Fainali Za Mashindano Ya Kuhifadhi Qur’an Afrika Mashariki Na Kati.
Mshiriki kutoka Tanzania, Ibrahim Ramadhan, akishiriki fainali za
mashindano hayo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo.
Mshiriki wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an, ambaye alishika nafasi ya
pili katika mashindano hayo, Kombo Bahi Makame kutoka Unguja-Tanzania,
akishiriki mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam leo, ambapo mgeni rasmi katika fainali hizo
zilizowashirikisha washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na
kati, alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal.
Mshiriki wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an, ambaye alishika nafasi ya
kwanza katika mashindano hayo,Jahuddin Adam, kutoka Sudan.
Mshiriki wa mashindano ya kuhifadhi
Qur’an, ambaye alishika nafasi ya tatu katika mashindano hayo,Mohammad
Sad Tawfiq, kutoka Egypt akishiriki mashindano hayo yaliyofanyika katika
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo wakifuatilia kwa
makini fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur’an.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akisoma Hotuba yake wakati wa fainali za mashindano ya
kuhifadhi Qur’an, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini
Dar es Salaam leo na kushirikisha jumla ya wshiriki 14 kutoka nchi za
Afrika Mashariki na Kati.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya
kuhifadhi Qur’an, Jahuddin Adam, kutoka Sudan,baada ya kutangazwa
mshindi wa fainali hizo, zilizofanyika leo katika Ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akimkabidhi zawadi, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan
Mwinyi, wakati wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur’an,
zilizofanyika leo kwenye ukumbi wa Diamondi Jubilee jijini Dar es
Salaam, na kuwashirikisha washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki
na Kati.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya
Viongozi wa dini ya Kiislamu, wakiwa katika picha ya pamoja na washindi
wa kwanza hadi wa tatu wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur’an,
baada ya kutangazwa washindi katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya
Viongozi wa dini ya Kiislamu, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki
wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur’an, baada ya kumalizika kwa
mashindano hayo katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo.
Picha na Muhidin
Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment