NILICHOKUKATAZENI KIEPUKENI.

Kutoka kwa Abu Hurayra Abdur Rahman Ibn Sakhr Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake alisema kuwa nimemsikia Mtume Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani akisema:
Kile
nilichokukatazeni kiepukeni, Na kile nilichokuamrisheni fanyeni kwa
wingi kadiri muwezavyo. Hakika kilichowaangamiza watu wa Umma
zilizopita, ni masuala (mahojiano) mengi na kupingana na Mitume yao.
Hadithi hii Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim
No comments:
Post a Comment