Tuesday, August 06, 2013

MWEZI MTUKUFU WA  RAMADHANI UNATUAGA .
Siku zenye kuhesabika zilizopita tulikuwa tuna hesabu zimebaki siku kadhaa tuanze kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani , Mwezi Mtukufu ukaingia tukaanza kufunga kuanzia Moja Mpaka leo tumetimiza siku 28.

Sekunde, Dakika , Saa , Masaa , Siku , Wiki , Mwezi , Mwaka kila kikipungua katika hivyo tulivyo viorodhesha na Umri wetu wa Kuishi Duniani Unapungua.

Ndugu yangu Mpendwa tumuombe M/Mungu atudumishe katika Mema na apokee Maombi yetu na Funga zetu.

Na tumuombe Mwisho wa Uhai wetu uwe Mwema , Awarehemu wazazi wetu na Waumini wote.

hatujui Mimi na wewe lini na wakati gani utakuwa Mwisho wetu huenda ukawa huu ndio Mwezi wa Ramadhani wetu wa Mwisho tulie kwa  Mola wetu  atusamehe Waja wake.

Nawatakia Funga Njema na Maandalizi Mema ya Eid - El Fitri.

No comments:

Post a Comment