Uislamu ni mojawapo kati ya dini kubwa nchini Tanzania.
Baadhi ya watu wanakadiria kuwa kwa mwaka wa 2007, dini hiyo imekuwa zaidi ya 50% ya idadi ya wakazi wa Tanzania bara (NA ZAIDI ) ila Takwimu hii ni kwa Mujibu wa Wikipedia (Tanganyika) na zaidi ya 99% jumla ya wakazi wa Zanzibar imekadiriwa kuwa Waislamu.
Historia
Ushahidi hasa wa uwepo wa awali wa Uislamu katika Afrika Mashariki
ni uanzilishwaji wa misikiti huko katika kisiwa cha Shanga na Pate
ambapo machimbo ya dhahabu, fedha na kopa ambapo sarafu zake ziliokotwa
zenye tarehe za kuanzia 830 wakati wa machimbo hayo kwenye miaka ya
1980.
Historia ya Uislamu nchini Tanzania imeanza kunako miaka ya 960-1000 AD, wakati Ali ibn al-Hassan Shirazi alikuwa mmoja kati ya watoto saba wa kiume wa Shah wa Shiraz,
Uajemi, mama'ke ani mtumwa wa Kihabeshi. Kufuatia kifo cha baba'ke, Ali
alitimuliwa na kunyimwa urithi na ndugu zake. Kachukua jahazi lake
kupitia Hormuz,
Ali ibn al-Hassan Shirazi, na kikundi kidogo cha wafuasi wakafanikiwa
kufanya mapumziko yao ya kwanza mjini Mogadishu, bohari la kibiashara
katika pwani ya Afrika Mashariki.
Miji Mikuu ya Afrika Mashariki, iliyotaliwa na Usultani wa Kilwa. |
Wakaendesha jahazi lao kuelekea pwani ya Afrika, Ali ibn al-Hassan
Shirazi kasema anataka kununua kisiwa cha Kilwa kutoka kwa mfalme wa
Kibantu aliyeitwa 'Almuli' na kuunganisha sehemu ndogo ya daraja la nchi
kavu ambalo linaonekana wakati wa maji madogo. Mfalme yule alikubali
kuiuza Kilwa kwa bwana Ali ibn al-Hassan Shirazi kwa nguo zenye
rangirangi na hariri kwa lengo la kupendezesha kisiwa hicho. Mara baada
ya kuinunua Kilwa, Washirazi wale wakaanza kuchimba daraja mpaka wa nchi
kavu, na Kilwa ikawa sasa kisiwa na baadaye yakawa makao makuu ya Usultani wa Kilwa.
Wakati wa umaarufu wake wa nguvu kunako miaka ya 1300-1400, Usultani wa Kilwa ukamiliki au ukadai umiliki wa miji ya bara kama vile Malindi, Sofala na nchi za visiwa kama vile Mombassa, Pemba, Unguja, Mafia, Comoros na Inhambane - kwa lengo la kutawala ambapo sasa hivi hutajwa kama Pwani ya Waswahili.
Jengo ambalo la zamani na bado lipo zima Afrika Mashariki ni Msikiti wa Kizimkazi huko mjini kusini mwa Unguja
tangu mwaka 1107. Inaonekana ya kwamba Uislamu ulikuwa una enea kwa
haraka zaidi katika maeneo ya Bahari ya Hindi kunako karne ya 14. Wakati
Ibn Battuta
katembelea Afrika Mashariki mnamo 1332, ameripoti kujisikia kama yupo
nyumbani kwa sababu ya Uislamu ulioenea katika maeneo hayo.
Kawaida ya idadi kubwa ya wakazi wa pwani ilikuwa Waislamu, na Kiarabu
ilikuwa lugha ya kufundishia na vilevile ya kiabishara. Bahari yote ys
Hindi ilipata kuonekana kama vile bahari ya Kiislamu. Waislamu walishika
hatamu katika biashara na uanzashwaji wa makazi katika pwani ya Kusinimashariki mwa Asia, India na Afrika Mashariki.
Uislamu ulienea hasa kwa njia ya shughuli za kiabisha katika pwani ya
Afrika Mashariki, sio kwa ushindi na uenezi wa mabavu kama jinsi
ilivyokuwa huko Kaskazini mwa Afrika,
na ikabaki kama pwani ya ajabu kwa muda mrefu. Wakati wa uvamizi wa
mabavu wa Wareno katika maeneo ya pwani yaliyotokea mnamo karne ya 16,
Uislamu ulikuwa tayari ushajikita vya kutosha karibia kila familia
ilikuwa imeungamana na Uarabu, Uajemi, Uhindi na hata kuungana kisiasa na Kusinimashariki mwa Asia na baadhi ya sehemu za kaskazini na mashariki mwa Bahari ya Hindi.
Mwishoni mwa karne ya 17 na mwanzoni mwa karne ya 18, Waislamu wa pwani waliweza kuwatimua Wareno kwa msaada wa Oman. Waomani wakaongeza athira ya kisiasa hadi hapo mwishoni mwa karne ya 19 ambapo Wazungu walipoanza kuwasili katika pwani ya Afrika Mashariki.
Wakati wa Oman inatawala pwani hiyo kisiasa, uenezi wa wa Uislamu uliongezeka pia ndani ya Afrika Mashariki.
Mawasiliano ya kibiashara na watu wa ndani, hasa Wanyamwezi, na kuanza
kupewa umuhimu kwa sehemu kama za Tabora katika maeneo yenye Wanyamwezi na Ujiji katika Ziwa Tanganyika ikawa kitovu kikuu cha uongezaji wa biashara ya utumwa na pembe za ndovu.
Machifu wengi, hata sehemu za Uganda,
wamesilimu na kuwa Waislamu na kuanza kushirikina na Waislamu wa pwani.
Biashara ya utumwa haijasaidia kueneza Uislamu tu, bali pia lugha ya
Kiswahili na tamaduni ya Waswahili. Kabla kuanzishwa kwa Afrika Mashariki ya Kijerumani kunako miaka ya 1880 athira za Waswahili zilikuwa na kikomo hasa waliishi katika maeneo yao tu walioyazoea.
No comments:
Post a Comment