Saturday, August 03, 2013

FUTARI NJEMA

Ni Sunna kuanza kufuturu kwa Kokwa ya Tende au Maji na Unatakiwa Usome Dua ifutayo wakati wa kufungua kwako.

EWE M/MUNGU KWA AJILI YAKO NIMEFUNGA, NA KWA RIZKI YAKO NIMEFUNGUA, KIMEONDOKA KIU , NA LIMELOANA KOO NA YAMETHIBITI MALIPO KWAKO M/MUNGU UKIPENDA.

Na tunajifunza katika Mafundisho kuwa Muda huu wa kufungua tunatakiwa kukithirisha Dua (Maombi) kwa M/Mungu kwani Dua ya Mfungaji hupokelewa kwa haraka sana na sana sana wakati anapofungua.

M/Mungu tunakuomba tuweke katika kundi la wenye kujibiwa Maombi yao. 

1 comment: