Katika Kuwaaga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuingia Sikukuu ya
Eid El Fitri Mama Salma Rashid Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete ametoa wito kwa Kina Mama Nchini
kuishi kwa Upendo , umoja na mshikamano hatua itakayosaidia
kuimarisha hali ya amani na utulivu.
Wito
huo umetolewa na Mama Salma wakati wa futari
ya pamoja aliyoiandaa kwa ajili ya wanawake viongozi na wake wa
viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mama Salma alisema hakuna dini hata moja inayowafundisha watu wake kuishi
maisha ya chuki bali dini zote zinasisitiza kuishi kwa amani, umoja, na
upendo jambo ambalo litamfanya binadamu aweze kumfikia Mwenyezi Mungu.
“Bila
ya kuangalia itikadi zetu tulizonazo, sisi kama viongozi na wake wa
viongozi tutumie nafasi tuliyonayo kuzungumza kwa vitendo maneno matatu
ya upendo, amani na mshikamo ili jamii yetu iweze kuiga mfano kutoka
kwetu”, alisema Mama Salma.
No comments:
Post a Comment