MAKALA

DUA YA KUWATENDEA WEMA WAZAZI WAWILI
YA
AL-‘ARIF BILLAH SHAYKH MUHAMMAD BIN AHMAD BIN ABI-L-HIBB, HADHRAMI WA TARIM
    (Mwenyezi Mungu amrehemu)
Alhabib Alwi Bin ShihaabHusomwa baada ya kuhitimishwa Qur’ani, hasa hasa katika mwezi wa Ramadhani. Al-Habib Alwy bin Abdallah bin Shihab (radhi za Mwenyezi Mungu zimwalie) ambaye ni mmojawapo wa ma-Shekhe wa Mwinyi Baraka (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) alikuwa akiitaja dua hii katika majalis yake kama mwenye kuwahimiza watu wawe wakiitumia.
بِسْمِ اللهِ الْرَحْمَنِ الْرَحِيْم
Himdi zote zile zinamhakia Mwenyezi Mungu pekee ambaye ametuamrisha kushukuru wazazi wawili na kuwafanyia hisani na aliyetuhimiza kuwania kuwafanyia wema wao wawili na kuwatengenezea yalo mazuri kwao na aliyetutia shime tuwainikie bawa la rehema kwa kuwatukuza na kuwaheshimu, na akatuusia kuwarehemu wao wawili kama vile walivyo turehemu sisi zama walipotulea nasi tu wadogo bado.
Allahumma basi warehemu wazazi wetu wawili (x3), na waghufirie wao, na waridhiye wao radhi ambazo zitawashushia wao Ridhwani Zako na kuwashusha wao kwenye nyumba ya Takrima Yako, na Amani Yako, na makazi ya Afua Yako, na Maghfira Yako, na wamiminie wao, teule za Wema na Ihasani Yako.
Allahumma waghufirie wao maghfira yenye kukusanya, utafuta kwa hayo maovu yao yaliyopita na ubaya wa kukamia kwao yale yasio sio na warehemu wao, rehema kuu itayowanawirishia malazi kwenye makaburi yao na kuwatuia katika amani siku ya fadhaa zama za kufufuliwa kwao.
Allahumma kuwa mwenye kite juu ya udhaifu wao kama wao, juu ya udhaifu wetu walivyokuwa ni wenye kite, na rehemu kimbilio lao asiye na pakushika wanapokimbilia Kwako, (Warehemu katika hali hiyo) kama vile wao walivyoturehemu sisi tulipokimbilia kwao kimbilio la asiye na pakushika, na waonyeshe kite kama vile wao walivyotuonyesha kite katika hali ya utoto wetu.
Allahumma wahifadhie wao yale mapenzi ya kina ambayo ulinywesha nyoyo zao na kite na imani uliojaza vifua vyao na upole ambao kwa huo walishughulisha viungo vyao, nawashukuru wao kwa ile bidii na sulubu ambayo ikishamiri kwetu kutuwania na wala usiwaondoshee patupu ile jitihada ambayo kwayo wakijitahidi juu yetu, na walipe mema kwa zile mbio walizokuwa wakienda kwa niaba yetu na machungo ambayo walikuwa wakituchunga (wajazi) yale yaliyo mema kabisa uliowajazi wenda mbio wasuluhishi na wachungaji walio halisi wa dhati.
Allahumma watendee wao wema kwa wingi wa wingi, kuliko wema wakitutendea sisi, na waangalie wao kwa jicho la rehema kama vile ambavyo walituangalia sisi.
Allahumma wasamehe wao yale waliyoyatupa katika haki ya Uola Wako wakati wameshughulika na haki ya ulezi wetu, na wasamehe wao pale waliposhindwa na kughafilika na haki huduma Kwako, kwa sababu walitanguliza haki huduma kwetu. Na wape afua kwa yale yenye walakini walioyapanda kwa sababu ya kuchuma kwa ajili yetu, wala usiwapatilize kwa yale walioyatenda kutokana na povu la hawa nafsi kwa sababu ya mapenzi yetu kughilibu nyoyo zao, na watue zile dhuluma walizozibeba wakati wanatuendea mbio sisi, na wafanyie upole kwenye makazi ya kuoza kwao, upole adhimu dhidi ya upole wao kwetu wakati wa uhai wao nasi.
Allahumma na zile twaa ulizotuongoza kuzitenda na yale mema uliyoyafanya mepesi kwetu na yale ya mkuruba uliotuwafikisha, tunakuomba ewe Allahumma, uwajalie wao humo sehemu na fungu. Na yale maovu tuliyoyachuma na makosa tuliyoyafanya na maelemevu tuliyoyabeba, basi usiwakutishe wao kutokana na hayo mabaya yeyote yale, wala usiwatwishe wao dhambi zezote zile kutokana na dhambi zetu.
Allahumma kama vile ulivyowafurahisha nasi wakati wa uhai basi wafurashishe nasi baada ya roho kufariki miili.
Allahumma wale usiwafikishie wao zile habari zetu sisi zitakazowafanya wasikie vibaya, wala usiwatwishe wao kutokana na mabaya yetu yatowashinda kubeba, wala usiwafedhehi wao kwa ajili yetu kwenye mkusanyiko wa waliokufa, kwa sababu ya zile fedheha tunazozitenda na mabaya tunayoyafanya, na zifurahishe nyoyo zao kwa amali zetu kwenye mkutano wa roho pale watu wema watapofurahi kwa wana wema, wala usiwasimamishe wao kwa sababu yetu msimamo wa fedheha, kwa sababu ya yale mabaya tunayoyachuma kwa viungo vyetu.
Ewe Allahumma na kisomo chechote kile cha Qur’ani tulichokisoma, Ukakitakasa na Kukistawisha kikachanua, na sala yeyote ile tuliyoisali Ukaikubali, na sadaka yeyote ile tuliyoitoa, Ukaikuza ikakuzika, na amali yeyote ile katika amali njema tuliyoitenda Ukairidhia, basi tunakuomba ewe Allahumma ujalie fungu lao humo kubwa kuliko mafungu yetu na qisma yao tonono zaidi kuliko qisma zetu, na sehemu yao ya thawabu imebariki zaidi kuliko sehemu zetu, kwani hakika Wewe (Ewe Allahumma) Umetuusia kuwatendea wema na Umetutia shime kuwashukuru hali ya kuwa Wewe ni bora zaidi kutenda wema kuliko wale wenye kutenda wema, na Mwenye haki zaidi ya kuunga kwa hisani kuliko wale walioamuriwa.
Ewe Allahumma tujalie sisi tuwe upeo wa furaha yao Kiyama kitakapo simama, na wasikilizishe wao wito mzuri kabisa kutoka kwetu siku ya malinganio, na wajalie wao kwa sababu yetu sisi kati ya wazazi waliofurahishwa upeo wa furaha na wana wao mpaka Utakapo tujumuisha sisi na wao na waisilamu wote kwenye nyumba ya takrima Yako, na matulio ya rehema Yako, na mahali pa Mawalii Wako, pamoja na wale Ulio waneemesha (kwa neema Zako) miongoni mwa Manabii na wenye Kusadiki, kusadiki kwa upeo na mashahidi na watenda zema, wazuri walioje waja hao kuwa nao, “hiyo ni fadhila kuu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na itoshe kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kujua”.
Ametakata na kila lisilo laiki nae Rabbu wako, Rabbu mwenye enzi na nguvu, Ametakata na yale (yasiyo laiki) ambao Humsifia. Na salamu ziwaendee Mitume mursali na himdi zote zile zinamhakia Mwenyezi Mungu pekee, Rabbi wa viumbe pia na Mwenyezi Mungu amswaliye Bwana wetu Muhammad, Nabii Ummii na juu ya ‘Aali zake na Sahabaze na Amsalimie taslima adhimu, tena nyingi.
  
                                                     KWA MAKALA ZAIDI BOFYA HAPA


ADABU ZINAZOTAKIWA KUFUATWA KATIKA SIKU YA EID.

1.Muislamu anatakiwa katika siku za Eid akoge (Josho kubwa) , ajitie manukato (mwanamume) na avae nguo nzuri za kupendeza.

Ni sunna kula kwanza kabla ya kwenda kuswali swala ya Eidil-Fitri kinyume na Eid -Adh-haa unatakiwa ule ukitoka kuswali kama alivyo tuelekeza Mtume.

2.Kuleta Takbira kwa wingi tangu usiku wa Eid zote mbili.

MUDA WA TAKBIRA KWA EID - EL FITRI zinaanza Usiku wa Eid na kuendelea Mpaka baada ya swala tu,  ama zile za Eid l Adh-haa  hudumu mpaka siku ya mwisho ya kuanikwa Nyama (Alasiri ya mwezi 13 - Mfunguo tatu).

MATAMSHI YA TAKBIRA ZA EID.
   
ALLAAHU AKBAR ALLAAHU AKBAR ALLAAHU AKBAR . LAA ILAAHA ILLAL-LAAH WALLAAHU AKBAR . ALLAAHU AKBAR WALILLAAHIL-HAMDU. ALLAAHU AKBAR KABIYRAA . WAL-HAMDU LILLAHI KATHIYRAA. WASUB-HAANALLAAHI BUKRATAN WA ASWIYLAA. LAA ILAAHA ILLAL-LAAHU WAHDAU. SWADAQA WA’ADAU. WANASWARA ‘ ABDAU . WA A’AZZA JUNDAU WAHAZAMAL - AHZAABU WAHDAU. LAA ILAAHA ILLAL-LAAHU. WALAA NA-'BUDU ILLAA IYYAAU MUKHLISWIYNA LAHUD - DIYN WALAU KARIHAL- KAAFIRUUN.

ALLAAHUMMA SWALLI ALAA SAYYIDNAA MUHAMMAD WA ALAA AALI SAYYIDNAA MUHAMMAD . WA ALAA ASW-HAA BI SAYYIDNAA MUHAMMAD WA ALAA ANSWAARI SAYYIDNAA MUHAMMAD WA ALAA DHURRIYATI SAYYDINAA MUHAMMAD . WASALLIM TASLIYMAN KATHIRYRAA.
    
3.Ni suna kwenda msikitini kwa njia moja na kurudi kwa njia nyingine isiyokuwa ile uliyo tumia wakati wa kwenda.
    
4.Vilevile ni sunna waislamu kupeana mikono siku ya Eid , na kuombeana Dua kwa Kusema  ( TAQABBALALAAHU MINNAA WA MINKA ) (Mwenyezi Mungu atutakabalie Ibada zetu Sisi na wewe). Hii Ni Dua Itikia Amiin.

Hivi ndivyo ilivyopokelewa  Maswahaba wa Mtume walikuwa wanapokutana siku ya Eid huambiana (huombeana)  " Taqabbalal-laahu Minnaa waminkum " Na si kama Mazoea yetu ikiwa kama Mazoea yatakuja baada ya kuombeana Dua kwa Namna tuliyo elekeza hakuna tatizo  Mazoea yetu  " MKONO WA EID  UKINIONA KIMNYA UJUE SINA ".

 5.Eid ni siku ya Furaha hivyo basi furahi na wafurahishe familia yako kwa Vyakula , Vinywaji ( Vinywaji vya halali) pasina kufanya fujo (Israafu) na hapa ni muhimu tuwakumbuke Ndugu zetu wasio na uwezo kwa sadaka ili nao wapate furahi siku hii tukufu.

Siku ya Eid ni Siku ya Kula na Kunywa ( Vinywaji vya halali) , Kumshukuru M/Mungu , kutembelea Ndugu , Jamaa na Marafiki na Mengi ya kheri yaliyo katika ratiba zako.

TAMBUA Siku hii hairuhusiwi kufunga kwa Mtu yeyote .

Baada ya kusherehea Siku ya Eid inayo fata Ni Sunna iliyokokotezwa na Mtume nayo ni Sunna ya Funga ya Sita .

Ni Bora kufunga Siku ya Pili au Mwezi Pili Shawali lakini inaruhusiwa kufunga Muda wowote  Funga hii ya Sita isipokuwa Isitoke tu ndani ya Mwezi wa Shawali

Imepokewa hadithi na Abu Ayoub (Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake )  kwamba Mtume Muhammad (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie juu yake na amani amesema, " Atakayeufunga mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani, na kisha  akaufuatishia Mwezi huo wa Mtukufu wa Ramadhani na  siku sita za Mwezi wa Shawali(Mfungo mosi) itakuwa kama kufunga mwaka mzima" kama alivyosema Mtume hadithi imepokelewa na Imamu Muslim.



UBORA WA ELIMU.

Uislamu unahimiza Elimu kutokana Umuhimu wake na Ubora wake Ukirejea katika uteremshwaji wa Wahyi kwa Mtume Muhammad (S.A.W)Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani unakuja kukuta kwamba Aya za Mwanzo 5 Kumteremkia Mtume zilikuwa zinazungumzia Elimu (Kusoma).

M/Mungu anasema " Soma kwa Jina la Mola wako ambaye ameumbaa ...". Qur an.
Elimu ndio pambo zuri , lenye Thamani kuliko Mapambo yote anayojipamba nayo Mwanadamu. 

Elimu ndio mwangaza na taa pekee inayomuangazia mwanadamu katika Maisha ya ulimwengu huu.

Elimu ndio chombo pekee anachoweza kukitumia mwanadamu katika kumtii Mola wake, kwani kutokana na elimu ndipo mwanadamu huweza kujua halali na haramu na akapambanua baina ya lenye kunufaisha na lenye kudhuru.

Elimu ndio njia pekee ambayo inaweza ikakutoa au kulitoa Taifa katika Kiza cha Utororo na kuwa katika Mwanga wa Maendeleo na Utukufu wa Elimu ndio Mataifa Mengi yamesonga mbele.
Isipokuwa tutambue kwamba Elimu pekee bila ya Vitendo haina faida wala Msaada kwa Msomaji SUBHANA ALLAH .

Ili Elimu iwe Elimu chukua Muongozo wa Wanachuoni huu (Elimu bila ya matendo ni kama mti usiotoa matunda).

UKIREJEA AYA TULIYO ANZA NAYO " Soma kwa Jina la Mola wako ambaye ameumbaa ...". 
Tuzisafishe Nyoyo zetu ki Nia  katika  Usomaji wetu uwe kwa Ajili ya M/Mungu na wala si kutaka kujulikana kwamba wewe ni Msomi .

Pili chukua Muongozo huu Mwenye kutaka kupata elimu ya nyingi , pamoja na kufanya juhudi ya kusoma basi ajilazimishe sana kumcha Mwenyezi Mungu katika Dhahiri na Siri  SUBHANA ALLAH , M/MUNGU : "NA MCHENI MWENYEZI MUNGU NA MWENYEZI MUNGU ATAKUELIMISHENI; NA MWENYEZI MUNGU NI MJUZI WA KILA KITU" Qur an Sura 2 Aya 282.

Katika kuonyesha ubora na utukufu wa elimu Mwenyezi Mungu anatuambia: "SEMA, JE WANAWEZA KUWA SAWA WALE WANAOJUA NA WALE WASIOJUA?.." Qur an Sura ya 39 Aya 09.
Jibu la hawawezi kuwa sawa wenye kujua na wasio Jua ....
SOMA HADITHI YA BWANA MTUME MUHAMMAD ( S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani " Kutafuta elimu ni faradhi  ya lazima kwa kila muislamu (Neno Muislamu linakusanya Mwanamume na Mwanamke)". kama alivyosema Mtume.

FAIDA ZA KUSOMA.
Ziko faida nyingi sana ambazo anazipata Mtu mwenye kusoma miongoni Mwazo tumekwisha tangulia zitaja.

ila kubwa katika nyengine faida za kusoma ni kukupa wewe Msomi Muongozo wa kuweza kutekeleza vyema kazi ya kulingania kama M/MUNGU ANAVYOSEMA "WAITE(watu) KATIKA NJIA YA MOLA WAKO KWA HIKIMA NA MAWAIDHA MEMA NA UJADILIANE NAO KWA NAMNA ILIYO BORA… "Qur an Sura ya 16 Aya 125.

Vilevile M/Mungu anasema  "MWENYEZI MUNGU ATAWAINUA WALE WALIOAMINI MIONGONI MWENU; NA WALIOPEWA ELIMU WATAPATA DARAJA ZAIDI" Qur an Sura ya  58 Aya 11. Hii nayo ni moja katika faida za Msomi.

Nimalize kwa kusema kwamba ELIMU NI BAHARI (PANA) INAKUSANYA FANI NYINGI SANA JUU YETU KUSOMA ELIMU AMBAZO ZITAKUWA NA MSAADA KWETU KWANZA WA KUJUA DINI YETU KISHA ELIMU ZA KUWEZA ENDESHA MAISHA YETU.

WABILLAHI TAUFIQH . Na Sheikh Amir Ibrahimu Maine