FIQH

متن سفينة النجا
 
للعلاّمة المعلم القاضي الفقيه الشيخ
سالم بن عبدالله بن سعيد بن سُمَير الحضرمي الشافعي
المتوفى سنة 1271هـ
Mtunzi wa Kitabu ameanza na utangulizi wa kumshukuru M/Mungu na kumtakia Rehma Mtume Muhammad Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani.

Baada ya Utangulizi huo akaanza na somo la kwa kwanza kwa kueleza 

NGUZO ZA UISLAM.

Nguzo za Uislam ni tano.
  1. Kukiri kwa Moyo na kutamka kwa ulimi kuwa hapana Mola apasae kuabudia isipokuwa M/Mungu mmoja ( Allah) na Muhammad Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani ni Mtume wake.
  2. Kudumisha Swala.
  3. Kutoa Zakkah.
  4. Kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 
  5. Kwenda kuhiji kwa mwenye uwezo. 
 -----------------------------------------------------------------------------------------------------  
   NGUZO ZA IMANI
Nguzo za Imani Sita
  1. Kumuamini M/Mungu 
  2. Kuamini Malaika wake.
  3. Kuamini vitabu vyake.
  4. Kuamini Mitume yake.
  5. Kuamini Siku ya Mwisho.
  6. Kuamini Uwezo wake M/Mungu (Kheri na Shari ni zake ).
--------------------------------------------------------------------------------------------------------
وَمَعْنَى لاَ إِلَهَ إَلاَّ اللهُ
Maana ya Laaillaha ila Allah 
Maana yake ni kwamba hakuna apasae kuabudiwa kwa kweli katika Ulimwengu isipokuwa Allah pekee (M/Mungu).
--------------------------------------------------------------------------------------------------------

TWAHARA ( USAFI) .

Alama za Kubaleghe ni Tatu .
  1. Kutimiza Umri wa Miaka 15 kwa Mwanaume na Mwanamke .
  2. Kuota kwa Mwanaume na Mwanamke anapotimiza Miaka 9.
  3. Kutokwa na Damu ya hedhi kwa Mwanamke anapotimiza miaka 9.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------
Sharti za kupasa kutumia Mawe ni Nane.
  1. Kuwepo na Mawe Matatu.
  2. Yasafishe sehemu iliyotoka Najisi Mawe hayo.
  3. Najisi isiwe imekauka
  4. Najisi isiwe Imehama (kugula).
  5. Isijitokeze Najisi nyengine.
  6. Isiwe Imetapakaa katika tupu zake hiyo Najisi.
  7. Isiwe imepataa Maji hiyo Najisi .
  8. Na Mawe yanayo tumika katika kuondosha Najisi hiyo yawe Twahara(Safi). 
-------------------------------------------------------------------------------------------------------- 
FARADHI (NGUZO) ZA UDHU 
Faradhi za Udhu ni Sita 
  1. Nia 
  2. Kukosha Uso
  3. Kukosha mikono Mikono pamoja na Mirfaq mbili.
  4.  Kukosha sehemu katika Kichwa.
  5. Kukosha Miguu miwili pamoja na vifundo viwili.
  6. Mpangilio.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------- 
NIA 
 Maana ya Nia ni kukusudia kitu chenye kuambatana na kitendo .
Sehemu ya Nia : Moyoni .
Kuitamka Nia : Sunna
Wakati wake hiyo Nia : Wakati wa Mwanzo wa kukosha sehemu katika Uso.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------
MPANGILIO
Maana ya Mpangilio ni kutotanguliza kiungo wakati wa Kuchukua Udhu isipokuwa kuenda na Mpangilio ambao tume ueleza Juu katika Faradhi za Udhu,
 --------------------------------------------------------------------------------------------------------
MAJI ( katika Twahara).
Maji yako ya aina Mbili Machache na Mengi  .
Maji machache ni yale ambayo yako chini ya Qulateen.
Maji mengi ni yale ambayo yamefikia Qulateen na zaidi.

Maji machache yana Najisika (hayafai kuji twaharishia) kwa kuingia  Najisi ndani ya Maji hayo  hata kama hayajabadilika.

Maji Mengi haya Najisiki ( kutofaa kutumia kwa Twahara) isipokuwa yatakapo badilika Radhaa yake , Rangi yake au harufu yake .
--------------------------------------------------------------------------------------------------------
YENYE KUMUWAJIBISHA MTU KUKOGA
Mambo yenye kumuwajibisha Mtu kukoga yapo Sita .
  1. Kuingiza tupu katika tupu ( Kuingilia).
  2. Kutokwa na Manii.
  3. Hedhi
  4. Nifasi
  5. Kuzaa
  6. Kufa   --------------------------------------------------------------------------------------------------------
FARADHI ZA KUKOGA 
Faradhi za kukoga Mbili 
  1. Nia 
  2. Kueneza Mwili wote Maji.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------
SHARTI ZA UDHU 
Sharti za Udhu ni Kumi (10)
  1. Uislamu
  2. Upambanuzi
  3. Kusafika na Hedhi na Nifasi
  4. Kutokuwa  na kitu katika Mwili chenye kuzuia kufika Maji katika Ngozi
  5. Kusiwe katika kiungo kitu ambacho kitabadilisha rangi ya Maji  
  6. Kuwa na Utambuzi wa Nguzo za huo Udhu.
  7. Kuto itakidi Nguzo katika Nguzo za Udhu kuwa ni Sunna
  8. Maji Masafi ( yaliyo Twahara )
  9. Kuingia wakati.
  10. Kufululiza(katika kuosha Viungo) kwa Mtu Mwenye Hadathi ya kuendelea.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------- 
VITENGUZI VYA UDHU
Mambo Manne yenye kutengua Udhu
  1.  Chenye kutoka katika Moja ya Njia Mbili ya Mbele au Nyuma Upepo au kitu kingine isipokuwa Manii ( hayatengui Udhu ).
  2. Kuondokwa na Akili kwa kulala au kwa aina nyengine yeyote isipokuwa hautenguki Udhu wa Mtu Mwenye kulala ambaye Makalio yake ameya makinisha katika Aridhi.
  3. Kugusana Ngozi mbili ya Mtu Mwanaume na Mwanamke wa kando (Ambaye ni halali kumuoa) pasina kizuizi.
  4. Kugusa tupu(mbele) ya Binaadamu au ya Nyuma kwa Matumbo  ya viganja  au ya Mkono .
--------------------------------------------------------------------------------------------------------
MAMBO AMBAYO HAYAFAI KUFANYA KWA MTU ASIYE KUWA NA UDHU.
Mtu asiye kuwa na Udhu ( Uliye tenguka Udhu wake) ni haramu kwake (haruhusiwi) kufanya mambo ma nne.
  1. Kuswali.
  2. Kutufu Al Kaaba. ( katika Ibada ya Hija).
  3. Kuugusa Msahaafu ( Qur an Tukufu)
  4. Kuubeba huo Msaahafu.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------
MAMBO AMBAYO NI HARAMU KWA MTU MWENYE JANABA.
Ni haramu kufanya Mtu Mwenye Janaba Mambo Sita .
  1. Kuswali.
  2. Kutufu Al Kaaba
  3. Kuugusa Msahaafu 
  4. Kuubeba
  5. Kukaa Msikitini 
  6. Kusoma Qur an Tukufu
INAENDELEA INSHAALLAH ....     

No comments: