PICHA NA MATUKIO


Ust Mohd Khamis wa Msikiti wa Qiblaten akiwa katika harakati za Daahwa
Waumini wakiwa katika Ibada ya Swala katika Msikiti wa Qiblateen - Kariakoo
Msikiti wa Qiblateen

Sheikh Kwangaya akiongea katika Moja ya Hafla za kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Ustaadhi Kwangaya Akipokea zawadi
Sheikh Kwangaya akiwa na Baadhi ya Vijana wa Kiislam katika Picha ya Pamoja akiwemo Ust Ahmad Mchen

----------------------------------------------------------------

Mwili wa Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo Wawasili Zanzibar.

Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo, aliyefarika Nchini Congo, akiwa katika Jeshi la Kulinda Amani.
 Ndege iliobeba Mwili wa Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar ikitokea Dar-es-Salaam.
 Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakijumuika na Ndugu na Jamaa kuupokea mwili wa marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo.ulipowasili Zanzibar kwa mazishi Kijijin kwao Fujoni kwa mazishi jioni hii.
 Ofisa wa JWTZ akitowa maelezo ya ratiba ya kuupokea Mwili wa Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo katika uwanja wa ndege wa Zanzibar leo mchana na kuzikwa katika Kijiji cha Fujoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
 Mjane wa Marehemu na Watoto wake wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume leo mchana wakitokea Mjini Dar-es- Salaam.
 WANAJESHI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa na mwili wa Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo, baada ya kuuteremsha katika ndege maalum ya Jeshi.
 Wanajeshi wa JWTZ wakitembelea kwa mwendo wa pole wakiwa na Mwili wa Marehemu Hatibu Shaban Mshindo, baada ya kuwasili Zanzibar, tayari kwa mazishi yanayofanyika jioni hii katika Kijiji cha Fujoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja.

 Wananchi wakiwa katika viwanja vya ndege vya Zanzibar wakiupokea mwili wa marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo, aliyefariki Nchini Congo akiwa katika Jeshi la Kimataifa la kulinda Amani Nchi Congo.
 Msafara wa Magari ya JWTZ ukiondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kuelekea katika Msikiti wa Bezredi Muembeladu kwa kuusalia na maziko yatakayofanyika katika Kijiji chao Fujoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja, saa kumi jioni.
KUMBUKUMBU 2012

RAIS KIKWETE KATIKA SWALA YA IDD LEO MSIKITI WA KINONDONI MUSLIM MASJID EL FARUOQ

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda wakati alipowasili katika msikiti wa Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Swala ya Idd leo Agosti 19, 2012.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa  wakati alipowasili katika msikiti wa Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Swala ya Idd leo Agosti 19, 2012.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa miongoni wa waumini kusikiliza mawaidha kutoka kwa Sheikh Abubakar Zubeir katika  msikiti wa Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam baada ya  ya Swala ya Idd leo Agosti 19, 2012.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na waumini  katika  msikiti wa Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam baada ya Swala ya Idd leo Agosti 19, 2012.
 
Mama Salma Rashid Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono wa Iddi na kinamama waliohudhuria Swala ya Iddi leo Agosti 19, 2012  katika msikiti wa Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA IKULU).


KUMBUKUMBU YA SWALA ZA EID ZILIZOPITA HII NI August 31, 2011

MAKAMU WA RAIS KATIKA SWALA YA EID EL FITR MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum, wajumuika pamoja na waumini wa dini ya kiislamu kuswali swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum, wakiwa katika swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Immam Mkuu wa Msikiti wa Manyema jijini Dar es Salaam, Masoud Mohamed Jongo, akitoa mawaidha baada ya swala ya Eid El-Fitr iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo, Agosti 31, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, baada ya kumalizika kwa Swala ya Eid El- Fitr, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba, baada ya kumalizika kwa Swala ya Eid El-Fitr leo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
 

Rais Kikwete shiriki swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani,Magomeni Mapipa jijini Dar es salaam leo

Kumbukumbu ya Swala ya Eid , August 31, 2011
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu waumini waliohudhuria swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa mkono wa Iddi baadhi ya waumini waliohudhuria swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo asubuhi
(picha na Freddy Maro).

KUMBUKUMBU RAIS KIKWETE AFUTURISHA MKOANI LINDI …

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya Magharibi na waumini wengine wa Mkoa wa Lindi aliowakaribisha katika futari Ikulu ndogo ya Mkoani Lindi leo Julai 30, 2012
Mkuu wa Mkoa a Lindi Mhe Ludovick Mwananzila akishiriki katika futari hiyo pamoja na waalikwa wengine
Kadhi wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Shekhe Mkuu wa Mkoa Mohamed Saidi Mushangani akitoa neno la shukurani baada ya futari
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na waalikwa walioshiriki katika futari hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wageni waalikwa baada ya kufuturu.

Rais Kikwete ashiriki Swala ya IDDI kijijini Msoga

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya Iddi katika Masjid Rajab kijijini kwake Msoga-Chalinze.
 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono wa Iddi na baadhi ya waumini walishiriki swala ya Iddi katika Masjid Rajab Kijijini kwake Msoga, kata ya Chalinze,Wilayani Bagamoyo
(picha na Freddy Maro)


RAIS DK SHEIN ASHIRIKI SALA YA EID EL HAJJ

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein,pamoja na Viongozi wengine
wakijumuika na waislamu na wananchi katika  swala ya EID el Hajj
katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
 

Baadhi ya Waislamu na wananchi wakisikiliza Hotuba,baada
ya Swala ya Eid el Hajj iliyotolewa na Sheikh Soraga,katika Msikiti wa
Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na waumini ya Dini ya
Kiislamu baada ya kuswali swala ya  EID el Hajj katika Msikiti wa
Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]


 

1 comment:

  1. Anonymous3:22 PM

    dogo umekuwa habari Maelezo Nini?

    ReplyDelete