LIKE OUR PAGE ON FACEBOOK
Monday, June 30, 2014
Saturday, May 24, 2014
YAH MUALIKO WA MAULID YA MTUME MUHAMMAD REHMA ZA MWENYEZI MUNGU ZIMSHUKIE JUU YAKE NA AMANI
Bismillahi Rahmani Rahim
Ungozi wa Madrasatul
Amini ya Marhum Sheikh Nassor Amran Iliopo kwa Ali Maua A Chini ya
Uongozi na Usimamizi wa Mudiru Alhaj Sheikh Mohammad Nassor Unapenda
Kukualika na Kuwakaribisha Wadau wote na Wapenzi Wa Mtume Muhammmad
Rehma za Mwenyezi Mungu zimshukie Juu yake Shughuli hii Itafanyika hapa
MADRASANI KWETU KWA RATIBA IFUATAYO SIKU YA IJUMAA TAREHE 30 / 5 / 2014
Kuanzia Saa 4 Asubuhi Maonyesho ya Wanafunzi na Baada ya Swala ya
ISHAAI MAULIDI YA JUMUIA
MASHEIKH NA WAALIKWA KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI
WATAHUDHURIA NAWE TUNA KUKARIBISHA KUUNGANA NASI KATIKA JAMBO HILI.
Watendaji wa Kuu na Waratibu wa Shughuli hii MAPACHA NA WAPENZI WA MTUME MUHAMMAD REHMA ZA MWENYEZI MUNGU ZIMSHUKIE JUU YAKE NA AMANI KATIKA Moja ya hafla kama inayo tarajia fanyika Siku ya Ijumaa. |
Kwa Mdau yeyote Ambae atahitaji kuchangia Baadhi ya Vifaa kama Maji , Juice N.k Unakaribishwa Ujachelewa.
Wednesday, December 25, 2013
RAIS KIKWETE AKUTANA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani jana tarehe 24/12/2013.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akimwonyesha sehemu ya kukaa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya kufanya mazungumzo naye.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon alipomtembelea ofisi kwake jijini New York, Marekani jana 24/12/2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mwenyeji wake,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon mara baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini New York, Marekani 24/12/2013.
Rais Kikwete yupo jijini New York nchini Marekani ambapo anaendelea vyema na ukaguzi wa kawaida wa afya yake.
(Picha na Freddy Maro / Ikulu)
Wednesday, December 18, 2013
Mama Kikwete aitaka jamii kusaidia kuinua elimu ya wanawake
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu
wa CEO Clubs Network, Bwana Tareq Ahmed Nizami, mwandaaji mwenza wa
Mkutano wa Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia, 'The
Africa -Middle East-Asia' unaofanyika katika Hoteli ya Atlantis The
Palm, huko Dubai katika Jamhuri ya Falme za Kiarabu (UAE), tarehe
16.12.2013. Mwandaaji mwingine wa mkutano huo ni Kituo cha Maendeleo ya
Kiuchumi na Uongozi (CELD).
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Penehupifo Pohamba, Mke wa
Rais wa Namibia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa wanawake
kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unaofanyika Dubai kuanzia
tarehe 16.12.2013.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Balozi wa Tanzania katika nchi
za Falme ya Kiarabu (UAE) wakati wa sherehe za ufunguzi wa Mkutano wa
wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unaofanyika katika
hoteli ya Atlantis The Palm iliyopo Dubai, Jamhuri ya Falme za Kiarabu
tarehe 16.12.2013. Kushoto kwa Mama Salma ni Mke wa Rais wa Namibia Mama
Penehupifo Pohamba, na wa kwanza ni Mshauri Maalum wa Mama Pohamba
Mchungaji Justina Hilukiluah na wa mwanzo kushoto no Bwana Tariq Nizami,
Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa CEO Clubs Network.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiwasilisha mada ya Elimu: Key to the Future
of Women in Emerging Economies, kwenye mkutano wa siku tatu wa Wanawake
kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unaofanyika huko Dubai tarehe
16.12.2013.
Mke wa
Rais wa Namibia Mama Penehupifo Pohamba akimpongeza Mke wa Rais, Mama
Salma Kikwete baada ya kutoa mada iliyosisimua wajumbe wa Mkutano wa
Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unafanyika jijini
Dubai, Jamhuri ya Falme aza Kiarabu tarehe 16.12.2013.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na Mheshimiwa Margaret
Zziwa, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki. Viongozi hao ni miongoni mwa
viongozi wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia wanaohudhuria
mkutano wa siku tatu huko Dubai.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Dr. Angela Moore, Balozi
wa Heshima kutoka Jimbo la Georgia, nchini Marekani wakati wa mkutano
wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia huko Dubai tarehe
16.12.2013. PICHA NA JOHN LUKUWI
Na Anna Nkinda – Maelezo, Dubai
Serikali
, Asasi za kiraia, Sekta binafsi na watu mbalimbali wametakiwa kusaidia
kuinua elimu ya wanawake kwakuwa faida yake ni pana na endelevu na kwa
kufanya hivyo watakuwa wameotesha mbegu ambayo matunda yake
yatanufaisha ulimwengu kwa kuufanya uwe na ustawi zaidi, amani na
utengamano.
Wito
huo umetolewa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea
kwenye mkutano wa siku tatu wa wanawake kutoka nchi za Afrika, Asia na
Mashariki ya Kati unaofanyika katika Hoteli ya Atlantis The Palm
iliyopo Dubai , Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Mama
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) alisema elimu pekee ndiyo mkombozi wa mwanamke kwa kuwa husaidia
kuboresha afya, uchumi, usalama na hupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya
watoto. Husaidia watoto kuwa na lishe bora na kuboresha afya ya uzazi
na kupunguza kusambaa kwa maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi.
“Umuhimu
wa elimu kwa wasichana na wanawake unafahamika kwetu sote kwa sababu
elimu ni mlango kwa ajili ya fursa na inafaida zaidi katika familia,
jamii, nchi na bara zima kwani wanawake walio na elimu ya msingi
wanafursa kubwa ya kuepuka umaskini, kuwapatia watoto elimu na kuongeza
kipato chao kwa asilimia 10 hadi 20.
Mtoto
aliyezaliwa na mama aliye na elimu ana nafasi zaidi ya kuishi
ukilinganisha na aliyezaliwa na mama asiye na elimu, watoto walio na
mama mwenye elimu ya msingi walau kwa miaka mitano wananafasi ya
asilimia 40 ya kuishi zaidi ya miaka mitano salama pia mwanamke
aliyeelimika anauwezekano zaidi kwa asilimia 50 ya watoto wake kupata
chanjo dhidi ya maradhi ya utotoni”, alisema Mama Kikwete.
Kwa
upande wa Tanzania Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema idadi ya watu ni
asilimia 44.9 kati ya hao wanawake ni asilimia 51.3 Serikali imepiga
hatua kubwa za maendeleo za kuwaendeleza wanawake na tayari imeridhia na
kusaini maazimio ya kitaifa na kimataifa yanayukusudia kuendeleza haki
za wanawake.
Alisema
Serikali imeanzisha sera, mikakati, sheria na kanuni madhubuti
zinazoboresha mazingira wezeshi kwa ajili ya usawa wa kijinsia na
kuwekeza rasilimali na nguvu kubwa kuimarisha haki za wanawake,
kuboresha majukumu na fursa katika siasa, kijamii na kiuchumi.
Mama
Kikwete alisema, “Pamoja na mafanikio makubwa tuliyoyapata katika kutoa
elimu ya msingi kwa watu wote, kufuta ujinga na kupunguza tofauti za
kijinsia bado idadi ya wasichana katika vyuo vya elimu ya juu ni ndogo
ukilinganisha na wavulana hii inasababishwa na utoro mashuleni ambao
unatokana na tatizo la ujauzito, ndoa za utotoni na mila hatarishi”.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Maendeleo ya kiuchumi na
Uongozi (CELD) chenye makao yake makuu nchini Nigeria ambao ndiyo
waandaaji wa mkutano huo Mama Furo Giami alisema huu si muda wa kujadili
mambo ya usawa wa kijinsia bali ni wakati wa kuchukua hatua ili kuona
kwamba usawa wa kijinsia unatekelezeka katika jamii.
Alisema
takwimu zinaonyesha ifikapo mwaka 2028 asilimia 75 ya wanawake
watajihusisha katika biashara Dunia nzima ingawa hivi sasa wanawake
wanamiliki robo ya biashara na nusu ya biashara hizo ni katika
kuendeleza masoko na kukua kwa kazi za kiuchumi wanazozifanya.
“Ingawa
takwimu hizi zinaonyesha uchumi wa mwanamke utakuwa umekuwa lakini
hakuna usawa wa kijinsia kwa mfano idadi ya wanawake ambao ni
wakurugenzi watendaji katika makampuni 500 ni chache kwa mwaka 2012
ilikuwa ni asilimia 4, katika viwanda vya uchumi asilimia 11.1 na
katika masoko idadi ilishuka hadi kufikia asilimia 7.2”, alisema Mama
Giami.
Mkurugenzi
huyo Mtendaji alisema wanawake wanatakiwa kupewa nafasi ya uongozi ili
waweze kupata maendeleo ya kiuchumi kwa kuwawezesha kiuchumi siyo tu
kuwapatia haki zao katika sekta za afya na elimu.
Mama
Giami alisema, “Viongozi wa nchi zetu wanatakiwa kuwapa wanawake
teknolojia, mitaji, kuunga mkono miradi ya kijamii na kudhibiti biashara
haramu ya usafirishaji wa binadamu kwa kufanya hivyo maendeleo
yatapatikana . Pia wahakikishe wanawake siyo kwamba wanapata nafasi
pekee ya uongozi bali wanapata nafasi ya kuchangia katika uchumi wao.
Mada
kuu katika mkutano huo ni Uongozi ni Elimu: Ufunguo wa mustakabali wa
wanawake katika nchi zenye uchumi unaoibuka ambapo washirikiki kutoka
nchi za Afrika, Asia na Mashariki ya Kati walipata nafasi za kujadili
mafanikio na changamoto za kuwaendeleza wasichana na wanawake kielimu.
Wednesday, December 11, 2013
RAIS KIKWETE KATIKA KUMBUKUMBU YA HAYATI NELSON MANDELA
Rais Jakaya Kikwete (wa nne kutoka kulia mstari wa pili) akiwa na mkewe mama Salma Kikwete katika ibada ya Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani, Mheshimiwa Nelson R Mandela.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Desemba 10, 2013, ameungana na viongozi wa mataifa mbali mbali duniani na maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani, Mheshimiwa Nelson R Mandela.
Maelfu kwa maelfu ya wananchi wamehimili mvua kubwa iliyokuwa inanyesha kwa nguvu kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg kumwaga Mzee Mandela ambaye alikuwa ishara kuu ya upinzani wa siasa za ubaguzi wa rangi za makaburu wa Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Mandela ambaye alifariki duniani Ijumaa iliyopita, Desemba 5, 2013, alikuwa Kamanda wa Jeshi la Ukombozi la Chama cha African National Congress la Umkhoto we Sizwe akafungwa jela kwa uhaini kwa miaka 27 na utawala wa Makaburu.
Baada ya kutoka jela mwaka Februari 1990, Mzee Mandela alichaguliwa kuwa Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini ya mwaka 1994. Lakini Mheshimiwa Mandela alitumikia kipindi kimoja tu cha miaka mitano na kukataa kutumikia kipindi cha pili.
Kiasi cha viongozi 91 kutoka sehemu duniani wamehudhuria Kumbukumbu hiyo iliyokuwa na kila aina ya mchanganyiko wa hisia – wengine wakiwa na majonzi na wengine wakicheza na kuimba kwa muda wote wa shughuli hiyo iliyochukua kiasi cha jumla ya saa tano.
Mbali na Rais Kikwete ambaye amefuatana na Mama Salma Kikwete, marais wengine mashuhuri duniani waliohudhuria Kumbukumbu hiyo ni Mheshimiwa Barack Obama wa Marekani, Mheshimiwa Francois Hollande wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon.
Kumbukumbu hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa zamani wa Marekani wakiwemo marais watatu wa zamani wa Marekani – Mheshimiwa Jimmy Carter, Mheshimiwa Bill Clinton na Mheshimiwa George W Bush na mawaziri wakuu wawili wa zamani wa Uingereza, Mheshimiwa Tony Blair na Mheshimiwa Gordon Brown.
Rais Kikwete kesho, Jumatano, Desemba 11, 2013, ataungana na viongozi wenzake katia katika kutoa heshima za mwisho na kuuaga rasmi mwili wa Marehemu Mandela ambao utawekwa kwenye Majengo ya Urais wa Afrika Kusini ya Union Buildings mjini Pretoria.
(Kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Pretoria, Afrika Kusini)
Monday, December 09, 2013
RAIS JK AWASILI UWANJA WA UHURU KUONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA TANGANYIKA
Rais Jakaya Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Uhuru kwa maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika hivi punde.
Subscribe to:
Posts (Atom)