti kwa kuwapuuza Waislamu kuhusu Mahakama ya Kadhi,” alisema.

CHANZO CHA HABARI MUNIRAMADRASA BLOG

WAZIRI MKUU MHE. PINDA AZUNGUMZ NA WANANCHI WA ENDULENI- NGORONGORO

IMG_0002IMG_0037Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Karatu baada ya kuwasili kwenye Lodge ya Bashay Rift  akiwa njiani kuelekea Enduleni wilayani Ngorngoro, Septemba 19, 2013.IMG_0059Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kushoto) wakipokea salamu maalum kutoka kwa wasichana  wa Kibarabaig baada ya kuwasili katika kijiji cha Enduleni wilayani Ngorongoro Septemba 9, 2013.IMG_0093Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya cha Enduleni wilayani  Ngorongoro Septemba 19, 2013.
IMG_0109Baadhi ya Wazee wa Kimasai wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alizungumza nao kwenye Kituo cha Afya cha Enduleni wialyani Ngorongoro Septemba 19, 2013. 
IMG_0164Mwananchi wa Kijiji cha Enduleni  wilayani  Ngorongoro  akinyosha mkono kuomba kumuuliza swali Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  ambaye alihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hichoSeptemba 19, 2013.  
 (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE BUSEGA


Kikundi cha Ngoma cha Mwanalyaku Dance Group kikionyesha uwezo wake wa kucheza ngoma ya bugobogobo ikiwa sehemu ya utangulizi kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara wa CCM uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mkuu wa Wilaya ya Busega Ndugu Paul Mzindakaya katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kisesa, Lamadi na kumuambia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana maji bado ni tatizo kwa wakazi wa wilaya yake.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lamadi wilayani Busega kwenye Mkutano wa hadhara na kuwaambia wananchi wawe makini na makanjanja wa kisiasa ambao kwa sasa wamefunga ndoa batili kutaka kuvuruga mchakato wa kupata Katiba mpya.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lamadi kwenye Viwanja vya Kisesa wilaya ya Busega mkoa wa Simiyu na kuwaambia wananchi kuwa muda wa walimu kuendelea kupata tabu umeisha na kuagiza mamlaka husika kutatua kero na madai ya walimu ndani ya miezi sita na kama wameshndwa wajiuzulu kupisha watu wengine.

KUTOKA ZANZIBAR

Waandishi wa pata Semina ya Kuripoti Sheria za Utambuzi wa Ardhi Zanzibar.


 Mratibu wa Mafunzo ya kuripoti Utambuzi wa Sheria za Ardhi Zanzibar Ali Rashid, akitpowa  mada kuhusu matumizi ya Ardhi na jinsi ya kufanyiwa Utambuzi kwa mmiliki halali wa ardhi, mafunzo hayo yaliwashirikisha waandishi wa habari mbalimbali Zanzibar, wakati kukiwa na zoezi la Utambuzi wa Ardhi na Usajili linalofanyika katika Wilaya  za Unguja.

 Mtoa Mada AliRashid akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo kwa  waandishi wa habari yaliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Kikwajuni Zanzibar.
 Afisa Mtambuzi wa Ardhi Zanzibar Shawana Soud Khamis, akitowa mada ya kisheria jinsi ya Utambuzi wa Usajili wa Ardhi unavyofanyika na kumpata mmiliki halali, zoezi hilo linafanyika katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, likiazia katika Wilaya za Kati na Mjini kusajili Ardhi na kupata Wamiliki wa ardhi halali na kupata hati miliki ya Ardhi anayomiliki na kutambuliwa Kisheria.
 Waandishi wakifuatilia mafunzo hayo ya kuripoti habari za Usajili wa Ardhi Zanzibar, linalofanyika katika wilaya mbalimbali za Unguja.

British mission eases visa conditions for Tanzanians

BY CORRESPONDENT DAVID


 
The British High Commission to Tanzania has announced a new priority ‘fast-track’ visa service as an option to ease visa access for Tanzanians.

Speaking to members of the press at the official launch of the Priority Visa Service at the British High Commission yesterday in Dar es Salaam, the High Commissioner Dianna Melrose said that the Commission has introduced the service as one of its initiatives to strengthen diplomatic relationships between the two countries.

The Commissioner explained that her country would like to see a two way traffic between the United Kingdom and Tanzania. To do that they have introduced the fast track service, this will ease the obtaining of a visa to the UK for a maximum of five working days.

She noted that the available visas falls under the categories of business visas, student visas and visit visas in which an applicant is required to pay an additional fee of 250,000/- for his/her application to be processed ahead of others.



“The service has been launched as a response to our clients’ demand, it will help us achieve the objectives of our new UK/Tanzania prosperity partnership to increase trade and investment, support Tanzania’s development and generate prosperity and employment for both Tanzania and UK,” she said.

However, she made it clear that with this service, the normal immigration rules still apply. 
SOURCE: THE GUARDIAN

Serikali ya Uingereza kupitia Ubalozi wake nchini, imetangaza huduma mpya ya haraka ya utoaji viza inayoitwa ‘huduma ya upendeleo ya utoaji visa kwa haraka’  ili kuwawezesha Watanzania  kupata viza hizo ndani ya siku tano.

Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose, alisema huduma hiyo inalenga kuwasaidia waombaji wa visa kwa ajili ya shughuli za kibiashara, masomo kwa wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini humo na zile za kusafiria, ili wapate haraka tofauti na nyuma kwani ilikuwa inatumia muda mrefu.

Balozi Melrose alisema huduma hiyo pia imelenga kukuza ushirikiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na pia kusaidia kukuza biashara, uwekezaji na maendeleo ya Tanzania na hivyo kuongeza ustawi na ajira kati ya pande hizo mbili.

Aliongeza kuwa huduma hiyo pia itawasaidia waombaji kusafiri kwa haraka pale wanapokuwa na shughuli zao za dharura.

Kwa mujibu wa Melrose, kuanzia sasa kupitia huduma hiyo, waombaji wanapaswa kulipia Paundi za Uingereza 100 (sawa na Sh. 250,000) ambazo zinaweza kulipwa kwa njia ya mtandao kwa kujaza fomu na pia kutembelea ofisi za Ubalozi huo kitengo cha viza.
 
CHANZO: NIPASHE

Rais Kikwete akutana na uongozi wa CCM DMV Washington DC Marekani

 Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete Mwenyekiti CCM Taifa akielekeza jambo katika kikao chake na uongozi wa CCM DMV. Kikao hiki kimefanyika leo Sept 19,2013 jijini Washington DC, Marekani. Picha na Swahilitv

Mhe. Rais Kikwete akiwa na Bwana DMK Mkurugenzi wa MMK MEDIA GROUP: Swahili TV, Swahili Radio na Swahilitv Blog. Picha zote na Swahili TV.

Mama Mwanamwema Shein, Ahimiza Jamii Kuwekeza katika Madrasa.

Na Mwantanga Ame

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein, ameitaka jamii kuona umuhimu wa kuwekeza katika shughuli za madrasa ili kuweza kupata kizazi kilichobora.

Mama Shein, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na walimu na wanafunzi wa Madrasa Hidayatu ya Kidoti Nungwi, Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja, baada ya kukabidhi vifaa mbali mbali kwa ajili ya matayarisho ya ufunguzi wa Madrasa hiyo, iliyojengwa kwa mchango wa ahadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.

Akitoa nasaha zake kwa niaba ya Mama Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais, Mama Asha Suleiman Iddi, alisema ni vyema jamii ikaona umuhimu huo kwa vile utaweza kujenga kizazi kilicho bora kutokana na maeneo hayo huchangia imani njema ya dini ya kiislamu.

Alisema nyingi ya Madrasa hivi sasa zimekuwa zikionekana kama vile si maeneo ya msingi yanayohitaji kuwekezwa katika hali ya ubora, jambo ambalo jamii inapaswa kuona inabadili tabia hiyo.

Alisema maeneo ya madrasa hivi sasa yanahitaji kuonekana kuwa bora, ili yaweze kwenda sambamba na mafunzo yaliomo katika dini ya kiislamu, ambayo kwa kiasi kikubwa yanasaidia kuandaa kizazi kilicho bora.

Alisema sehemu kubwa ya jamii ya kiislamu inasahau umuhimu wa kuwekeza katika madrasa na kuwa tayari kusaidia maeneo mengine ambayo hayana msaada katika kujenga jamii iliyo na umani za kidini.

Alisema mfano halisi hivi sasa baadhi ya watu wamekuwa wakitoka nje ya misingi ya kidini kuitana majina ambayo yanapingana na uislamu, jambo ambalo kama wangelikuwa na elimu ya kutosha wangeliepuka.

Kutokana na hali hiyo, Mama Shein, alisema ni lazima jamii kuanza kuziona kasoro hizo na kuachana na mambo yalio nje ya misingi ya kiislamu.

Mama Asha, aliwakabidhi madrasa hiyo, vifaa mbali mbali, vikiwemo sare kwa wanafunzi na walimu wa madrasa hiyo, misahafu 210, Vijuzuu 200, pamoja na meza, kabati na viti ambapo vyote vinathamani ya shilingi milioni 12.

Baadhi ya viongozi wa Mkoa huo akiwemo Mkuu wa Wilaya Riziki Juma Simai, alipongeza hatua ya Mama Shein, kuona madrasa hiyo inakamilika kwa wakati, kwani itachangia utoaji wa elimu bora kwa watoto wa kijiji hicho.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, anatarajiwa kuifungua madrasa hiyo kesho, ambayo ina wanafunzi wapatao 358.

KUTOKA ZANZIBAR

Wawaa Madrasatul Hidaaya Islamia Kidoti Nungwi.



Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akizungumza na Walimu na Wanafunzi wa Madrasa ya Hidaya Islamia Kitodi, alipofika kwa ajili ya kumuakilishi Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, kukabidhi vifaa vya na sare na Misahafu Juzuu kwa ajili ya Wanafunzi wa Madrasa hiyo.

Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akimkabidhi Sare za Wanafunzi na Walimu wa Madrasa kwa ajili ya matumizi ya madrasa hiyo vilivyotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein.
Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif Ali, akimkabidhi misahafu Mwalimu wa Madrasa hiyo Makame Juma.


Wanafunzi wa Madrasa Hidaya Islamia Kidoti wakiwa katika viwanja vya Madrasa yao Kidoti wakati wa sherehe za kukabidhiwa vifaa vyao na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, kwa Niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein.


Wanafunzi wa Madrasa Hidaya Islamia Kidoti wakiwa katika sherehe za kukabidhiwa Vifaa kwa ajili ya madrasa yao mpya, wakiwa katika viwanja vya madrasa yao Kidoti Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
 Walimu wa Madrasa Hidaya Islamia Kidoti wakiwa na sare za wanafunzi wao baada ya kukabidhiwa na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, kwa ajili ya Wanafunzi wao ikiwa sare ya Madrasa yao.
 Jengo jipya la Madrasa Hidaya Islamia Kidoti lililojengwa na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, kwa ajili ya watoton wa madrasa hiyo kupata Elimu ya Dini katika mazingira mazuri, jengo hilo linatarajiwa kufunguliwa kesho Ijumaa.


Jengo la Madrasa Hidaya Islamia Kidoti lililojengwa na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, kwa ajili ya Watoto wa Kijiji hicho kupata elimu ya Dini baada ya jengo lao la zamani, kwa kushirikianana Mama Asha Balozi Seif na Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM Zanzibar. kusaidia jamii katika maendeleo ya Elimu kwa Watoto. 

Kinana Haipasha Wizara Ya Elimu Na Mafunzo Ya Ufundi

Abdurahman Kinana ameipapa miezi sita Wizara Ya Elimu Na Mafunzo Ya Ufundi kutatua kero za walimu, vinginevyo CCM itachukua hatua kali dhidi ya watendaji wa wizara hiyo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana awasili katika kijiji cha Nyashimo Wilayani Busega katika mkoa wa Simiyu,  Ndugu Abdulrahman Kinana amemaliza ziara yake kwenye mkoa huo ambapo amekagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wenyeviti wa mashina pamoja na wanachama wa CCM ili  kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi katika maeneo mbalimbali moani humo, Kinana anaaza Ziara ya siku sita katika mkoa wa Mara. Akihutubia katika mkutano wa hadhara leo uliofanyika mjini Lamadi Busega  Kinana ametoa miezi sita kwa Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Serikali za Mitaa TAMISEMI Hawa Ghasiapamoja na watendaji wengine wa Serikali katika sekta ya Elimu kuhakikisha wanashughulikia kero za walimu hasa katika malipo yao mbalimbali ili kumaliza tatizo  la malimbikizo hayo, Kinana amesema kama watendaji hao wa serikali hawatamaliza tatizo hilo atawashughulikia kwa kuwashitaki kwa wabunge wa CCM ili wawawajibishe kwa kukiuka agizo la Rais Dr.Jakaya Kikwete ambaye aliagiza watendaji hao kumaliza matatizo ya walimu, Katika picha katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Besega Ndugu Paul Mzindakaya na aliyenyanyua mkono kushoto ni Mbunge wa jimbo la Busega Dr. Titus Kamani.
1
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye wakifurahia ngoma za akina mama walipowasili katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
9
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pikipiki kwa mwenyekiti wa kikundi cha waendesha bodaboda wa Nyashimo Gasper Mabula
7
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana  akimnawisha mikono Mwenyekiti wa shina Sina namba 1 kijiji cha cha Nyamatembe Bi.  Sophia Kayenze tayari kwa kupata kifungua kinywa cha  chai kwa Michembe .
5
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana  akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Busega Ndugu Paul Mzindakaya katika kijiji cha Nyamatembe.
4
Nape Nnauye katibu wa NEC  Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza na wananyamitembe mara baada ya kuwasili kijijini hapo wakitokea Bariadi.
10
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana  akisimikwa kama mshauri mkuu wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Kikwete katika kijiji cha Mwamanyiri mahari ambapo Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. nyerere alipumzika na kulala akitokea Butiama kwenda Mwanza wakati akiunga mkono Azimio la Arusha mwaka 1967.
14
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana   akishiriki kujenga ofisi ya Chama cha Mapinduzi kata ya Mwamanyiri huku Nape Nnauye akimsaidia kumpati tofari. 
15
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana  akipanda mti katika kata ya kabita wilayani Besega.
17
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana  akikabidhi pikipiki kwa mwenyekiti wa kikundi cha waendesha Lamadi Busega bodaboda  Doto Paulo .
21
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Ndugu Pascal Mabiti kulia akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Besega Paul Mzindakaya kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Lamadi Busega.
20
Kikundi cha ngoma cha lamadi Busega kikitumbuiza katika mkutano huo.
23
Wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wa hadhara  wakifuatilia matukio ya mkutano huo.
24
Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akuhutubia wananchi katika mkutano huo wa hadhara mjini Lamadi wilayani Busega.
25
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Lamadi Simiyu.


 (PICHA NA KUKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-LAMADI SIMIYU)

RAIS DKT. KIKWETE AONGEA NA MABALOZI WA HESHIMA (HONORARY CONSULS) WASHINGTON D C

0L7C0488Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi wa heshima watakaoiwakilisha Tanzania katika majimbo mbalimbali nchini Marekani wakati wa hafla ya kuwapa hati za utambulisho zilizofanyika katika ubalozi wa Tanzania jijini Washington Marekani  (picha na Freddy Maro)

PRESIDENT DR. KIKWETE MEETS CONGRESS MEMBERS AT CAPITOL HILL

0L7C0117President Jakaya Mrisho Kikwete with his delegation  during a working meeting with Congress woman Kay Granger(second left), Chairwoman of the State, Foreign operations and related Programs Sub-Committee House appropriations at Capitol Hill, Washington DC this morning. On the right is the Minister for Foreign Affairs and International Cooperation Bernard Membe, Fourth Right is the Minister for  Natural Resources and Tourism Ambassador Khamis Kagasheki and third right is Tanzania’s ambassador to the US Liberata Mulamula(photo by Freddy Maro).