Thursday, August 01, 2013

MIRADI YA RAMADHANI


Je unataka kikingwa na kiu y siku ya kiyama kwa miaka 50,000?ukifunga siku moja ya ramadhani ina maana unafunga takriban masaa 14 sawa na sekunde 50,000 ambazo utakingwa n kiu ya kiyama kwa miaka 50,000.Hii ina maana sekunde moja ya ramadhani ni sawa na mwaka mzima wa kugingwa na kiu na joto la siku ya kiyama.[hadiith]

JE UNATAKA KUWA MILIONEA?
Je unajuwa katika siku za kawaida ukihitimsha qurani yote una andikiwa mema 3,300,000 kwa sababu kila herufi moja unalipwa mema kumi.Malipo ya kusoma qurani ndani ya mwezi wa ramadhani ni sawa na mtu anayefanya umra ndani ya mwezi wa ramadhani ambayo malipo yake inakuwa sawa na kuhiji pamoja na mtume s.a.w. Ikiwa malipo ya umra ndani ya mwezi wa ramadhnai ni kubwa kiasi hicho je malipo ya kusoma qurani ndani ya ramadhani yatakuwa vipi?

TARAWEHE
Soma na pitia juzuu itakayosomwa ndani ya swala ya tarawehe kabla.Utapata kuelewa zaidi pindi utakaposikiliza.Ukiweza pia pitia tafsiri ya kipande kitakacosomwa.Hii itakupa tatdabur zaidi na utapata fadhila mara mbili.moja ya kujisomea wewe mwenyewe na pili ya kusikiliza kwa makini.


 HAZINA ILIYOP0TEA
Usipoteze mda baada ya futari.Unaweza kabisa kusoma angalau juzuu moja.Ukifanya hivyo utaweza kuhitimisha quran yote katika mda huo pekee.Usipoteze hazina hiyo kwa vitu visivyo na maana.

UNASUBIRI KITU GANI?TUBU.
Toa ahadi kwa Allah s.w ndani ya ramadhani kutubia madhambi yako.Kwa mfano siku ya kwanza acha sigara.siku ya pili epukana na ikhtilati[kukaa na mwanamke asiyekuwa mahram wako].siku ya tatu weka azma kutosikiliza tena miziki na nyimbo.Siku ya nne futa toka kwenye simu zako na computer yako kila kinachoweza kukuletea ghadhabu za Allah.s,w. Jaribu kutumia mitandao ya intaneti na televisheni kwa manufaa ndani ya ramadhani na siku za baadae.

UNASUBURI KITU GANI DADA?TUBU
Ewe dada muisilamu.jisitiri kwa vazi la hijab lenye sifa kamili.Usipoteze rehema za Allah s.w katika siku ambazo milango zote nane za pepo na milango zote saba za mbingu zipo wazi.Ukikosa rehema za Allah s.w kipindi hichi utapata lini tena?

IBADA YA USIKU
Kila usiku wa ramadhani Allah s.w anashuka hadi mbingu ya chini kasha anauliza:Je kuna yeyote anayetaka msamaha nimsamehe?Je kuna yeyote anayehitaji riziki nimrizuku?Je kuna yeyote mwenye mazito nimfanyie wepesi?Je kuna mwenye hili na lile nimtatulie?Hadi kunapopambazuka.Hadithi hii imetajwa na ibn maajah na kusahihishwa na Al-Albani.Allah s.w anashuka hadi mbingu ya chini inapofika thuluthi ya mwisho kila usiku mwaka mzima.Lakini ifikapo mwezi wa ramadhani,Allah s.w anashuka ifikapo tuluthi mbili ya usiki yaani kuanzia saa nne ya usiku badala ya saa nane siku za kawaidaElewa ewe ndugu muisilamu usiku wa ramadhani ni fursa kubwa kupata msamaha na dua zako zikajibiwa.Usitafute usingizi kwa nguvu.Jikurubishe kwa Allah s.w.Mda ni mfupi.Malipo ni makubwa.

PIGA MOYO KONDE.
Anza kila siku ya ramadhani kwa ari na moyo.Weka nia inshaallah leo utapata kukombolewa kutokana na moto wa jahannam Allah s.w atukombowe sote.Leo jipinde kuliko jana na juzi.Weka azm leo ni leo.Mla ni mla leo mla jana kelani?
HIJJA SABA
HIJJA TANO,Je Junajuwa kila unapotawadha na kujibu adhana kasha ukaelekea msikitini unapata malipo ya hajj?[sahiih al-jaami.imesahihishw na Al-Albani] Katika swala tano utapata hijja tano.
HIJJA NYINGINE.Yeyote atakayeswali swala ya alfajiri pamoja na jamaa kisha akakaa akimdhukuru Allah s.a hadi kupambazuke kasha akaswali rakaa mbili za ishraaq anaandikiwa malipo ya hajj na umra iliyo kamili..[sahiih al-jaami] hii ina maana utapata malipo ya hijja na umra 30 ndani ya ramadhani ukujipinda kuswali ishraaq.
HIJJA NYINGINE:Imepokewa atakayehudhiria darsa ya elimu anapata malipo ya hajj.Hivyo basi baada ya swala za jamaa usikose darsa zinazoendelea miskitini.
Kila siku una fursa ya kupata hijja saba.ndani ya mwezi wa ramadhani jipatie hijja  210..hii si mzaha wala si habari za bingo.Ni  habari za ukweli

FUNGUO ZA HAZINA YA ALLAH S.W
Je unajuwa kila mchana wa ramadhani una fursa ya kujibiwa dua na kukombolewa na moto wa jahhanam?Je unajuwa kila usiku wa ramadhani una fursa ya kujibiwa dua na kukombolewa na moto wa jahhanam?Unazo fursa 60.Matatizo yako 60 inaweza ikatatuliwa ndani ya ramadhani.Ndoto zako 60 zinaweza zikatatuliwa ndani ya ramadhanii.Kila muisilamu na dua musjaba siku na usiki wa ramadhani[sahiih al-jaami]Fikiria kama tajiri Fulani amekupa cheki tupu wewe ujaze kiasi unachotaka.Ungefurahi vipi?Kumbuka kubeba kitabu cha dua zilizopokelewa au omba kheri ya dunia na akhera.usipoteze hazina hizi.Funguo unazo..

LAYLATUL QADR
Usiku wa laylatul Qadr una masaa 12 ambazo ni bora kuliko miezi 1000,yaani bora kuliko masaa 720,000.Katika usiku huu saa moja ni bora kuliko masaa 60,000 za kawaida.Aya moja ya qurani ina malipo zaidi kuliko aya 60,000.siku za kawaida.Rakaa moja ni bora kuliko rakaa 60,000 ya siku za kawaida na kadhalika.Bila shaka mtu akinyimwa fadhila hizi amenyimwa kitu kikubwa mno.Kwa hakika ni usiku wa maisha ya kweli.Tumia kila sekunde ya usiku huu katika kheri.Waalike watu futari.Wajulie hali ndigu na jamaa zako.Swali kadri uwezavyo.Wasamehe wote waliokukosea.Unganisha udugu na waliokukata.Zidisha kheri.

PATA FADHILA YA KUWA SAHABA
Umra ndani ya ramadhani ni sawa na kuhiji pamoj na mtume s.a.w[sahih al-bukhari]Umra ndani ya ramadhani pekee ndiyo inaweza kukupa fadhila ya kuwa sahaba.Kama Allah s.w amekupa uwezo usipoteze mda,Fanya hima kufanya umra ndani ya Ramadhani.

 ZIDISHA RIZIKI NA MAISHA YAKO.
Je unamatatizo ya upungufu wa riziki?Je unahitaji kupata watoto?Mke mwema?Mume mwema?Unahitaji kurefusha maisha yako tena yenye afya?Wajulie hali ndgugu na jamaa zako.silatul rihim[kuunganisha udugu inazidisha riziki na kurefusha maisha.[bukhari]

 KASRI 30 PEPONI.
Usikose rakaa 12 za sunnah kila siku.2 kabla fajr,4 kabla ya adhuhuri,2 baada ya adhuhuri,2 baada ya magharibi na 2 baada ya ishai.kila unapopata rakaa hizi 12 unajengewa kasri peponi.Ndani ya mwezi wa ramadhani jijengee kasri 30.

FUTURISHA.
Ukimfuturisha aliyefunga unapata fadhila ya funga ya siku moja kama yeye.Kila jema inalipwa kwa uchache mara 10.Hivyo ukiwafuturisha wato 36 kwa mfano unaandikiwa fadhila ya funga ya siku 360 sawa na mwaka mzima.usisahau mkoba wako wa tende na maji.Wafuturishe watu njiani na pia waalike nyumbani kwako.Usiogope kuwafurisha watu,,Bomoa kuta za ubakhili..utashangaa kuona chakula cha wawili  kinawtosha wanne..

LINGANIA
Allah s.w aliwapa nusra waisilamu katika vita vya badr ndani ya ramadhani.Makka pia iliunguliwa na kusalimu amri ndani ya mwezi wa ramadhani.Je wewe utafunguliwa nini ndani ya mwezi huu? Ramadhani ni mwezi wenye Baraka.Mioyo ya watu yanakuwa laini.Watu wapo tayari kusikliza.Tumia fursa hii kusambza juzuu,misahafu,kanda na makala mazuri kwa kila mtu.Tumia mda wako,nguvu zako na pesa zako kuwalingania watu kwa kuwamrisha mema na kuwkataza mabaya.usisahau kuwalingania wasiokuwa waislimu huenda Allah akwapa hidaya kwa ajili yako.

ITIKAFU.
Jipinde kufanya itikafu siku 10 za mwisho.malipi na matunda yake ni makubwa.Ni shule na darsa  ya ajabu itakayo zidisha imani yako.Hata kama huwezi kukaa siku zote basi angalau siku kadhaa kati ya siku hizi 10 za mwisho..kama huwezi kabisa basi angalau siku ya laylatu qadr.Allah s.w atutakabalie ramadhani yetu.Allahuma Amiin.

No comments:

Post a Comment