VIJANA Sita wilayani Kyela mkoani Mbeya wamefikishwa Mahakama
ya Wilaya ya Kyela kujibu mashtaka manne wanayokabiliana kutokana na vurugu walizozifanya
msikitini, ambapo Sheikh Mkuu wa Wilaya Kyela, Nuhu Mwafi lango na waumini wengine
walipigwa na kuumizwa.
Tukio hilo lilitokea wakati wa Sikukuu ya Idiel- Fitr, wakati sheikh huyo akiongozwa swala. Wakisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kyela, Joseph Luambano, ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Nicholaus Tiba kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa manne.
Ilidaiwa kuwa kosa la
kwanza ni kula njama za kutenda kosa, kufanya vurugu msikitini, kufanya shambulio
la kudhuru mwili na kujeruhi. Alidai kuwa siku ya tukio Sheikh Mkuu wa wilaya
alishambuliwa akiwa anaendesha swala ambapo katika tukio hilo watu wengine, akiwemo mtunza hazina wa
msikiti, Hamisi Hussein, alijeruhiwa kichwani.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni Ibrahimu shaban (17), Ambokile Mwangosi (19), Sadick Abudul
(28), Mashaka Kassimu (30), Ahmed Kassimu (35 ) na Issa Juma (37). Alidai kuwa watuhumiwa
hao wanakabiliwa na makosa hayo. Watuhumiwa wote walikana mashtaka wanayokabiliana
nayo na upande wa mashtaka uliomba mahakama hiyo isiwapatie dhamana watuhumiwa
ili wasivuruge ushahidi. Watuhumiwa walirudishwa rumande hadi hapo kesi yao itakapotajwa tena
Agosti 26, mwaka huu ambapo shauri lao litasikilizwa tena
No comments:
Post a Comment