Friday, August 02, 2013

KCB BANK WAFUTURISHA JIJINI DAR‏

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba (kulia), akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bara (CCM) Philiph Mangula muda mfupi kabla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya KCB jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni mwenyekiti wa bodi ya KCB Benki Docta Edmund Mndolwa.
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya KCB Moezz Mir akiteta jambo bna Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) muda mfupi kabla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya KCB jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Twaha Taslima, mmoja wa Wanazuoni wa Kiislam walioalikwa kwenye futari.
Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Philiph Mangula akichukua chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania jijini Dar es Salaam jana. Anayemfuatia ni Babu Othman mmoja ya waalikwa wa futari pamoja na Dr Edmund Mndolwa ambaye ni mwenyekiti wa bodi wa benki.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, akisoma hotuba muda mfupi kabla ya kuanza kwa futari liyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya akina mama wakiwa kwenye foleni ya kuchukua chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na benki ya KCB jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye foleni ya kuchukua chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na benki ya KCB Tanzania jijini Dar es Salaam jana mbele kabisa kulia ni Sheikh Abdallah Haroun Nyumba.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, akifurahia jambo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bara (CCM) Philiph Mangula muda mfupi kabla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya KCB jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni mwenyekiti wa bodi ya KCB Benki Docta Edmund Mndolwa.
Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania Dkt Edmund Mndolowa akitoa neon la shukrani kwa wawakilishi kutoka jumuiya za Waislamu walioshiriki katika futari iliyoandaliwa na benki yake jijini Dar es Salaam jana.